NEC ya CCM yatofautiana na REDET na SYNOVATE kuhusu umaarufu wa Dr. Slaa...........


Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,613
Likes
610,864
Points
280

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,613 610,864 280
Pamoja na hisia kubwa zilizojengeka miongoni mwa jamii kuwa Dr. Slaa ndiye aliyeshinda kinyang'anyiro hiki cha Uraisi lakini tathmini ya kura za maoni za REDET SYNOVATE ambao ni wadau wa CCM zilimbeza mno Dr. Slaa wakati hata NEC ambayo ni mdau asilia wa CCM iliona angalau impe Dr. Slaa 26.34% ya kura zote ili kuupaka ushindi wa Jk mafuta ya uhalali feki.................

REDET na SYNOVATE zilimkandamiza kwa makusudi mazima Dr. Slaa kwa kushindwa hata kumpa 20% ya kukubalika lakini NEC ya CCM imemwonea haya na kumfariji kwa 26.34%..........

Tungependa REDET na SYNOVATE watueleze huu uchakachuaji wao wa kumkandamiza Dr. Slaa ulifanyika kwa sababu zipi zile................

Maoni yao yalichangia kuvipotosha vyombo vya habari na wapigakura kuwa JK alikuwa anatarajiwa kuwa Raisi huku ni asilimia 27 ya waliojiandikisha kupiga kura ndiyo waliokuwa wanamuunga mkono na hivyo kufanya makisio ya kukubalika kwa JK kuwa yalikuwa ni ya upotoshaji tu............

Yawezekana kabisa, idadi ya wapigakura imepungua katika uchaguzi huu kutokana na kupotoshwa na REDET na SYNOVATE..............wapo wapigakura ambao hawakwenda kupiga kura kwa sababu waliona hawana sauti ya kubadilisha mwelekeo wa nchi hii baada ya porojo za REDET na SYNOVATE kuwafikia
 

babayah67

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2008
Messages
493
Likes
9
Points
35

babayah67

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2008
493 9 35
DR BANA anatakiwa atueleze uhalali wa JK kuwa Rais kwa kuchaguliwa na Watanzania 5 million sawa na 12% ya Watanzania wote. Je hii ndio Demokrasia tunayoihubiri na kuifundisha Vyuoni????? Dr BANA do you believe that hili kweli ndio chaguo la mungu??????
 

Forum statistics

Threads 1,204,797
Members 457,514
Posts 28,170,694