NECTA yasitisha mtihani wa udahili kwa kidato cha kwanza

ENANTIOMER

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
1,419
804
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za sekondari za serikali uliokuwa ufanyike Februari 28, mwaka huu.

Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Salumu alisema hayo juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.

Salumu alisema mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi hao ulitokana na matakwa yaliyowasilishwa Necta na baadhi ya wakuu wa shule za serikali wakipendekeza kupitia maofisa elimu wa mikoa na wilaya kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa na kupangiwa shule zao wengi hawana sifa na uwezo wa kumudu masomo.

Naibu Katibu Mtendaji wa Necta alisema wakuu wa shule walikuwa wakiomba kupata idhini ya kuwafanyia mtihani wanafunzi ili kubaini uwezo wao na kwamba baraza liliwasiliana na maofisa elimu mkoa na wilaya likiwataka kuwasilisha orodha ya idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kwenye shule ya zao.

Alisema baada ya kufahamika idadi ya wanafunzi hao, baraza ndilo litatunga maswali ya mitihani yenye kuzingatia mfumo na vigezo maalumu na kutumiwa wakuu wa shule hizo ili kuusimamia kwa lengo la kuweka uzani sawa wa mtihani huo.

Alisema moja ya masharti ni kwamba mtihani huo ulitakiwa ufanyike kwa wanafunzi wa kidato hicho kwa shule zote za serikali siku moja na kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo, alisema baada ya kuwatumia masharti hayo, wakuu wa shule hizo walishindwa kuwasilisha orodha ya wanafunzi kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya ili itumwe Necta na kutokana na mazingira hayo, baraza limeamua kusitisha kuwadahili wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuitaka mamlaka inayosimamia elimu kuendelea na utaratibu wao wa kawaida.

“Necta imewasiliana na wahusika kwa barua rasmi ya kusitisha mtihani huo ambao ulipangwa ufanyike Februari 28, mwaka huu na wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha kwanza shule mbalimbali za serikali zikiwemo za bweni, waendelee na masomo kama yalivyopangwa,” alieleza Naibu Katibu Mtendaji wa Necta.

Novemba mwaka jana, serikali ilitangaza kuwa wanafunzi 526,653 sawa na asilimia 94.8 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza huku 28,638 wakishindwa kupangiwa shule katika awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 268,052 sawa na asilimia 94.5 ya wasichana waliofaulu na wavulana ni 258,601 sawa na asilimia 95.2 ya wavulana waliofaulu.

Chanzo: Habari Leo
 
Niliyashangaa maamuzi ya ajabu ya NECTA,mwanafunzi amefaulu na amepangiwa shule ya serikali na sasa anajiandaa kuripoti shule mpya ya sekondary unamwambia kuna mtihani mwingine,,,,,,,,hii ni aibu kwa Taifa na wizara kwa ujumla.Watoto waende wakasome form 1 kama kuna mtu hana uwezo atabaki form 2 baada ya mtihani wa kwenda form 3 kufanyika.
 
kwanza wanatakiwa kukaza darasa la saba, kisha wakaze kidato ccha pili ili kupata wenye sifa.
Siku hizi ukipata D mbili kidato cha pili, unakua kipanga mwenye akili na uliyefaulu vizuri na kuingia kidato cha tatu. sasa hapa napata shida kama kwa upimaji huu wa D mbili wa kidato cha pili, utaweza kuchuja vilaza kweli!!
 
Niliyashangaa maamuzi ya ajabu ya NECTA,mwanafunzi amefaulu na amepangiwa shule ya serikali na sasa anajiandaa kuripoti shule mpya ya sekondary unamwambia kuna mtihani mwingine,,,,,,,,hii ni aibu kwa Taifa na wizara kwa ujumla.Watoto waende wakasome form 1 kama kuna mtu hana uwezo atabaki form 2 baada ya mtihani wa kwenda form 3 kufanyika.

hahahaha mkuu kwani mtihani wa form 2 kwenda 3 bado una maana kama zamani, sasa hata upate F zote ni kwenda tu.

elimu ilisha kufa zamani mkuu
 
Suala la kuuondoa mtihani huo wa feb 28, binafsi siafikiani nalo kwa kuwa ule mtihani wa darasa la saba ulikuwa na maswali ya kuchagua kwa kusiliba tu na kalamu ya risasi, hakukuwa na swali hata moja la kukokotoa au kuandika walau sentensi moja, kwa mwanafunzi ambae hajui kusoma na kuandika ni rahisi kufaulu kwa mitihani ile.
 
kwahiyo unapendekeza nini kuhusu mitihani ya darasa la saba? maana wakiacha kama ulivyo, basi kila mwaka kutakua na mtihani wa mchujo wa kidato cha kwanza, hivyo mtihani wa darasa la saba unakua kama hauna kazi na ni hisara tu kuuendesha. shauri kitu kuokoa kodi zetu, au kodi zetu zitumike kiusahihi.
 
kwahiyo unapendekeza nini kuhusu mitihani ya darasa la saba? maana wakiacha kama ilivyo, basi kila mwaka kutakua na mtihani wa mchujo wa kidato cha kwanza, hivyo mtihani wa darasa la saba unakua kama hauna kazi na ni hisara tu kuuendesha. shauri kitu kuokoa kodi zetu, au kodi zetu zitumike kiusahihi.
Warudishe mfumo wa mitihani waliyoiondoa ambayo inampima mwanafunzi ktk nyanja zote za kitaaluma, pia uchunguzi ufanyike ili kumuwajibisha aliesimamia mitihani hii ya kusiliba, inaonekana sio mtu mwema ana lengo hasi la kuua elimu ya watoto wetu.
 
uchunguzi huu sijui utakua unamtafuta nani? waandaaji wa mitihani, wasimamizi wa mitihani, walimu wakuu, au wanafunzi wanaotazamia maajibu maana nirahisi sana kutazamia au kusaidia ktk mitihani hii ya kuchagua majibu ktk maswali yote!!!
 
Naibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Salumu ametangaza kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, NECTA limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za sekondari za serikali.

Usitishaji huo umetokana na wakuu wa shule za serikali kushindwa kukidhi baadhi ya masharti yaliyotolewa na NECTA, mazingira yaliyopelekea NECTA kusitisha zoezi la udahili wa wanafunzi hao wanatakiwa kujiung na masomo kidato cha kwanza.

Ambapo NACTE iliwataka wakuu wa shule kuhakikisha mtihani huo unafanyika kwa wanafunzi wote wa shule za serikali siku moja na muda uliopingwa, pia masharti yaliwalazimu wakuu wa shule za serikali kuwasilisha orodha ya majina ya wanafunzi kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya ili yatumwe NECTA.

Mazungumzo hayo yalifanyika juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.

Back
Top Bottom