NEC wagoma kuwaapisha mawakala wa CHADEMA, hii ndio Tanzania

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Mawakala CHADEMA wanyimwa viapo Kinondoni

Leo ikiwa ndiyo siku ya kuwatambulisha na kuwaapisha mawakala kwa ajili ya Uchaguzi wa Marudio Jimbo la Kinondoni, Mawakala wa CHADEMA wamekataliwa kuapishwa. Awali tulibaini tatizo hilo Kata ya Hananasif ambapo Mtendaji wa Kata aitwae Richard Supu (0655998777), aligoma kuwaapisha mawakala hao akiwataka waache majina yao hadi atakapowaita siku tatu kabla ya siku ya kupiga kura. Jambo ambalo ni kinyume cha taratibu zinazosimamia uchaguzi. Yeye amesisitiza kuwa ndivyo inavyofanyika na hawezi kufanya tofauti.

Taarifa zaidi zimeonesha kuwa karibu watendaji wa kata wote katika jimbo hilo, wamefanya hivyo kwa mawakala wa CHADEMA. Hakuna sababu yoyote ya msingi inayotolewa na wahusika kuhusu dalili hizo mbaya kabisa za kuzidi kuvuruga Uchaguzi huo. Hali hiyo ndiyo ambayo wasimamizi wa uchaguzi katika Kata ya Saranga (kati ya zile kata 43) walifanya.

Tayari chama kimewasiliana na NEC kuingilia kati suala hilo kwa haraka na kuwataka wasimamizi hao waache kutumika kufanya hila za kuharibu uchaguzi huo.

Makene
 
sasa waliogoma ni nec au watendaji? mbona hujaeleweka vizuri na source ya habari ni ipi?
 
Eti NEC iingilie kati! Try to be serious.

Kama mnategemea NEC hii hii ndiyo iweke hayo mazingira mtakuwa wapumbavu tofauti nilivyokuwa nawafikiria awali.

Kilichofanya msuse kule si ni hao hao NEC?
Sasa nani aingilie kati kama wa ccm wameapishwa chadema wasubiri siku 3 kabla ya uchaguzi, na zikifika hizo siku 3 wanazima simu na kupotea ofisini hawataonekana
 
sasa waliogoma ni nec au watendaji? mbona hujaeleweka vizuri na source ya habari ni ipi?
Watendaji wa kata ni wawakilishi wa nec wao wanamwakilisha mkurugenzi ambbaye ndiyo returning officer wa jimbo husika. Kumbuka nec haina watumishi wake huko majimboni na hili linafanywa makusudi kabisa ili kurahisisha upatikanaji wa bao la nape
 
Lazima kuna tatizo na sio bure,,Nec hawawezi kufanya jambo hilo bila sababu..Chadema na sisi tunajifanya wajuaji sana ,ukute kuna kitu lazima..tusubiri tuone
Basi hayo matatizo kwa chadema tu, tunaona figisu figisu wanazofanyiwa hawa cdm, sidhani ama unavyosema kuna tatizo, wacha wakubwa watakuja kusema tatizo ni nini, inahuzunisha kwa kweli
 
nitashangaa sana kama chadema watashindwa kupambana na jama hizo hapo dar. kwa nini wasiwakabe kina kailima hapo? mbona ni karibu tu. kwa tume hii upinzani kushinda bila nguvu ya umma wasahau.
 
Makene atuambie sababu ni nini ya mawakala wote wa kata 10 za kinondoni kukataliwa, au hao maofisa waje na majibu kwanini wamekataa, ila kata zote, hapana kuna hujuma hapa, ingekuwa kata 1 sawa, lakini 10, halafu wanaambiwa siku 3 kabla ya uchaguzi, si ndio mambo yale ya kuzima simu zao na kupotea ofisini kama uchaguzi wa madiwani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lazima kuna tatizo na sio bure,,Nec hawawezi kufanya jambo hilo bila sababu..Chadema na sisi tunajifanya wajuaji sana ,ukute kuna kitu lazima..tusubiri tuone
Lkn jiulize , Je Chadema ndio mara ya kwanza kuingia kwenye chaguzi ? Kama NEC wamebadili utaratibu si wanapaswa kuviarifu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi?

Vv
Uchaguzi ukiharibika ni nec mkuu... Ndio maana nchi ikiongozwa vibaya inalaumiwa ccm
 
Ujinga wa watendeji wa kata unaweza ukaanzisha vuguvugu LA hatari na kupelekea machafuko yanayoweza sambaa mkoa mzima.
 
Back
Top Bottom