NEC yapata pigo kuzuiwa upendeleo wa kampuni ya vifaa vya uchaguzi

What the F is this sh.t...
Chicken head.

komaa mkuu, kuwa na political tolerance, matusi hayasaidii kitu, kuna kamsemo kanasema "dying without bitterness" kwa kiswahili nnaweza kukafananisha na "sikio la kufa halisikii dawa"

tulikuwa tunaisema CCM inatumia hoja ya nguvu, huku CHADEMA ikijipambanua kwa nguvu ya hoja, days has gone CHADEMA is now practicing hoja ya nguvu, likewise CCM. CHADEMA bado inanafasi kubwa sana kwenye jamii ya mtanzania, bado kuna nafasi ya kukaa chini kutafakari, kujirekebisha na kusonga mbele, unlike CCM ambayo nothing can be done to rescue it.

"truth will set you free"
 
".......Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa PPAA, uamuzi huo ulifikiwa mwezi uliopita ambapo NEC imeamriwa kurudia upya mchakato mzima wa kutoa zabuni, ikiwemo kutangaza katika vyombo mbalimbali vya habari kwa utaratibu unaokubalika.

Mkakati wa NEC kutoa zabuni kwa kampuni hizo uliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambapo alisema ulikuwa na lengo la kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.

Zitto alisema lengo ni kuhakikisha mchakato wa vitambulisho vya kupigia kura vya kielektroniki vinakuwa na faida kwa CCM na kukiingizia fedha chama hicho za kutumia kwenye uchaguzi huo kupitia mfumo huo dhaifu wa vitambulisho hivyo.

Kampuni zilizokosa tenda zililalamika kwa mkurugenzi wa NEC namna mchakato wa kutoa zabuni hiyo ulivyoendeshwa, na kwamba ulikuwa haujawatendea haki ikiwa ni pamoja na kutofahamishwa sababu zilizowafanya wakose kazi hiyo.

Kampuni hizo zilihoji njia na sababu zilizowafanya wakose tenda hiyo licha ya kuwa na uzoefu, vifaa bora pamoja na kuwa na kiwango kidogo cha gharama tofauti na kampuni iliyopewa kazi.

Katika moja ya malalamiko yao, Kampuni ya M/S Morpho ililalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo licha ya kuwa na sifa za kimataifa za kufanya kazi, huku ikiwa imetoa bei nafuu kuliko kampuni iliyopata kazi.

“Tulikuwa miongoni mwa washindani muhimu kwa kuwa kiwango chetu kilikuwa ni sh bilioni 97.8 ambazo ni sawa na euro 44,939,912, ujuzi, vigezo na uzoefu wetu havilingani, duniani kote tumefanya kazi katika maeneo mengine kwa ufanisi na tunashindwa kuelewa kivipi walishinda hao ambao wamepata kazi kwa kiwango cha zaidi ya sh bilioni 27.8 ikilinganishwa na yetu,” ilisomeka sehemu ya barua yao ya malalamiko waliyopeleka NEC....."

Source: Tanzania Daima.
 
Ushindi wa ccm unawategemea wananchi wa tz ambao wanaipenda mno, sio nec
 
Lakini bado huyu anaitwa msaliti, na hao wanaokesha wakinywa na kubadilisha mabibi na wagombea urais wa CCM ndio wazalendo. Wao Zitto ndio adui, lakini hao wanaopanga kutengeneza utaratibu mrahisi na haramu kwa ushindi wa CCM sio tatizo. Wivu kwenye siasa ni kitu hatari sana!
 
nikiona tanzania daima tu nahisi kuchefuka haliajawahi kuandika tarifa ya maana hata siku moja.
 
takwimu zinaonesha kuwa ccm mtaji wake wa ushindi upo kwa watanzania kwa kuwa ni chama ambacho kinawatumikia vema watanzania.
 
albertomsando hebu eka hii habari ikamilike bhana!!!
mimi sijapata picha halisi ya nini kinacholeta shida manake umequote habari nusu, ama wewe ulilenga tu kutuonyesha kazi Zitto aloifanya??

naamini wapo wengi ambao hataona mantiki yako lkn mie kwa upeo wangu mdogo nilichoona hapa zaid ya kumpigia debe Zitto ama kuonyesha alotenda hukuwa na nia ingine..............

