NECTA yaonya udanganyifu mitihani ya kidato cha 6 inayoanza leo Mei 9, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Watahiniwa 95,955 wa kidato cha sita wanatarajiwa kuanza mitihani ya Taifa leo Mei 9, 2022 na wakitarajiwa kumaliza Mei 27, 2022 ambapo washiriki wanatoka katika shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250.

Kuelekea kuanza kwa mitihani hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza za Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde ameonya juu ya vitendo vyovyote vya udanganyifu.

Amesema baraza halitosita kukifutia kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa kinahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.

Dk Msonde alisema mitihani ya kidato cha sita ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwani hupima maarifa, stadi na umahiri wa wanafunzi katika yote waliyojifunza ndani ya miaka miwili.

"Baraza linatumia nafasi hii kuwataka wamiliki wa shule wote kutambua kuwa shule ni vituo maalumu vya mtihani hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote.

"Mtihani wa kidato cha sita ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwani upima maarifa, stadi na umahiri wa yale waliyojifunza katika kipindi cha miaka miwili ya elimu ya sekondari ya awamu ya juu," alisema.

Ameongeza kuwa watahiniwa 85,531 ni wa shule wakati 10,424 ni watahiniwa wa kujitegemea. Kati yao wanaume ni 47,859 sawa na 55.9% wakati wanawake apo 37,672 sawa na 44%.
 
Waimarishe ulinzi haswa kwenye hizi shule zenye majina makubwa............ili tujue ni kweli huwa wanafaulu kiuhalali au wananunua Mitihani?
 
••••••Kati yao wanaume ni 47,859 sawa na 55.9% wakati wanawake apo 37,672 sawa na 44%.
Kweli hisabati ni janga la kitaifa! Hii inaonesha kuna watahiniwa 96 ambao siyo wanaume au Wanawake yaani asilimia 0.1. Hii ni kutokana na jumla ya 55.9 na 44 ni sawa na 99.9. Ili ikamilike kuwa 100 ni lazima ijumulishwe 0.1.

Kihesabu ukionesha decimal points lazima ziwe kila upande. Aidha hakuna haja ya kuonesha decimal points kama kuna significant differences. Mfano angalionesha wanaume ni asilimia 56 na Wanawake asilimia 44.

Ikumbukwe kwa matokeo ya form four 2021 ni asilimia 19 tu ya watahiniwa waliopata angalau D ya Maths! Zanzibar ni asilimia 3 tu
 
Eti kuna mahali nimeona eti CCM WANA WATAKIA MTIHANI MEMA WATOTO WETU.
Mie nimekemea hiyo wishes yao kwa mwanangu.

Wakae mbalibkabisa na mwanangu
 
Mkuu, kwani hakuna typing error?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribio la kwanza kwa Prof: Mkenda.
Chonde chonde dhibiti udanganyifu/wizi wa mitihani.

Kuna tetesi kuwa Shule za binafsi zenye majina makubwa zinatabia ya kununua mitihani au hata kuhonga wasimamizi wa mitihani, tunaomba sana mamlaka zinazo husika kuwa macho.........
 
Bongo lazima kuibia mitihani iyo ni biashara za watu utaona tu
 
Eti kuna mahali nimeona eti CCM WANA WATAKIA MTIHANI MEMA WATOTO WETU.
Mie nimekemea hiyo wishes yao kwa mwanangu.

Wakae mbalibkabisa na mwanangu
wanataka kuleta uchuro kwenye maisha ya watu.
 
Bongo lazima kuibia mitihani iyo ni biashara za watu utaona tu
inawezekana lakini inawezekana biashara hiyo inafanywa na shule kubwa zenye uwezo ambazo kila kulicha zinashika 10 bora, hizo ndio lazima ziwekewe uchunguzi wa kina, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viwe macho.
 
Waimarishe ulinzi haswa kwenye hizi shule zenye majina makubwa............ili tujue ni kweli huwa wanafaulu kiuhalali au wananunua Mitihani?
Shule vipaji maalumu ziko aina mbili za kwanza za Serikali ambazo kuchukua beat students kitaifa kwenda Mzumbe au kibaha au Tabora secondary za Serikali

Private wao pia wana mfumo wao wa kuchukua vipaji maalumu walio fanya vizuri shule za binafsi zisizo za Serikali
Hizo shule best performers za private ni shule za vipaji maalumu za watoto waliosoma Private

Mwisho wa siku best performer wanakuwa shule za vipaji maalumu wa Serikali na za binafsi za kanisa au watu binafsi za vipaji maalum
 
Back
Top Bottom