NEC yataka Tume yao ipewe meno ili iwe Huru

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage, Agosti 21 akiwasilisha ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2020 kwa Rais Samia alitoa mapendekezo saba ya kufanyiwa kazi, likiwemo la kuanzishwa kwa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itawapa meno zaidi.

Mapendekezo ya NEC ya kutaka ianzishwe sheria inayowatambua na kuwapa mamlaka zaidi imetoa tafsiri kuwa wanataka wajiendeshe kwa uhuru na ufanisi zaidi pasi hofu ya kuingiliwa na viongozi, yanaipa nguvu hoja ya wanaotaka tume huru ya uchaguzi.

Licha ya NEC na viongozi wa Serikali mara kwa mara kupinga kutoa au kupokea maelekezo ya uendeshaji wa uchaguzi, lakini ukweli unabaki kuwa kuna mkanganyiko wa kisheria na tume hiyo haiko huru.

Baadhi ya mapendekezo yanaonyesha wanalenga kuboresha utendaji, kuongeza kuaminika kwa wadau na kupata uhuru zaidi.

Kama pendekezo hili litapitishwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2025, ingawa inaonekana gharama ndizo zitakuwa kikwazo cha utekelezwaji wake kama alivyodokeza Rais Samia.

Pendekezo jingine ni kuunganishwa sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura namba 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, sura ya 292 ili kurahisisha utekelezaji wa sheria hizo.

Vilevile, NEC inapendekeza uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu usimamiwe na mamlaka moja.

Kimsingi mapendekezo ya NEC yanaonyesha taasisi hiyo inavyofanya kazi katika mazingira magumu ambayo pia yanawafanya wasipate uungwaji mkono wa baadhi ya wadau pindi wanapotangaza matokeo ya kuendesha uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi
 
B
Binafsi sina ugomvi na tafsiri yako juu ya mapendekezo ya Jaji Kaijage wa NEC kwani kila mtu anayo haki ya kutafsiri kitu kadri alivyo elewa na kufuatana na mawazo, mapenzi, matakwa na ushabiki wake kwenye hoja au suala husika.

Hivyo nami nasema kuwa Jaji Kaijage anataka NEC iwe "huru" kwa kupitia kutungiwa Sheria yao ILI waweze kufanya mambo yao ya usimamizi wa NEC na kazi zake zote BILA kutegemea wafanyakazi wa Serikali au kusubiri mgao wa fedha in a form of RUZUKU.

Jaji Kaijage anataka awe na afanye kazi kama "AGENCY", ili apate mgao wa fedha moja kwa moja kwenye bajeti yao na NEC iwe na bajeti yake inayo eleweka, siyo kusubiri kupewa pesa kutoka Hazina kwa ajili ya uendeshaji wa NEC na iwe na wafanyakazi watakao wajibika moja kwa moja kwa NEC na siyo kwa mamlaka na madaraka nyingine ya ajira.

Hii ndiyo tafsiri yangu siyo kuwa eti "wanabanwa" na Serikali katika kufanya maamuzi yao eti kwa vile hawana Sheria yao wenyewe. This is my take.
 
Binafsi sina ugomvi na tafsiri yako juu ya mapendekezo ya Jaji Kaijage wa NEC kwani kila mtu anayo haki ya kutafsiri kitu kadri alivyo elewa na kufuatana na mawazo, mapenzi, matakwa na ushabiki wake kwenye hoja au suala husika...
Maelezo uliyo yatoa ni sahihi ila hapo kwenye kusubiri pesa kutoka hazina sidhani kama ni sahihi,maana Taasisi zote za Serikali Wizara,Mamlaka za Serikali za mitaa,Taasis na mashirika ya umma karibu zote zinapokea fedha kutoka hazina.

Hata Taasisi ambazo zinakusanya na kitumia Mkakati uliopo kwa sasa wakusanye wapeleke kisha wapewe mgao.
 
Maelezo uliyo yatoa ni sahihi ila hapo kwenye kusubiri pesa kutoka hazina sidhani kama ni sahihi,maana Taasisi zote za Serikali Wizara,Mamlaka za Serikali za mitaa,Taasis na mashirika ya umma karibu zote zinapokea fedha kutoka hazina.

Hata Taasisi ambazo zinakusanya na kitumia Mkakati uliopo kwa sasa wakusanye wapeleke kisha wapewe mgao.
Yaah uko sawa ila tofauti hapa ni kuwa NEC ya sasa haina bajeti yake yenyewe, yaani ile ya kupitishwa na Bunge bali inaombewa na kupangiwa na aidha Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais - UTAWALA BORA; sina hakika sawa sawa na hili (inabidi kurudi kwenye makabrasha yangu on this). Ila wakiwa na Sheria yao wenyewe watakuwa na "nguvu" za kufanya maamuzi hasa hasa ya staff.
 
Tunasubiri na polisi nao waje na mapendekezo yao! Maana na wenyewe wanafanya pia kazi zao katika mazingira magumu!

Kuna wakati inawalazimu kufanya maigizo, ili tu kuwafurahisha wanasiasa wa upande mmoja, huku wakiwaumiza wale wa upande mwingine.
 
Tushaujua ujanja wa CCM kuelekea uchaguzi wa 2025 - bila katiba mpya watanzania msikubali kurubuniwa.
 
Back
Top Bottom