NEC yatangaza madiwani 30 wa CCM kupita bila kupingwa baada ya wapinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Tume ya taifa ya uchaguzi, NEC wamesema wagombea wa udiwani 3O kutoka CCM wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti

Vyama vya upinzani, CHADEMA na ACT wiki ilyopita vililalamika wagombea wao kufanyiwa zengwe mablimbali ikiwa ni pamoja na kuvamiwa na watu wenye bunduki na kuporwa fomu za kugombea, kuambiowa sio raia wa Tanzania na wengine kuwekewa pingamizi za kutokugombea katika muda uliokaribiana na mwisho [deadline] kinyume na utaratibu na kushindwa kujibu mapingamizi hayo kutokana na muda

Mkurugenzi wa NEC akitoa maelezo zaidi juu ya wagombea hao

======

Wagombea 30 wa udiwani katika uchaguzi wa kata 77 wamepita bila kupingwa, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Dkt. Kihamia amesema kwamba madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi (CCM).

“Katika Uchaguzi huu wa Kata 77 Wagombea Udiwani katika Kata thelathini (30) wamepita bila kupingwa na wagombea hao wote ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” alisema.

Dkt. Kihamia amefafanua kwamba wagombea hao wamepita bila kupingwa baada ya Tume kukutana, kujadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.

Amesema kwamba rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

“Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa 25 ambapo jumla ya wagombea kumi (10) walifanikiwa na hivyo kuendelea na uchaguzi na wagombea 15 rufaa zao hazikufanikiwa na hivyo kutoendelea kuwa wagombea,” alisema.

Dkt. Kihamia amesema kwamba katika kata sabini na saba (77) wanachama 254 kutoka vyama kumi na moja (11) vya siasa walichukua fomu za uteuzi na kwamba jumla ya wanachama 186 sawa na asilimia 73.2 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea ambapo kati yao wagombea 179 sawa na asilimia 96.2 ni wanaume na wagombea 7 sawa na asilimia 3.8 ni wanawake.

“Hadi muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika (saa 10.00 jioni siku ya uteuzi) wanachama 68 sawa na asilimia 26.8 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda unaokubalika kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo,” alisema.

Dkt. Kihamia amesema katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani jumla ya vyama kumi na moja (11) vimesimamisha aagombea.

Wagombea katika Kata kwa kila Chama ni kama ifuatavyo: ACT-Wazalendo Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), ADC Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), CCM Wagombea 77 (sawa na asilimia 100) CHADEMA Wagombea 54 (sawa na asilimia 70), CHAUMMA Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6), CUF Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), Demokrasia Makini Wagombea 4 (sawa na asilimia 5.2), NCCR-MAGEUZI Wagombea 6 (sawa na asilimia 8), NRA Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), SAU Mgombea 1 (sawa na asilimia 1) na UPDP Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6).

Wakati huohuo, Dkt. Kihamia amesema kwamba katika jimbo la Buyungu jumla ya wanachama kumi (10) kutoka vyama kumi (10) vya siasa vya AAFP, ACT-Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF, DP, Demokrasia Makini, NRA, UMD na UPDP walichukua fomu za uteuzi.

“Wanachama wote kutoka vyama hivyo walirejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea wa Ubunge katika Jimbo hilo, kati yao wanaume ni tisa (9) na mwanamke mmoja (1),” amesema Dkt. Kihamia.

Amevitaka vyama vya siasa na wagombea wao kuzingatia maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na siku ya uchaguzi.

Hivi ikitokea siku ha kupiga kura kwa mfano asitokee mpiga kura hata mmoja hivi nec huwa wanafanya uamuzi gani hapo
 
Napongeza hatuwa hiyo, itaepusha vifo visivyo na ulazima na ulemavu usio na ulazima kwa innocent people refer Akwilina.

Pesa zote zilizopangwa kama bajeti ya uchaguzi wa kata hizo zirudishwe hazina haraka na CAG akaguwe hesabu za NEC.

Napendekeza Magufuli apitishwe bila kupingwa mwaka 2020, kwani kufanya uchaguzi itakuwa ni kupoteza pesa za Watanzania bure huku matokeo yakiwa yanajurikana waziwazi.
 
Haiwezi kutokea si wangombea wenyewe watapiga kura?
Ok. Kwa hiyo kumbe mgombea akajipigia kura na akapata kura moja hiyo na akawa hakuna mpinzani huyo huyo ndo anapitishwa kuwa kashinda?
 
Siyo NEC sema Tume ya Uchaguzi ya CCM ..refa kaweka mpira kwapani,wala vumbi utawala huu mtalia na kusaga meno mana mlishakubali maisha ya telemka tukaze.
 
Tume ya taifa ya uchaguzi, NEC wamesema wagombea wa udiwani 3O kutoka CCM wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti

Vyama vya upinzani, CHADEMA na ACT wiki ilyopita vililalamika wagombea wao kufanyiwa zengwe mablimbali ikiwa ni pamoja na kuvamiwa na watu wenye bunduki na kuporwa fomu za kugombea, kuambiowa sio raia wa Tanzania na wengine kuwekewa pingamizi za kutokugombea katika muda uliokaribiana na mwisho [deadline] kinyume na utaratibu na kushindwa kujibu mapingamizi hayo kutokana na muda

Mkurugenzi wa NEC akitoa maelezo zaidi juu ya wagombea hao

Huyu mkurugenzi ni mpumbafu sijapata kuona. Sasa kunesanesa hivyo ndio nini au anafurahia wagombea 30 wa chama chake kupita bila kupingwa?
 