Nakusifu kwamba umeweza kuleta habari inayomhusu Zitto kwa njia ya tofauti kabisa yaani umetumia gia ya CCM kumpigia debe Zitto. U have good brain dude!!
 
Last edited by a moderator:
Maccm wana mbinu nyingi sana,hii moja kubuma sio issue kwao,wataibuka na jingine tu

"mwizi huwa updated zaidi kuliko mlinzi"
 
NEC yapata pigo
11/12/2013 | Posted by Mwandishi Wetu | Kitaifatangulizi | 0 comments | 87 views
TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), imepata pigo baada ya Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), kuizuia isitoe zabuni za kuandaa vifaa vya uchaguzi vya kielektroniki kwa kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution zenye thamani ya sh bilioni 126.3.

PPAA imefikia hatua hiyo baada ya kampuni za M/S Morpho na M/S IRIS Corporation Technology kukata rufaa kupinga uamuzi wa NEC kutoa zabuni kwa kampuni hizo.

M/S Morpho ililalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo iliyoahidi kuifanya kwa sh bilioni 97.8 lakini zikapewa kampuni zilizoahidi kuifanya kwa sh bilioni 126.3.

Habari kamili hiyo hapo brother.
 
Hizi ni hoja zenye sifa ya kubebwa kitaasisi lakini kama kawaida kwa kupenda sifa Zitto atasema tu haya kwa waandishi alafu atapata sifa huku akiwa ameisaidia kuishtua CCM "mko uchi chutama".
Hili lingetengenezewa mkakati wa ndani kitaasisi then iwe mtu kati kama wasemavyo watoto wa mjini maana si issue ndogo na wizi utahalalishwa kwa kupakwa mafuta tu ya kurudia mchakato na taratibu kufuatwa.

Au na hii mtasema tulitaka atutonye?
 
Kwa akili yako ya Bavicha unaona Slaa alipotoa list of shame Mwembeyanga ilikuwa ushujaa, lakini Zitto kuongelea hili tayari amekosea!

Hamjitambui, mpompo tu na wala hamjui mnapigania nini!!!
 
Dr Slaa hakuibuka tu pale mwembeyanga na kuisoma list of shame bali Chama kilimpa hiyo kazi!! Huo ndio mkakati wa kitaasisi.

Be smart not clever !!
 
Kwa akili yako ya Bavicha unaona Slaa alipotoa list of shame Mwembeyanga ilikuwa ushujaa, lakini Zitto kuongelea hili tayari amekosea!

Hamjitambui, mpompo tu na wala hamjui mnapigania nini!!!

Hajamtaja Dr.Slaa huyo,vipi anakuwasha eeh!?
 
NEC yapata pigo
11/12/2013 | Posted by Mwandishi Wetu | Kitaifatangulizi | 0 comments | 87 views
TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), imepata pigo baada ya Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), kuizuia isitoe zabuni za kuandaa vifaa vya uchaguzi vya kielektroniki kwa kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution zenye thamani ya sh bilioni 126.3.

PPAA imefikia hatua hiyo baada ya kampuni za M/S Morpho na M/S IRIS Corporation Technology kukata rufaa kupinga uamuzi wa NEC kutoa zabuni kwa kampuni hizo.

M/S Morpho ililalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo iliyoahidi kuifanya kwa sh bilioni 97.8 lakini zikapewa kampuni zilizoahidi kuifanya kwa sh bilioni 126.3.

Habari kamili hiyo hapo brother.

naona Candid Scope kaiweka vizuri zaid............BTW uko poa lkn ama upepo wa kisuli suli unakuzingua??
am dying to see you kwakweli.
 
Last edited by a moderator:
Another Zitto saga. Kwa haya ndo huwa najiuliza hivi hawa wanaompinga zitto ni wazalendo kweli au wachumia tumbo tu?. Thanks Zitto kwa kazi yako iliyotukuka ya kuonyesha ufisadi kutoka chama cha mafisadi. TEKELEZA WAJIBU WAKO, JIONDOKEE NA USISUBIRI SHUKURANI. HAWA NDO WALIMWENGU, hawanaga jema.
Acha kuwa na mahaba ya kijinga. Watu wamekata rufaa wewe unasema Zitto ameibua, ujinga uliopitiliza. Uvivu wa kusoma na kufuatilia mambo uliowagubika nyie watanzania usifanye mtu aliyeibua kitu cha kawaida sana kama hiki kuwa ndio shujaa wenu.
 
Back
Top Bottom