OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 669
Waungwana katika kupambana tunajua zikitokea fursa huwa tunazichangamkia kwa nguvu sana. Kila mwaka wa uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi huwa inatoa nafasi za kazi za muda mfupi ili kusaidia shughuli za uchaguzi.
Ni wazi kuwa kwa miaka mingi kazi hizi zimekuwa zikiwa njia sahihi ya walimu kuomba na mara nyingi wamekuwa wakipata, lakini hiki sio kigezo pekee kwa kigezo cha msingi ni mtu kutokuwa na chama cha siasa.
Ni wazi kuwa hatuna mfumo wa moja kwa moja wa mtu kujulikana bila mashaka kwamba ana kadi au hana kadi ya chama fulani, kutokana na ufinyu wa matumizi ya teknolojia.
Swali langu linakuja kuwa ni kwa njia zipi NEC wanahakikisha kuwa wanayemchagua kusaidia shughuli za uchaguzi hana ushabiki na chama cha siasa.
Kwa kuwa kuandika barua kuwa mtu hana chama haimaanishi hana chama, lakini kama kungekuwa na mfumo centralized labda ingekuwa rahisi.
Nauliza hivi kwa sababu zisizo za kisiasa:
Signed
OEDIPUS

- Inawezekana wasio na vyama wakaachwa kwa kuwa hakuna mfumo wa kumjua asiye na chama
- Nafasi hizi zinaweza kuwa ni sehemu ya kuwapa posho waalimu tu huku wengi wasio na ajira wakikosa walau neema kwa kipindi hiki
Signed
OEDIPUS