Elections 2010 NEC wanahakiki vipi matokeo?

shimbe

New Member
Mar 16, 2009
1
0
Nimemsikia mwenyekiti wa NEC anadai kuwa wao wanahakiki matokeo ya urais yanayotoka kwenye majimbo na wakigundua yamekosewa wanayarekebisha.Hapa kwa kweli, sijamuelewa!anahakiki vipi wakati wanpokea figures tu? watajuaje kuwa figures hizo zina makosa wakati wao wako Dar na uchaguzi umefanyia mbali? Ina maana wanaletewa form za matokeo ya kila kituo?Hapa si ndipo uchakachuaji unapofanyika?
 
ni kweli unachoöngea. haiji akilini kuwa mtu yupo Kazozibakaya au twabagondozi then unasema unahakiki. how? na kutoka wapi? watz sasa hivi havtaki kudanganywa. kwa ujumla sikubaliani na tamko lake la jana
 
Labda kuna watu walipiga kura ofisini kwao

Bse unahakiki kura za Makete DSM?Au za Mbambabay DSM wapi na wapi?
 
Makame yupo sahihi ila ninyi hamjamwelewa. Naomba nikueleweshe hivi: Makame kapewa maagizo kwamba ampe kiasi fulani cha kura, hivyo akiona haiendani na kile alichoambiwa inabidi ahakiki (arekebishe). Kuna nni cha ziada.

Jamani Watanzania tulihangaika kupiga kura lakini Tume tayari walikuwa na matokeo.
 
Nimemsikia mwenyekiti wa NEC anadai kuwa wao wanahakiki matokeo ya urais yanayotoka kwenye majimbo na wakigundua yamekosewa wanayarekebisha.Hapa kwa kweli, sijamuelewa!anahakiki vipi wakati wanpokea figures tu? watajuaje kuwa figures hizo zina makosa wakati wao wako Dar na uchaguzi umefanyia mbali? Ina maana wanaletewa form za matokeo ya kila kituo?Hapa si ndipo uchakachuaji unapofanyika?

safi kabisa.. hili ni swali zuri sana na linalenga kugusa mojawapo ya matatizo niliyoyaona mimi pia. Yawezekana katika kuhakiki wakikuta makosa kwenye fomu wanampigia simu Msimamizi wa Jimbo na kumuuliza "hivi hapa mlimaanisha namba ngapi?" halafu wakiambiwa wanabadilisha... Vinginevyo waandishi wanatakiwa kumuuliza huyo mwenye tume.. wanahakiki vipi matokeo?
 
Back
Top Bottom