Elections 2010 NEC wako wapi wakati JK anawatumikisha watoto kazi kwa kuhudhuria kampeni zake?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kama umesoma Mwananchi Jumapili ya leo ukurasa wa 4 JK anaonekana akisalimiana na watoto wadogo chini ya miaka kumi hivi kwenye kampeni zake. Watoto hao wadogo hawajafikisha umri wa kupiga kura na siyo sahihi hata kidogo kuwatumikisha watoto wadogo kwenye shughuli yoyote ile hususani hii yenye mtaji wa kisiasa kwa mgombea.

Sheria ya ajira inayokataza watoto kutumikishwa kazi JK ameikiuka kikamilifu na bado anataka awe au aendelee kuwa Raisi wetu na huku anazibeza sheria za Nchi ambazo yeye mwenyewe alizisaini..............Kuhudhuria shughuli za kampeni hizi kwa watoto ambao wazazi wao wanajua wapo shuleni wakisoma kumbe siku hiyo wamechukiuliwa mkuku-mkuku kwenda kujaziliza kadamnasi ya watu baada ya viongozi wa CCM kuona mgombea wananchi wamemkataa na ukiukwaji wa maadili wa hali ya juu.

Watoto hao angalau basi walipaswa kuandamana na wazazi wao vinginevyo NEC imkaripie huyu bosi wa CCM proper
 
Nadhani upo sahihi....NEC wana wajibu ya kuyatolea matamko matokeo kama haya, waangalie nao historia isijewahukumu!
 
Heee hao ni akina kadogoo wa DRC...nafikiri kuna kesi ya kujibu...lakini pia walikuja kuona buradani.
 
Kama umesoma Mwananchi Jumapili ya leo ukurasa wa 4 JK anaonekana akisalimiana na watoto wadogo chini ya miaka kumi hivi kwenye kampeni zake. Watoto hao wadogo hawajafikisha umri wa kupiga kura na siyo sahihi hata kidogo kuwatumikisha watoto wadogo kwenye shughuli yoyote ile hususani hii yenye mtaji wa kisiasa kwa mgombea.

Sheria ya ajira inayokataza watoto kutumikishwa kazi JK ameikiuka kikamilifu na bado anataka awe au aendelee kuwa Raisi wetu na huku anazibeza sheria za Nchi ambazo yeye mwenyewe alizisaini..............Kuhudhuria shughuli za kampeni hizi kwa watoto ambao wazazi wao wanajua wapo shuleni wakisoma kumbe siku hiyo wamechukiuliwa mkuku-mkuku kwenda kujaziliza kadamnasi ya watu baada ya viongozi wa CCM kuona mgombea wananchi wamemkataa na ukiukwaji wa maadili wa hali ya juu.

Watoto hao angalau basi walipaswa kuandamana na wazazi wao vinginevyo NEC imkaripie huyu bosi wa CCM proper

Huu ni upupu? umeona wamebebeshwa kokote? au wanachimba mitaro. sheria imeeleweka vibaya hapa.
 
Hao wazee wa NEC wamekaa pale tu kama matoy, hawana ubavu wa kumlipia kikwete. Atakachosema kikwete ndo watakachofanya. Nashukuru hao wazee(makame na kiravu) si ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom