NEC yatangaza tarehe ya Uchaguzi Majimbo ya Simanjiro na Serengeti

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe mbili Desemba kuwa siku ya Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Simanjiro,Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage amesema fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 28 Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.

Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo mawili (2),Jimbo la Serengeti lililopo Mkoani Mara la Mh.Marwa Ryoba na Jimbo la Simanjiro la Mh.JAmes Ole Millya baada ya wabunge hao kuhama Chama chao.
 
Aaah hizi chaguzi tumevunja rekodi ya dunia,tunatakiwa tuingie kwenye world record
 
Siku hizi wanaitisha uchaguzi chap chap ili mnunuliwa asikae muda mrefu bila in flow...!
 
Wangesubiria Baada ya December tutangaze marudio ya Majimbo Kama 18 hivi ikiwemo Mawili ya Dar
 
Waste of time and resorces, huu ni ufisadi wa kutisha. Watu wanaharibu pesa kwenye vitu fake fake fake. Watu weusi tutaendelea kutukanwa na haki yetu. Hivi huyu mhaya Kaijage haoni aibu kusimamia vitu fake?
 
Siku hizi wanaitisha uchaguzi chap chap ili mnunuliwa asikae muda mrefu bila in flow...!
Mngekuwa mnasomaga basi na sheria za uchaguzi zinasemaje Jimbo linapokuwa wazi, badala ya kukurupuka na mineno isiyokuwa na msingi na si muwatulize basi hao wanaohama wabaki kwenye vyama vyao kama kweli walienda huko kwa moyo wa kufia chama na si kutafuta maisha.
 
Waste of time and resorces, huu ni ufisadi wa kutisha. Watu wanaharibu pesa kwenye vitu fake fake fake. Watu weusi tutaendelea kutukanwa na haki yetu. Hivi huyu mhaya Kaijage haoni aibu kusimamia vitu fake?
Kaijage ye ndio anawatoa hao wabunge kwenye vyama vyao
naijiuliza sipati jibu hivi Mke akichukuliwa na Mwanaume mwingine tena jirani yako na anakukana hadharani utamlaumu huyo mwanaume?? au na alikoenda akiamua kuolewa utamlaumu Shekh/Mchungaji kwa nini unafungisha ndoa ya mke alokukimbia na talaka kakupa, na matusi juu tafuteni hoja zenye mashiko Muacheni Kaijage afanye kazi yake kama iliyoelekezwa kwenye sheria za uchaguzi pambaneni na hama hama yenu
 
Afu ni jaji... Mfuko wa pole pole c mchezo
 
Poor argument and out of touch, mwanamke huwa anajitongoza au huwa anatongozwa na mwanaume? Je kwa nini mwanaume akifumania huwa anaua mwanaume aliyemkuta na mke wake? kwa nini asiue huyo mwanamke?
Kama hufahamu imeandikwa mwanaume usimtamani mke wa jirani yako kwa hiyo toka awali inajulikana anayemtamani mke wa mtu ndo mwenye makosa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom