Uchaguzi 2020 NEC yatangaza Nchi na Taasisi zilizoruhusiwa kuwa watazamaji (Observors) wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,245
24,108
29 September 2020
Arusha, Tanzania


Source: video : Global online TV

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia kwa mkurugenzi wake, Dkt Willson Mahera, leo Septemba 29, wamezungumza na wanahabari na ili kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 28 mwaka huu.

Aidha, katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Uchaguzi ameweka bayana kuwa Tume ya Uchaguzi imetoa kibali kwa asasi zipatazo 245 za kutoa elimu ya Mpiga kura kwa upande wa Tanzania Bara wakati Zanzibari asasi 7. Akifafanua kuhusu hili Mahera amesema asasi hizi zilipewa kibali kutokana na kukidhi vigezo na baadhi ya asasi hizo zimeshaanza kutoa elimu kwa mpiga kura.

Zaidi ya hayo, Charles Mahela anaweka bayana kuwa Tume imeruhusu kuwepo na Watazamaji wa ndani na nje katika uchaguzi Mkuu ambapo Watazamaji wa ndani na asasi za kiraia ni Taasisi 97 wakati watazamaji wa nje zimekwishafika asasi 18 na miongoni mwa hizo ni nchi mbalimbali kama vile Marekani, Japani, Uholanzi, Ujerumani, Ubelgiji, Denmak Sweden nchi hizo zimepata kibali cha kutazama.

Aidha, Mahela ameongeza kuwa ushirikishaji mwingine wa wadau katika Uchaguzi Mkuu utakuwa kupitia Mawakala wa Vyama vya Siasa ambapo siku ya Uchaguzi vyama vya siasa vitapewa fursa ya kuweka mawakala katika kituo cha kupigia kura, wakala katika kituo cha kuhesabia kura na wakala katika kituo cha Kutangazia matokeo. Hivyo, amesisitiza kuwa katika vyumba vya kupigia kura sio Tume tu inakuwepo bali kunakuwa na mawakala na wasimamizi.

Sambamba na hayo, Mkurugenzi wa Tume amesisitiza Wagombea kuzingatia maadili ya Uchaguzi na kuepuka kufanya vitendo ambavyo vitaharibu amani ya nchi. Aidha, mahela amewasisitiza Wananchi kutojisahau kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi sheria za nchi hazijasimama hivyowanapaswa wajiepushe na vitendo ambavyo vitakiuka sheia za nchi.

===
NEC: WENYE MAHITAJI MAALUMU WAMEANDALIWA MAZINGIRA RAFIKI KUSHIRIKI UCHAGUZI

Mkurugenzi Mkuu wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, Dkt Charles Mahera amesema watu wenye mahitaji maalum watapewa kipaumbele kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28
-
Watu wenye mahitaji maalumu kama walemavu na wajawazito, wanaonyenyesha, waliokwenda na wazee na wagonjwa watapiga kura mapema na kuondoka

Watu wasiojua kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini. Wasiokuwa na uwezo wakuona watawekewa maandishi ya nukta nundu au wanaweza kwenda na wanaowaamini kuwasaidia

Aidha wenye ulemavu wowote ule pia atawezeshwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo. Maelezo hayo yote yameshatolewa kwa wasimamizi wa vituo vya kupiga kura
 
Mahera ni refa mshambuliaji 😂😂. Ila nayeye ajiandae kwenda The hague.

Nashauri waendeelee kuropoka ili pawe na ushahidi wa kutosha ili wote wafungwe the hague. Pia ushahidi uhifadhiwe na video zao wakiongea zitafsiriwe kwa kingereza na ziwe na subtitle za kingereza.
 
Umesema vema ni kweli unapitia wakati mgumu, zaidi ya barua ya Amsterdam, pia unashinikizo kutoka kwa aliyekuteua, polepole na chama chako kwa ujumla.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mahera amesema amepokea barua hiyo kutoka kwa raia wa Marekani anayefahamikama kwa jina la Robert Amsterdam akiitisha NEC.
sawa, we endelea kupuuza kanuni na taratibu za uchaguzi ili uvurugike kisha utajua huyo robeti ni nani !!
 
Back
Top Bottom