Nec yarejesha majina ya madiwani viti maalumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nec yarejesha majina ya madiwani viti maalumu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 9, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Nec yarejesha majina ya madiwani viti maalumu

  Imeandikwa na Christopher Maregesi, Bunda; Tarehe: 8th December 2010 @ 21:20

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imerejesha majina ya madiwani wa viti maalumu kwa vyama vya CCM na CHADEMA huku chama cha TLP kikiwa hakijarejeshewa jina la diwani wake kwa vile hakijaitumia tume hiyo mapendekezo.

  Katika majina hayo, CCM imerejeshewa madiwani watano tu ikiwa ni pungufu kwa majina ya
  awali ilipokuwa imeletewa madiwani wanane kati ya kumi wanaotakiwa kwa nafasi hiyo huku CHADEMA ikiwa imepatiwa jina mmoja.

  Msimamizi wa Uchaguzi kwa majimbo ya Bunda na Mwibara, Cyprian Oyeir amesema Desemba 8 kuwa Nec imeahidi kurejesha majina yaliyosalia ya CCM na jina moja la TLP kadri vyama hivyo vitakavyokuwa vikiwasilisha mapendekezo yao kwenye Tume hiyo.

  Oyeir ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, amewataja madiwani hao waliopitishwa na Nec kuwa ni Salome Lutoryo, Agness Mathew, Nyachiro Chitema, Mariam Nyamoko na Mariam Sindano ambao wote ni wa CCM huku Diwani wa Chadema akimtaja kuwa ni Lucy Mzuma.

  Hii itakuwa mara ya pili kwa Nec kurejesha majina ya madiwani wa viti maalumu kwani wiki iliyopita ilirejesha majina ya wanaCCM nane yaliyopingwa na wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wilayani hapa wakiyaelezea kuwa yamechakachuliwa na
  kuutaka uongozi wa CCM kuyarejesha kwa Tume ili yarekebishwe.

  Kutokana na mgomo baridi huo wa wanachama hao wa UWT, iliulazimu uongozi huo wa CCM wilayani hapa kupitia kwa Katibu wake, Charles Mwangwale kuyarejesha majina hayo kwa Tume ili yafanyiwe marekebisho.
   
 2. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama wenye kwa wenyewe wanachakachuana iweje kwa wengine??? HUU NI UGONJWA SUGU KAMA UKOMA TIBA NI KUWATENGA WAGONJWA
   
Loading...