NEC yatangaza Ratiba ya Chaguzi ndogo nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC yatangaza Ratiba ya Chaguzi ndogo nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donatila, Dec 7, 2016.

 1. Donatila

  Donatila JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2016
  Joined: Oct 23, 2014
  Messages: 2,184
  Likes Received: 2,156
  Trophy Points: 280
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uchukuaji wa fomu za kujaza nafasi zilizo wazi ya Mbunge na Madiwani katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

  Imesema kuwa inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Dimani , Mkoa wa Mjini Magharibi ,Tanzania Zanzibar kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Tume hiyo, hatua hiyo itanatokana na vifungu vya 37(1)(b) na 46(2) vya sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 13(3) na 48(2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292.

  Aidha ,Tume hiyo pia itaendesha Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi za wazi za Udiwani katika kata 22 kwenye baadhi ya Halmashauri za Tanzania Bara zilizokuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

  Imezitaja Kata hizo Ng’hambi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ihumwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Kiwanja cha Ndege ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Igombavanu na Ikweha za Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa pamoja na Ngarenanyuki iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha.

  Kata nyingine ni Kijichi ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam, Kata ya Kinampundu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida, Isegehe ya Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, Kasansa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi, Malya na Kahumulo Mkoani Mwanza, Maguu na Tanga Mkoani Ruvuma pamoja na Kata ya Kimwani Mkoani Kagera.

  Imeongeza kuwa Kata nyingine ni pamoja na Nkome Mkoani Geita, Kata ya Lembeni Mkoani Kilimanjaro, Mkoma ya Mkoani Mara, Duru ya Mkoani Manyara, Mwamtani ya Mkoani Simiyu, Misugusugu ya Mkoani Pwani pamoja na Mateves ya Mkoani Arusha.

  Tume hiyo imesema kuwa zoezi la kutoa fomu za uteuzi litaanza Desemba 10 hadi 22 na kufuatia kwa zoezi la uteuzi wa wagombea siku ya tarehe 22 mwezi Desemba na Desemba 23 hadi Januari 21 mwakani itakuwa ni kipindi cha kampeni ambapo Januari 22 mwakani itakuwa siku ya kupiga kura.
   
 2. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2016
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,074
  Likes Received: 15,725
  Trophy Points: 280
  Wenyeviti wa mitaa/vijiji ambao walifariki au kutenguliwa matokeo yao, naona halmashauri zimekaa kimya sijui hawana mpango wa kufanya uchanguzi
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2016
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Tuone sasa ngoma itakavyokwenda, kuwe na fair ground tu
   
 4. habari ya hapa

  habari ya hapa JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2016
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 10,127
  Likes Received: 5,424
  Trophy Points: 280
  Wasira akachukue fomu
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Hakuna siasa hadi mwaka 2020.Mgombea unachukua fomu hakuna kuomba kura kwa wananchi unabandika karatasi na wasifu wako inatosha.
   
 6. Shukrani A. Ngonyani

  Shukrani A. Ngonyani Verified User

  #6
  Dec 7, 2016
  Joined: Feb 23, 2014
  Messages: 1,012
  Likes Received: 1,219
  Trophy Points: 280
  kwa hyo wataruhusu kampeni huru?
   
 7. eden kimario

  eden kimario JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2016
  Joined: Jun 13, 2015
  Messages: 5,927
  Likes Received: 9,107
  Trophy Points: 280
  Hii tume nayo ni jipu tu
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2016
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kampeni zipo tume imesema
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2016
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Msimu wa CCM kugaragazwa tena
   
 10. Nnangale

  Nnangale JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2016
  Joined: Jul 20, 2013
  Messages: 1,240
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Ya kata gani?
   
Loading...