NEC yaigwaya CCM...Je kutakuwa na uchaguzi halali mwaka huu?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC yaigwaya CCM...Je kutakuwa na uchaguzi halali mwaka huu??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu66, Sep 10, 2010.

 1. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mabango ya CCM yaipasua kichwa Nec
  Thursday, 09 September 2010 22:31


  Fredy Azzah
  SIKU nne baada ya katibu mkuu wa CCM kudai kuwa mabango ya mgombea wao wa urais hayana matatizo kwa sababu yalipitishwa kihalali, Tume ya Uchaguzi (Nec) imetumia siku mbili kujadili suala hilo lililoibuliwa na Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa.


  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa aliitaka CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu, ikiwa ni pamoja na mabango hayo ya kampeni yanayoonyesha picha za majengo ya ofisi na makazi hayo ya mkuu wa nchi, lakini chama hicho tawala kikatia ngumu kikisema hakitayaondoa kwa sababu yalipitishwa na Nec.


  Tendwa alitoa tamko hilo baada ya baraza hilo la ushauri kutaka CCM iache kutumia nyenzo hizo za Ikulu, zikiwemo picha hizo zinazoonyesha majengo ya Ikulu.
  Lakini habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Nec imetumia siku mbili kujadili mabango hayo yanayodaiwa kuihusisha Ikulu kama sehemu ya kujinadi kwa wapiga kura.
  Naibu katibu wa elimu ya mpigakura na habari wa Nec, Ruth Masham alilieleza gazeti hili jana kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa na tume hiyo tangu juzi na hadi mwandishi alipoondoka kwenye ofisi za tume hiyo kikao kilikuwa bado kinaendelea.


  "Mkurugenzi (wa uchaguzi, Rajabu Kiravu) kanipa maneno matatu tu ya kuwajibu. Hilo suala la mabango bado linajadiliwa," alisema Masham.
  "Jana (juzi) mpaka naondoka ofisini niliacha wakijadili suala hilo na hata sasa wanaendelea kulijadili, na mkurugenzi kaniambia hata mkienda ninyi, ni majibu hayo hayo atakayowapa."


  Alisema juzi kamati ya maadili ya Nec ilimhoji mwakilishi wa CCM juu suala hilo na kuwa hivi karibuni tume hiyo itatoa majibu rasmi ya suala hilo.
  "Mwakilishi wa CCM alikuwa hapa jana kwa ajili ya suala hilo, kwa sababu katika mikutano yao wanazungumzia pia mambo mbalimbali... siwezi kusema siku ya kutoa tamko lakini ni hivi karibuni," alisema Masham.
  Katibu wa kamati moja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kutokana na kile alichosema kuwa si msemaji, alikiri kujadiliwa kwa jambo hilo jana na kamati hiyo.
  "Najua kuwa jana walijadili hilo suala, lakini mimi si msemaji wa Nec na pia hata katika mkutano wa jana (juzi) mimi sikuingia. Kwa hiyo nenda kwa mkurugenzi wa Tume atawapa majibu mazuri zaidi," alieleza.

  Akitoa tamko lake, Tendwa alisema: "Picha za kampeni za CCM zinazoonyesha Ikulu zisitumike. Ukitumia hizo picha halafu chini yake ukasema chagua chama fulani, hiyo itakuwa siyo demokrasia... kwanza hata aliyepiga hizo picha ni mfanyakazi wa Ikulu."
  Kwa mujibu wa Tendwa, picha hizo pia zinawashawishi wananchi kuipigia kura CCM na kuwa vyama vingine haviwezi kuzipata kutokana na kutoweza kupiga picha katika eneo hilo.


  Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema katika orodha ya mabango yao hakuna hata moja lenye picha ya Ikulu na kusisitiza "kama lipo njoo sasa hivi ofisini, ili twende ukanionyeshe lilipo".
  "Hakuna bango lenye picha ya Ikulu, liko wapi? Naomba hili jambo lizungumzwe watu wakiwa wanalielewa vema. Wewe umeliona wapi hilo bango lenye picha ya Ikulu?"

  Makamba alipoelezwa kuhusu tamkoa la Tendwa, alisema: "Sikiliza bwana, sisi hatukukurupuka tu kuweka haya mabango. Mabango yetu; nasisitiza tena, yamepata baraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)."

  Hata hivyo, juzi mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame alinukuliwa na gazeti dada la The Citizen, akionya kwamba tume yake haijaruhusu mabango ambayo yanakiuka taratibu.

  Source: Mwananchi
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Eti kuna bango linesema Jk rafiki wa watoto.....kweli ukiwa hun a sera ni shida sana.rafiki wa watoto then what
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Then watoto wampigie kura.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Campaign manager anaweza tuambia alikuwa anamaanisha nini kwa msg kama iyo kwa watotot,au labda walitaka liandikwe JK anawapenda wafanyakazi jamaa wakawa wamekosea
   
Loading...