NEC yatupilia mbali pingamizi la Mgombea wa CCM katika Uchaguzi wa Ubunge Muhambwe

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali pingamizi lililowekea na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muhambwe (CCM) Dkt. AFlorence George Samizi dhidi ya Mgombea wa ACT-Wazalendo, Masabo Julius Joseph, ikisema anaweza kuendelea kuwepo katika Uchaguzi

Katika pingamizi la kutoambatanisha picha zenye muonekano wa rangi nyeupe kwa nyuma, NEC imesema haikuwa sababu ya pingamizi kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, kuhusu hoja kuwa saini za Wadhamini zimeghushiwa, NEC imesema imeshindwa kuthibitisha hilo na hakutaja majina ya Wadhamini anaodai saini zao zimeghushiwa.

62AD7F29-AAD8-4524-81B7-9702CFA885DD.jpeg
689F1F9D-C234-4A92-A134-EA983CE60A98.jpeg
 
Back
Top Bottom