Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1. Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a)

2. Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1) (b);
 
Je,mgombea anaweza kuwa kwenye timu ya kampeni ya mgombea mwingine?
Jibu unalotafuta hapo ni lile la wanafunzi wa darasa la pili. Aliyeko la saba anaelewa sana, ukimuuliza baba yako ni nani, akisema huyu ni mume wa mama inatosha. Yaonekana Lissu hakujua hilo na hakuitumia nafasi hiyo kwa uzembe. Sijui kwa nini hakujiuliza 2015 waliomsindikiza Lowasa walikuwa wanatafuta nini!
 
Jibu unalotafuta hapo ni lile la wanafunzi wa darasa la pili. Aliyeko la saba anaelewa sana, ukimuuliza baba yako ni nani, akisema huyu ni mume wa mama inatosha. Yaonekana Lissu hakujua hilo na hakuitumia nafasi hiyo kwa uzembe. Sijui kwa nini hakujiuliza 2015 waliomsindikiza Lowasa walikuwa wanatafuta nini!
Jibu swali!
 
Walikuwa wapi kipindi chote wasitoe ufafanuzi?

Je, Waziri mkuu anamfanyia kampeni rais na kutoa ahadi za kuagiza utekelezaji kama nai maana huku anatajwa kama mjumbe wa kamati ya kampeni na si waziri mkuu?

Je, sheria inamruhusu mjumbe kufanya kampeni eneo ambalo mgombea hayupo, na kama ndivyo, je ratiba si zitaingiliana na wagombea wengine?

Je, huyo waziri hakuwa na mpinzani kule ruangwa?
 
Walikuwa wapi kipindi chote wasitoe ufafanuzi?
Je Waziri mkuu anamfanyia kampeni rais na kutoa ahadi za kuagiza utekelezaji kama nai maana huku anatajwa kama mjumbe wa kamati ya kampeni na si waziri mkuu?

Je sheria inamruhusu mjumbe kufanya kampeni eneo ambalo mgombea hayupo, na kama ndivyo, je ratiba si zitaingiliana na wagombea wengine?

Je huyo waziri hakuwa na mpinzani kule ruangwa?
Hahahhaha.. Washabiki wa Lisu ni wajinga sana aisee!

Sheria zipo na Lisu anaejifanya kujua sheria hatukutegemea kuhoji swali la kipopoma kama hilo
 
Back
Top Bottom