NECTA & NACTE jihadharini kutumbuliwa

kukithiri kwa tabia ya watu kufoji na kutengeneza vyeti feki vya baraza la mitihani la taifa ndio chanzo kikuu cha kuonekana elimu yetu haina maana yoyote(inashuka).Hasa sekta binafsi watu wengi wanatumia vyeti visivyo vyao au wamejitengenezea vinavyofanana na vya baraza na wengine wamejitengenezea vya NACTE na elimu ya juu. tunaziomba mamlaka hizi zifanye operation ya kuhakiki vyeti hasa sekta binafsi ili kuimarisha muonekano wa elimu yetu. naamini elimu yetu si dhaifu udhaifu unatokea pale mambo haya yanafumbiwa macho na tasisi hizi za serikali

pengine mambo haya yakiendelea kufumbiwa macho hakutakuwa na haja ya kuwa na vyombo hivi hapa nchini.. hili naliona ni kosa kisheria sasa kwann watu waruhusiwe kuvunja sharia eti kisa sekta binafsi?

Rais wetu mpendwa tumbua haya majipu
1. anaetumia cheti cha mwingine bila kulipa kodi kwa mwenye cheti(huyu ni fisadi pia)
2.anaetumia cheti cha udanganyifu kujipatia kitu( huyu nae ni fisadi)
3. tasisi zinazofumbia mambo haya nazo zitumbuliwe
kumbuka wewe unaetumia cheti cha mtu mwenyewe aligharamia masomo hivyo unapaswa kutoa kodi.
Enzi za ujanja ujanja zimekwisha sasa ni kazi na kulipa kodi
Hapa kazi tu!
 
na wasomi wasiojua wa kiwango cha master na kuendelea wasiojua english nao ni majipu watumbuliwe
 
Kwa nini waziri mwenye dhamana asitoe tamko hili nalo mpaka rais aaaaaaaaahhhhhh wadanganyika wenzangu tumuonee rais huruma
 
na wasomi wasiojua wa kiwango cha master na kuendelea wasiojua english nao ni majipu watumbuliwe
kama hawajafanya kosa la kudanyanya nyaraka za elimu hakuna shida, shida ni udanganyifu ili kujipatia kitu isivyo halali!huu ndio ufisadi mwingine
 
kama hawajafanya kosa la kudanyanya nyaraka za elimu hakuna shida, shida ni udanganyifu ili kujipatia kitu isivyo halali!huu ndio ufisadi mwingine
huko ni kudanganya taifa kuwa umeelimika kumbe wapi
 
Hivi watu wakifoji vyeti nalo ni jipu kwa NECTA na NACTE!!!? Kama ni hivyo basi Bank kuu ya Marekani ni zaidi ya jipu manake hizi dollar zinazokamatwa kuwa ni feki zimetapakaa dunia nzima!!!! Kwa ufahamu wangu NECTA inatoa vyeti vya form 4 na 6, sasa hivi ndio vyeti pekee vinavyofanya mtu apate ajira!!??? Vipi Hizo shahada ya kwanza, uzamili na uzamivu vyenyewe watu hawafoji eeeh!!!!?
 
Ajira zenyewe hakuna, sasa wakiwa na vyeti faki kuna ubaya gan?
huko ni kuvunja sheria..ni tasisi Necta na Nacte zenye mamlaka ya kutunuku cheti kulingana na ulichosoma na sio ovyoovyo tu mtaani unajitengenezea na kukiita eti cheti cha necta au nacte
 
huko ni kuvunja sheria..ni tasisi Necta na Nacte zenye mamlaka ya kutunuku cheti kulingana na ulichosoma na sio ovyoovyo tu mtaani unajitengenezea na kukiita eti cheti cha necta au nacte
Ivi ni lin Watanzania tutaacha kusamini vyeti na kuanza kufuatalia kile mtu anachokijua na uwezo wa mtu kiujumla?.ivi unajua kua kuna form six wanajua kufundisha secondary school kuliko graduate.
 
Ivi ni lin Watanzania tutaacha kusamini vyeti na kuanza kufuatalia kile mtu anachokijua na uwezo wa mtu kiujumla?.ivi unajua kua kuna form six wanajua kufundisha secondary school kuliko graduate.
Kuwa mwelewe hapa hatuthamini vyeti..ila kumbuka taifa lisilo na elimu limekufa..hapa ni kushughulika na udanganyifu ili kulinda kile tunachozalisha (elimu) kisionekane feki pia. kama hujafanya udanganyifu hatunashida na wewe. je umefanya udanganyifu???unatumia cheti cha mwenzio bila kumlipa ???huu ni ufisadi pia!!!!!

lazima vitendo hivi vikomeshwe ili kulinda elimu inayodidimia.. unapotumia cheti cha mtu au feki utatutangaza mahali pote kuwa tunatoa elimu feki ..wengine hata kuandika jina hawawezi na wamezubaaa tu badala sasa ya kujiendeleza ..wamekalia kufanya ufisadi(kutumia akili za wengine na kufoji )
 
Ndugu yangu wenye elimu mzuri na vyeti vya necta ndio waliofikisha nchi kwenye lindi la umaskini. Jaribu kufuatalia elimu za makandarasi waliojenga barabara ivi za mwaka mmoja mashimo kibao. Fuatialia elimu za wakurugenzi hawa wanaotumbuliwa sasaivi.
Fuatialia elimu za hawa wenye mtandao wa wafanya kazi hewa.
Kuna huyu jamaa alikua kamishna wa Kodi alivyofanya madudu.
Hao ndio wenye elimu mzur na halali.

Kwa kifup nchi haijengwi na watu wenye elimu kubwa,Nchi nying wenye elimu ya kati na elimu kawaid ndio waliojenga nchi zao.
Fuatialia China, Singapore. Na Vietnam.
 
Mimi nionavyo kwenye hili la watu kutengeza vyeti fake wa kulaumiwa siyo NECTA au NACTE. Wanaotakiwa kulaumiwa ni wale waajiri au taasisi ambazo zinaajiri watu pasipo kufanya uhakiki wa vyeti vya hao waajiriwa kwa kuvipeleka huko NECTA au NACTE ambao wangeweza kuwapa majibu kama vyeti hivyo ni genuine au fake.

Taasisi husika ikiwa na mkakati wa kuhakikisha kwamba hawaajiri wafanyakazi wenye vyeti fake haiwezi kuona gharama kupeleka vyeti vya waajiriwa wake huko NECTA na NACTE ili kufanyiwa uhakiki.

Pengine kuwepo na sheria inayozibana taasisi za umma au binafsi kuhakikisha kwamba zinahakiki vyeti vya watumishi wake na kama ikigundulika kuwa kuna mwajiriwa mwenye cheti fake katika taasisi hiyo basi kuwepo na adhabu dhidi ya taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mkuu wa taasisi hiyo na maofisa wake wa idara ya HR kwa kuzembea kufanya uhakiki huo.
 
Back
Top Bottom