NEC ya CCM yamng'ang'ania Rostam; Yasema inamtambua ni mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC ya CCM yamng'ang'ania Rostam; Yasema inamtambua ni mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Bakari Kimwanga


  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema hadi sasa bado haijapata taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM).

  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu, alisema kuwa hadi sasa bado ofisi yake haijapokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge ya kumtaarifu kujiuzulu kwa mbunge huyo.

  "Sina hakika kama tume imepokea taarifa hizo lakini kwa kuwa mimi niko likizo siwezi kuzungumzia suala hili kwa undani zaidi na kama sula hili likifika ofisini naamini litakuwa wazi kwa mujibu wa sheria ni vema wananchi na hasa vyama vya siasa vikavuta subira juu ya jambo hili.

  Kutokana na majibu hayo ya mkurugenzi huyo wa Tume ya Uchaguzi, Tanzania Daima ilimtafuta Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, ili kuweza kupata maelezo ya kina kuhusiana na suali lakini hakupatikana ofisini kwake wala kwa njia ya simu.

  Julai 24, mwaka huu, ofisi ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo ilisema kuwa tayari imemwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame, kumjulisha juu ya kuwa wazi kwa kiti cha ubunge katika jimbo la Igunga.

  Spika Makinda alisema alifikia hatua hiyo baada ya kupokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz, ambaye alijiuzulu Julai 13, mwaka huu, nafasi hiyo na nyadhifa alizokuwa nazo ndani ya Chama cha Mapinduzi na kubaki mwanachama wa kawaida.

  Akizungumza na waandishi mwishoni mwa wiki iliyopita, Kaimu Katibu Mkuu wa Bunge, John Joel, alisema Spika Makinda alipokea barua ya Rostam Julai 19 akimjulisha rasmi kujiuzulu nafasi hiyo.

  Alisema kuwa kwa mujibu wa barua ya Rostam aliyoiandika Julai 15 mwaka huu ilipokewa na Spika Julai 20, hivyo kwa utaratibu wa Bunge ni lazima wapitie vifungu vyote vya sheria ili kubaini kuwa alijiuzulu kwa hiari yake na hapakuwa na shinikizo.

  Joel alisema baada ya kupitia vifungu hivyo na kujiridhisha, waliona kuwa Rostam alifikia uamuzi huo kwa ridhaa yake pasipo kushawishiwa.

  Alisema kuwa katika nukuu ya barua hiyo, Rostam alisema alifanya uamuzi huo kwa kuzingatia Ibara ya 71 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  "Taratibu za mbunge kujiuzulu zimefafanuliwa katika Katiba na Sheria ya Uchaguzi Ibara ya 149 inayoelekeza kwamba mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba ikiwa ni pamoja na kazi ya waziri, naibu waziri au mbunge, isipokuwa mbunge ambaye ni mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake."

  Aliongeza: "Anaweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiwa sahihi kwa mkono wake, ibara hiyo inafafanua zaidi kuwa kwa mbunge anayetaka kujiuzulu atawasilisha taarifa yake ya kujiuzulu kwa Spika."

  Alisema Ibara ya 149 (2) inafafanua zaidi kuwa mtu anayetoa taarifa ya kujiuzulu atahesabiwa kujiuzulu tangu siku taarifa yake ilipopokewa katika ofisi ya Bunge.

  Joel alisema kuwa mishahara pamoja na posho nyingine husimamishwa mara baada ya Spika kupokea barua hiyo na kwamba mafao atakayolipwa ni yale ambayo yalitokana na yeye kukaa ndani ya Bunge.

  Rostam alijiuzulu nafasi hizo kwa maelezo ya kuwa aliona ni afadhali awape nafasi wale wanaoendesha siasa uchwara na zisizo na tija, ambazo yeye hana muda nazo na hawezi kuwa sehemu yake.

  Alisema haoni sababu ya kuendelea kuvutana na viongozi wa chama chake na wanachama wenzake katika mambo ambayo yanaweza kumalizwa kwa njia muafaka.

  "Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM, haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba.

  "Nimeuchukua kwa dhamira ya dhati uamuazi wa kuachana na siasa hizi uchwara na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu," alisema.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM NEC watalala Masikini hakuna Pesa za Rostam; Kwahiyo Uchaguzi wa Rais itakuwa ni Utamu 2013 or 2014
   
 3. N

  Nipe tano Senior Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nngu007,
  Ni magwanda ndo yanakusumbua au this was your wishfully thinking? SIAMINI KAMA HUWEZI TOFAUTISHA KATI YA NEC YA TUME YA UCHAGUZI NA NEC YA CCM KAMA ULIVYO INTRODUCE THREAD
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hao wanachelewesha muda wa uchaguzi mdogo! Wameambiwa wasubiri ccm wajipange maana hakuna dalili za kutetea jimbo!
   
 5. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  We Magamba, nec ya tume ya uchaguzi na nec ya ccm si ni kitu kimoja? Kwani nani asiyejua kuwa tume ya uchaguzi siyo ya taifa bali ni tume ya uchaguz ya ccm? Are Kiravu and Makame not ccm puppets who r in the payrolls of corrupt ccm bulls?
   
 6. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata hiyo NEC ya uchaguzi ni ya ccm unabisha nini mkuu? Mbona hii kitu inaeleweka hata kipindi mhimu cha uchakachuaji kikifika, nec huwa inasimamia shoo nzima..
   
 7. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  acha wakatae lakini hilo jimbo limeenda upinzani tangu siku rostam alipotangaza kuliacha..
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Kama CDM kitaweza kulichuku jimbo hili basi itakuwa ni dalili njema ya kuiteka rasmi Tabora...mipango inatakiwa kuanzia Igunga ili kuichukua Tabora nzima,Igunga for capturing Tabora Operation,ITO!!
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuwa mwelevu, jamaa anamaanisha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendeshwa na CCM na sio kwa maslahi ya wananchi!!!!!!!
   
 10. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watajua tu ngoja wajishebedue kidogo.
   
Loading...