NECTA Yabadili mfumo wa mtihani darasa la saba

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Katibu mkuu wa baraza la mitihani Tanzania Dr
Msonde amesema kuwa kuanzia mwaka huu mitihani ya darasa la saba nchini itakuwa na maswali 40 ya kuchagua pamoja na maswali matano ambayo siyo ya kuchagua.
Msonde amesema hayo leo akiwa katika ofisi za Baraza hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mitihani ya taifa ya darasa la saba inayotarajiwa kufanyika kesho.

“Kabla ya mwaka huu 2018 Mitihani ya darasa la saba ilikuwa na maswali 50 ya kuchagua, wadau mbalimbali wa elimu wakiwepi wamiliki wa shule, Walimu na Wazazi waliliomba baraza lifanye maboresho ya muundo wa mtihani wa darasa la saba yawepo maswali ya kuchagua na yasiyo yakuchagua,” amesema Msonde.

Aidha Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 960, 202 ambapo kati yai Wavulana ni 456, 230 sawa na 47.51% na wasichana 503, 972 sawa na 52.49%.

Amesema kuwa kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 43, 130 (4.7%) kwa mwaka 2018 ukilinganisha na 2017 ambapo watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba walikuwa 917, 072.

“Watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka 2018 kati yao 918, 653 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na Watahiniwa 41, 549 watafanya mtihani kwa lugha ya Kingereza ambayo wameitumia katika kujifunzia,” amesema.

Pia amesema kuwa kati yao watahiniwa wasioona ni 90 wakiwemo wavulana 59 na wasichana 31 huku wenye uoni hafifu wakiwa ni 846 ambao kati tai wavulana ni 475 na wasichana 371.

Mitihani hiyo itakayofanyika Tanzania Bara itafanyika kwa siku mbili mfululizo ambapo itaanza kesho Septemba 4 hadi 5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom