Uchaguzi 2020 NEC yataka raia wa kigeni kudhibitiwa wasipige kura Uchaguzi Mkuu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama zilizo kwenye mipaka ya nchi ziwadhibiti raia wakigeni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

NEC imesema kitendo cha wageni kuingia nchini na kupiga kura ni kinyume na sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuepusha vurugu na uvujifu wa amani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ametoa agizo hilo katika kikao kati ya maofisa wa tume na wadau wa uchaguzi kilicholenga kutoa elimu ya mpiga kura kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi itekeleze kwa vitendo miongozo iliyoitoa, kwa kutoa haki sawa kwa makundi yote kushiriki uchaguzi mkuu.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama zilizo kwenye mipaka ya nchi ziwadhibiti raia wakigeni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

NEC imesema kitendo cha wageni kuingia nchini na kupiga kura ni kinyume na sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuepusha vurugu na uvujifu wa amani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ametoa agizo hilo katika kikao kati ya maofisa wa tume na wadau wa uchaguzi kilicholenga kutoa elimu ya mpiga kura kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi itekeleze kwa vitendo miongozo iliyoitoa, kwa kutoa haki sawa kwa makundi yote kushiriki uchaguzi mkuu.
Ina maana hao wageni taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zipo?
Na kama zipo udhaifu huu ulikuwaje mpaka watu wakapata hivyo vitambulisho?
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama zilizo kwenye mipaka ya nchi ziwadhibiti raia wakigeni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

NEC imesema kitendo cha wageni kuingia nchini na kupiga kura ni kinyume na sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuepusha vurugu na uvujifu wa amani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ametoa agizo hilo katika kikao kati ya maofisa wa tume na wadau wa uchaguzi kilicholenga kutoa elimu ya mpiga kura kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi itekeleze kwa vitendo miongozo iliyoitoa, kwa kutoa haki sawa kwa makundi yote kushiriki uchaguzi mkuu.
Mnawagusa wapiga kura wa Heche sasa
 
Wanapigaje ikiwa hawajaandikishwa? Na kama wameandikishwa kwa nini NC isiwaondoe ktk daftari?
 
Hapa naona kuna kizungumkuti , ina maana kuna watu ambao sio watanzania wamejiandikisha ? Kwnn hawakudhibitiwa toka mwanzo? Kama hawaandikwa kwnn wahe kupiga kura kama hawana vitambulisho lkn pia majina yao hayapo ktk daftali la kupiga kula? Naona hapa kama sielewi vileeeeeeeeeee

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Ina maana hao wageni taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zipo?
Na kama zipo udhaifu huu ulikuwaje mpaka watu wakapata hivyo vitambulisho?
Hujui kuna rushwa? na hiyo rushwa ndo mgombea wenu anataka irudi kwani ukipata rushwa unaenda nyumbani na furaha na samaki kabisa au kuku.
 
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ni muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini Tanzania. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa na mkosaji kujiadhibu mwenyewe, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. Uliona wapi nyani anajizuia kula mahindi ya mkulima? Nyani wamezoea kula mahindi ya mkulima kiasi kwamba mkulima akiwafukuza au kuwaua wasimalize mahindi yake, watamuona kama anawaonea bure! Wanadhani kula mahindi wasiyoyalima ni haki yao ya msingi au ya kuzaliwa.

Jinsi ambavyo wanakula mahindi ya mkulima, vivyo hivyo CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya chama cha mapinduzi ilipotufikisha.

Na kama ambavyo ili mkulima ajiepusha na nyani anapaswa kuwaua au kuwafukuzilia mbali nyani, vivyo hivyo kwa chama cha mafisadi na serikali yake, ili kuepukana na ufisadi wao, hatuna budi kuwapiga chini mwaka huu wa 2020. Hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang’oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang’oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.

Ndugu watanzania tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na kupe hawa wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hupenda kuchakura mwenyewe vichakani kutafuta chakula bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wajitafutie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa. Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona humtakii mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.

Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa wanakiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2015. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hiyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (maCCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo waaliyoyaleta MABEBERU wa kikoloni.

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 22 alizoziacha Mkapa hadi Tsh trillion 55 sawa na ukuaji wa 150%! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi maisha bora tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukampigie kura Mgombea wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hii ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020!
 
Back
Top Bottom