NEC yatangaza uchaguzi kata 27 kufanyika mwezi February mwakani

DR. PHONE

JF-Expert Member
Nov 12, 2012
504
91
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema uchaguzi huo utafanyika katika halmashauri 23 baada ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa.

Alizitaja kata hizo na halmashauri zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).

Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti (Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba), Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na Namikago (Nachingwea).
Kata nyingine ni Partimbo na Loolera (Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na Nyasura (Bunda).

Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9.
 
Mbona kata ya Kisesa haipo, iliyokuwa ya Mabina, aliyepigwa na wapiga kura wake hadi kufa?
 
Tunasubiri watu kufa na kumwagiana Tindikali,Hamna mgombea Uraisi wa Upinzani aliepata kura nyingi kama MREMA,lkn kinachotokea sasa uaribifu wa mali na mauaji, inasababishwa na chama kikuu cha upinzani CDM kupinga kila kitu.
 
Wanaibaga kura sio?
 
Tuache sasa kukesha mitandaoni na kumtukana zitto,twendeni mashinani sasa.tukipata angalau kata 20 tutakuwa na uwezo mzuri kushnda serikali za mitaa 2014. Chini ya hapo ni maumivu
 
kwa sasa chaguzi ndogo siyo ishu tunangoja uchaguzi mkuu ndiyo ishu kwa sasa.
 
msimu mwingine wa kumwagiana tindikali na kulipuana mabomu..! wanasiasa wa nchi hii tuombe Mungu awasamehe...
 
Waambie wakubali kuboresha daftari la wapiga kura - wanaogopa nini chama kikongwe miaka 60 madarakani?
 
Tunasubiri watu kufa na kumwagiana Tindikali,Hamna mgombea Uraisi wa Upinzani aliepata kura nyingi kama MREMA,lkn kinachotokea sasa uaribifu wa mali na mauaji, inasababishwa na chama kikuu cha upinzani CDM kupinga kila kitu.
Nenda hosiptali kacheki mfumo wa kumbukumbu wa ubongo wako inawezekana fusi moja imelegea.
 
Hapa nikitazama chap chap CHADEMA wanaweza kuambulia kata mbili tu!
poor analysis, kuna ukweli kuwa kata za dodoma kwa wagogo, na hizo za pwani kuna tatizo kidogo kwa upande wa CHADEMA na ndo zilizonyingi kwenye orodha lakini huko kwingine CCM itapoteza vibaya
 
Tunasubiri watu kufa na kumwagiana Tindikali,Hamna mgombea Uraisi wa Upinzani aliepata kura nyingi kama MREMA,lkn kinachotokea sasa uaribifu wa mali na mauaji, inasababishwa na chama kikuu cha upinzani CDM kupinga kila kitu.

Mrema alikuwa mpinzani wenu ndo mana mifano yote mrema na bado mtamtaja sana.andaeni minoti ya kugawa kwani nyie uchaguz ni nusu ya vita.sisi jukwaa na mic tu.nyie viti magari ya soda,pilau wasanii mtakoma.
 
Back
Top Bottom