beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka watazamaji wa uchaguzi wa ndani na wa kimataifa, waliopewa idhini na tume hiyo kuangalia uchaguzi mkuu, watekeleze wajibu wao kwa mujibu wa mwongozo na sheria iliyowateua.
Tume hiyo imewaonya waangalizi hao, kuepuka kuingilia au kuvuruga mwenendo wa uchaguzi na kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, tume hiyo imesema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, imeteua maofisa 329,864 kutoka maeneo mbalimbali kuwa sehemu ya timu ya watu watakaoshiriki kusimamia uchaguzi mkuu Oktoba 28.
Akizungumza na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na kutoka nje ya nchi, Dar es Salaam jana, Mjumbe wa NEC, Balozi Omar Mapuri alisema maandalizi ya uchaguzi huo yanaenda vizuri na vifaa vyote muhimu vingi vimeshafika majimboni na kwasasa vinasubiri kupelekwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Alisema NEC imetoa idhini kwa taasisi za kimataifa 17 kuwa watazamaji wa uchaguzi mkuu. Alisema taasisi za ndani zilizoidhinishwa ni 97 na wakalimani wa lugha wako 28.
Aliwataka waangalizi hao kuzingatia sheria, Katiba ya nchi na miongozo inayowaongoza kufanya wajibu wao wa utazamaji katika uchaguzi huo na kuhakikisha hawaingilii mwenendo wa uchaguzi au kusababisha vurugu.
“Cha msingi hapa kwa watazamaji wa ndani na wa nje kuzingatia sheria, Katiba ya nchi na miongozo iliyowapa kibali cha kutekeleza wajibu wenu huo, msiingilie au kuvuruga mwenendo wa uchaguzi, watakaokiuka sheria itachukua mkondo wake,’’ alisema Balozi Mapuri.
Alisema awali waangalizi hao, walipeleka maombi NEC ya kuteuliwa na jumla ya maombi 14,575 yalikubaliwa na kupewa idhini.
Kila mmoja alipewa vitu vyote muhimu ikiwapo miongozo iliyoandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, taratibu, majukumu yao, mipaka yao na kutakiwa kuisoma na kuielewa.