Alafu huyu mkurugenzi ni Dr, tena huenda ni wa sheria. Huu si uoga wa kusikiliza wasiojua sheria kukulazimisha kufanya kazi watakavyo!!!
 
Hivi ikitokea siku ha kupiga kura kwa mfano asitokee mpiga kura hata mmoja hivi nec huwa wanafanya uamuzi gani hapo
Kaka, wasimamizi watalazimishwa kupiga kura tena watapewa karatasi 20 mpaka 30 kila 1 na nafasi itally kama waliojiandikisha, wafanyakazi wa serikali watalazimishwa wa mtaa au eneo hilo watalazimishwa tena kwa attendance register akifika wanatick jina lake na anapewa karatasi za kura kama 30 akapige, nimeona uchaguzi wa marudio visiwani
 
hivi sheria inasemaje ikiwa mgombea kapita bila kupingwa je huwa apigiwi kura hata kama yupo peke yake au ndo nitolee asubiri kutangazwa tu..
 
W
Tume ya taifa ya uchaguzi, NEC wamesema wagombea wa udiwani 3O kutoka CCM wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti

Vyama vya upinzani, CHADEMA na ACT wiki ilyopita vililalamika wagombea wao kufanyiwa zengwe mablimbali ikiwa ni pamoja na kuvamiwa na watu wenye bunduki na kuporwa fomu za kugombea, kuambiowa sio raia wa Tanzania na wengine kuwekewa pingamizi za kutokugombea katika muda uliokaribiana na mwisho [deadline] kinyume na utaratibu na kushindwa kujibu mapingamizi hayo kutokana na muda

Mkurugenzi wa NEC akitoa maelezo zaidi juu ya wagombea hao

Waambie mods warekebishe hiyo heading yako. Ni madiwani 30 (siyo 3 kama ulivyoandika) wa CCM wapita bila kupingwa kwenye kata 77 za uchaguzi mdogo ujao.
 
Tume ya taifa ya uchaguzi, NEC wamesema wagombea wa udiwani 3O kutoka CCM wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu mbalimbali kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti

Vyama vya upinzani, CHADEMA na ACT wiki ilyopita vililalamika wagombea wao kufanyiwa zengwe mablimbali ikiwa ni pamoja na kuvamiwa na watu wenye bunduki na kuporwa fomu za kugombea, kuambiowa sio raia wa Tanzania na wengine kuwekewa pingamizi za kutokugombea katika muda uliokaribiana na mwisho [deadline] kinyume na utaratibu na kushindwa kujibu mapingamizi hayo kutokana na muda

Mkurugenzi wa NEC akitoa maelezo zaidi juu ya wagombea hao

======

Wagombea 30 wa udiwani katika uchaguzi wa kata 77 wamepita bila kupingwa, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Dkt. Kihamia amesema kwamba madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi (CCM).

“Katika Uchaguzi huu wa Kata 77 Wagombea Udiwani katika Kata thelathini (30) wamepita bila kupingwa na wagombea hao wote ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” alisema.

Dkt. Kihamia amefafanua kwamba wagombea hao wamepita bila kupingwa baada ya Tume kukutana, kujadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.

Amesema kwamba rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

“Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa 25 ambapo jumla ya wagombea kumi (10) walifanikiwa na hivyo kuendelea na uchaguzi na wagombea 15 rufaa zao hazikufanikiwa na hivyo kutoendelea kuwa wagombea,” alisema.

Dkt. Kihamia amesema kwamba katika kata sabini na saba (77) wanachama 254 kutoka vyama kumi na moja (11) vya siasa walichukua fomu za uteuzi na kwamba jumla ya wanachama 186 sawa na asilimia 73.2 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea ambapo kati yao wagombea 179 sawa na asilimia 96.2 ni wanaume na wagombea 7 sawa na asilimia 3.8 ni wanawake.

“Hadi muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika (saa 10.00 jioni siku ya uteuzi) wanachama 68 sawa na asilimia 26.8 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda unaokubalika kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo,” alisema.

Dkt. Kihamia amesema katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani jumla ya vyama kumi na moja (11) vimesimamisha aagombea.

Wagombea katika Kata kwa kila Chama ni kama ifuatavyo: ACT-Wazalendo Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), ADC Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), CCM Wagombea 77 (sawa na asilimia 100) CHADEMA Wagombea 54 (sawa na asilimia 70), CHAUMMA Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6), CUF Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), Demokrasia Makini Wagombea 4 (sawa na asilimia 5.2), NCCR-MAGEUZI Wagombea 6 (sawa na asilimia 8), NRA Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), SAU Mgombea 1 (sawa na asilimia 1) na UPDP Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6).

Wakati huohuo, Dkt. Kihamia amesema kwamba katika jimbo la Buyungu jumla ya wanachama kumi (10) kutoka vyama kumi (10) vya siasa vya AAFP, ACT-Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF, DP, Demokrasia Makini, NRA, UMD na UPDP walichukua fomu za uteuzi.

“Wanachama wote kutoka vyama hivyo walirejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea wa Ubunge katika Jimbo hilo, kati yao wanaume ni tisa (9) na mwanamke mmoja (1),” amesema Dkt. Kihamia.

Amevitaka vyama vya siasa na wagombea wao kuzingatia maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na siku ya uchaguzi.

Acha kutumika bro ww ni mtaalamu, achana nambo ya kuibeba ccm, Mungu hapendi kabisa dhuluma mnazowafanyia wapinzani
 
Back
Top Bottom