NEC yapiga marufuku CHADEMA Kuhamasisha Uandikishaji

Tunahuuru sana mwanasheria.
Afadhali umeliona hili.

Mwenyekiti wa NEC amepiga marufuku jitihada za CHADEMA kuhamasisha watu kujiandikisha kupiga kura huko Singida.

CHADEMA walikuwa wanatumia vipeperushi na matangazo ya magari kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi.

Kauli hii ya Mwenyekiti wa NEC inanishangaza kwani kila chama kina haki ya kuhamasisha wafuasi wake kujiandikisha na hiyo ndio kazi ya siasa.

Hii inatupelekea tuhisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina agenda ya siri maana katika hali ya kawaida Tume ingefurahi kwa vyama kufanya kazi ya uhamasishaji.
 
Hiyo ni kazi ya tume chadema nao wamezidi kila tukio wanaona watoke vipi watafute issue ya kuongea na wananchi.

nanukuu maelezo ya Mwenyekiti wa tume DAMIAN LUBUVA aliyoandika katika kitabu alichowaandikia vyama vya siasasa kitabu hicho kinaitwa MAELEKEZO KWA VYAMA VYA SIASA.
UJUMBE WA MWENYEKITI.
"katika uboreahaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya tume ya taifa ya uchaguzi ,vyama vya siasa na wadau wengine.Vile vile ,ili utekelezaji wa zoezi hili uwe na mafanikio mazuri , ni muhimu kuwepo elimu kwa umma na uhamasishahi wa kutosha juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, aidha utaratibu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura hauna budi ueleweke vizuri"
hapa tena akaendelea kuandika
"maelekezo yaliyomo katika kijitabu hiki yameandaliwa ili kuvisaidia vyama vya siasa viweze kushiriki katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"
hapa akaendelea kuandika
"napenda kutoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kutumia fursa hii kujielimisha juu ya dhana ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,utaratibu na hatua zitakazotumika katika zoezi hili"
MAELEZO HAYO YOTE JUU YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WA (iii).
katika ukurasa wa 1. kuna maelezo mengine kuhusu swala la uhamasishaji.
nanakiri maelezo hayo.
"vyama vya siasa vina wajibu mkubwa wa kuwaelekeza na kuwaelimisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla umuhimu wa kuwemo katika daftari la kudumu la wapigakura ,na utaratibu utakaotumika katika uboreshaji wa daftari hilo.Hivyo ni muhimu kwa vyama vya siasa kuhamasisha na kuelimisha wanachama wao pamoja na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu na kuelewa uboreshaji wa daftari hilo, haki na wajibu wao"
KABLA NA WAKATI WA UBORESHAJI
"kwa kuwa uboreshaji utafanyika katika kipindi cha siku kumi na nne(14) tu, ipo haja kwa vyama vya siasa kabla na wakati wa kipindi hicho , kuwahimiza wananchi wajitokeze kujiandikisha wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"
WAKATI WA UKAGUZI WA DAFTARI
"ni wajibu wa vyama vya siasa kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kukagua daftari la awali la wapiga kura mara litakapowekwa wazi kwa ukaguzi.
daftari la awali la wapiga kura litakuwa kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa muda usiozidi siku saba.kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa wananchi kuhamasishwa kujitokeza bila kuchelewa kukagua daftari hilo.
wananchi pia waelimishwe kuhusu utaratibu mzima wa kuweka pingamizi kama watakuwa na sababu za msingi. vile vile waelimishwe kuwa wana haki ya kukata rufaa kwenye mahakama ya wilaya ,iwapo hawakuridhika na uamuzi uliotolewa kuhusu pingamizi walilowekewa au waliloweka"
baada ya nukuu zote hizo hapo juu ambazo zimetokana na MAELEZO YA TUME YA UCHAGUZI CHINI YA JAJI MASTAAFU DAMIAN LUBUVA.
nitoe masikitiko yangu makubwa kama hili limetokea na kuamrisha CHADEMA ISITISHE UHAMASISHAJI KATIKA HILO ULILOTAJA.
kwa kuwa maelekezo hayo yanaenda kinyume na ujumbe wa jaji huyuhuyu alioutoa kwa vyama vya siasa.
lakini kibaya zaidi yanakiuka taratibu za kanuni na sheria ya uchaguzi.
hivyo vyama vya siasa visitishwe na kauli hiyo ya Lubuva kuzuia uhamasishaji. na badala yake viendelee kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi ili wasipoteze haki yao.
na kwa kuwa hakuna utaratibu uliotolewa ni kwa namna gani uhamasishaji ufanyike. itakuwa si kosa kwa vyama kuandaa na kuchapisha vipeperushi vya kuelimisha na kuhamisha, pia si kosa kutoa matangazo kwa spika, mikutano na hata matangazo kwa njia ya radio na television.
NA:
KATIBU MWENEZI CHADEMA KATA YA MSIGANI(jimbo la ubungo).
Joseph Mshinga.
 
Ndugu wewe ndio umesema kitu chenye msingi sana. Hili cdm wakilikalia kimya jamaa wataendelea kufanya kwa kujivuta kwani wana ajenda ya siri kwenye hili zoezi.

NOTE!
Inawezekana kabisa kuwa UKAWA/ au CDM wanajua kilicho nyuma ya pazia na wanafuatilia ili wakamirishe evidences! Maana hata sisi watu wa vijijini tunaona kuna agenda kali sana.
 
Ni vyema kuhamasishana, si CHADEMA tu hata sisi huku mitaani ni muhimu kuhamasisha kwa sababu si wote wanaoelewa kuwa ni muda wa uandikishaji.

Kuna baadhi ya watu wapo busy kiasi hata muda wa kupata hizo taarifa ni jambo gumu.

Ili kufanikisha zoezi la kupiga kura ni muhimu wananchi wote kujiandikisha.

Mimi Binafsi sioni kosa kwa wanasiasa, watu binafsi, viongozi wa dini zote kuhamasisha wananchi wajiandikishe kupiga kura. Endapo kama watahamasisha watu kukipigia kura chama fulani hapo kweli ni kosa lakini kumbe wanataka watu wote kujiandikisha!!!!!!

Sioni kosa.

NEC wakae chini na wajifikirie, au basi wao wapite mitaani na magari yenye vipaza sauti na kuhamasisha watu jambo ambalo hawajaifanya hadi sasa zaidi ya kutoa matangazo katika vyombo vya habari. Si wote wenye access na vyombo vya habari kila siku.....

Tukikumbuka uchaguzi uliopita wa Serikali za mitaa, ni kwamba ulipelekwa kimyakimya katika uandikisha na matokeo yake si wananchio wote waliopiga kura. Sasa huu wa mwezi wa October 2015 ni uchaguzi mkuu na muhimu kwetu. hivyo ni vyema wananchi wote wenye vigezo kushiriki

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ndugu yangu hiyo ndio kazi ya siasa. Soma gazeti la the Standard au the Daily Nation ya Kenya utakuta wanasiasa wanahamasisha watu kujiandikisha kwa ajili ya 2017. Watu wako wasipojiandikisha utashindaje? Ni mara ya kwanza Tanzania wapinzani kuhamasisha watu wajiandikishe maana miaka yote walikuwa wana wafuasi ambao hawapigi kura maana hawakujiandikisha. Sasa unawazuia kwanini kama si uonevu?
Sitaki kuamini hii kauli kama kweli imetolewa na NEC, kwa sababu si siku nyingi Mwenyekiti alivihimiza vyama vya siasa viwahamasishe watu kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu badala ya kuwalalamikia Tume na kusema uchaguzi mkuu hautakuwepo! Sasa haya yanatoka wapi, ebu tuwekeeni chano cha habari hii.
 
Kuna siku watasema CHADEMA hakuna kuvuta hewa mpaka kwa kibali cha NEC.
That old man is a spent force with a mild stroke. Hatoshi na ni aibu kuwa mwenyekiti wa NEC. It does not make sense kuzuia uhamasishaji. Ikija kuhamasisha chanjo Okay. Lakini kutimiza haki ya uraia Inakuwa taaabu. Hii serikali na NEC yake ni mkosi. Chadema kazi iendelee. Hakuna sheria inayozuia kuwaambia wanainchi waende kutekeleza wajibu wao. Ila ipo pale unapowazuia.
 
Upo sawa mkuu, kwani si ilitakiwa NEC washukuru kurahisishiwa kazi. Endeleeni na mchakato
Hivi si Tume hiyo hiyo kwenye chaguzi zilizopita wamekuwa wakilalama na kushangazwa sana, kwa kutojua sababu za watu kujitokeza 'kiduchu' wakati wa upigaji kura, ambao huwa wanakuwa chini ya asilimia 30?

Sasa kwa neema hii ya 'mafuriko' makubwa sana ya watu wanaotaka kujiandikisha kupiga kura, kwa mazingira ya kawaida Tume ya uchaguzi ingepaswa kuwa ya kwanza kuwapongeza wananchi waliohamasika kupita kiasi na kujitokeza kwa wingi sana kujiandikisha.

Kwa kuwa kutokana na wananchi wengi kujiandikisha kwa staili ya 'mafuriko' inaleta matumaini makubwa kuwa hata siku ya upigaji kura, ule ukame wa watu kujitokeza kwenda kupiga kura, ni dhahiri utatoweka na watu watakaojitokeza kupiga kura kutokana na hamasa waliyonayo wanakadiriwa kuwa wengi sana na kuzidi asilimia 90.

Sasa kwa Tume ya uchaguzi hiyo hiyo kuonyesha 'kununa' kutokana na neema hiyo ya wingi huo wa watu wanaojitokeza kujiandikisha kupiga kura, kunaleta tafsiri gani?

Kutokana na mazingira hayo ni lazima sasa wananchi tujiulize kwa undani kama kweli hiyo Tume ipo huru kweli?

Hivi kwa vitendo hivi vya Tume ya uchaguzi kwa kuamua kuendelea kuandikisha wapiga kura kwa kusuasua kwa mtindo wa 'kinyonga' na kwa kauli hiyo ya kuzuia vyama vya siasa visihamasishe wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye uandikishaji, hivi wananchi tukidhani kuwa Tume hiyo inaendeshwa kwa 'remote control' kutoka mtaa wa Lumumba tutakuwa tumekosea?
 
Wakati Chadema Wakihamasisha wananchi kujiandikisha CCM wao wanafanya jitihada watu wasijiandikishe...... Inaingia akilini kweli??? Hivi Kila siku CCM wanadai wanachama wao ni 6Milion. Wapiga Kura ni zaidi ya 20mil+ CCM wanashindaje??
 
Viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA popote pale mlipo ndani na nje ya nchi nawaombeni muendelee na juhudi za kuwahamasisha Watanzania katika kila kona ya nchi yetu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao. Hakuna kipengele chochote ndani ya hii fake Tume ya uchaguzi kinachozuia vyama vya siasa kupigwa marufuku kuhamasisha Watanzania katika kujiandikisha kupiga kura.

Alluta continua! continua!

:peace: :peace: :peace:
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupingwa na CCM na Tume ya uchaguzi kufanya zoezi la uhamasishaji, wakidai ni wajibu wa tume kutoa matangazo.

Maoni yangu ni kwamba, tume hawana nia njema na zoezi hili na wamekusudia kuzuia watu wasijitokeze, na Chadema watakuwa wamefanya kosa la karne kama watakubaliana na uamuzi huo wa tume.

Tulifanya vikao viongozi wa vyama kama wadau wa uandikishaji na Afisa Mwandikishaji ambaye ni mkuruganzi wa wilaya, na tukakubaliana kwa kupitia miongozo ya tume kuwa sisi ni wadau muhimu wa zoezi hili na tunawajibika kuhamasisha wanachama na wafuasi wetu kujitokeza kujiandikisha, na tumekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana ushirikiano huu watu wengi wanajitokeza kujiandikisha. Sasa Tume wanaogopa nini Chadema tukiwatangazia wananchi wakajitokeza kwa wingi kujianandikisha? Kwakuwa miongozo tulipewa na iko wazi hatutaacha kuhamasisha watu kujitokeza kujiandikisha hiyo ni kazi yetu kama viongozi wa chama na hatuhitaji ruhusa ya ya tume wala mtu yoyote, kama tutakuwa tunavunja sheria watupeleke mahakamani.
 
Viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA popote pale mlipo ndani na nje ya nchi nawaombeni muendelee na juhudi za kuwahamasisha Watanzania katika kila kona ya nchi yetu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao. Hakuna kipengele chochote ndani ya hii fake Tume ya uchaguzi kinachozuia vyama vya siasa kupigwa marufuku kuhamasisha Watanzania katika kujiandikisha kupiga kura.

Alluta continua! continua!

:peace: :peace: :peace:

CCM imeshaumia mpaka sasa, wameshaitonya tume yao kuwa hali yetu ni mbaya, tunafanya kazi kama mchwa na wananchi wanaiitikia wito wetu, CCM wameogopa.
:peace:
 
  • Thanks
Reactions: BAK
NAPE AWATAKA VIJANA KUJIANDIKISHA KWA WINGI KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Wednesday, May 20, 2015

ccmchama.blogspot.com/.../nape-awataka-vijana-kujia...

Yani CCM wahamasishe lkn CDM hapana??? Huu ni ubakaji wa kisiasa na haki ya msingi ya mpiga kura.
 
Ahsante sana Mkuu, inaonyesha ni jinsi gani MACCM yanaweweseka na hivyo kutaka kutumia kitengo chao fake cha Tume ya uchaguzi kuminya haki za vyama vya upinzani kuwahamasisha Watanzania katika kujiandikisha katika upigaji kura.

Back
Top Bottom