Misterdennis
JF-Expert Member
- Jun 4, 2007
- 1,741
- 480
Duuuuuh,very unproffesional
Hivi kwelu ndugu, ulishawahi kuona mambo ya serikali ya bongo yanaendeshwa professionally? Hilo neno halipo kabisa kwenye misamiati yao!!
Duuuuuh,very unproffesional
bi mkora hiyo inawezekana, nadhani wakiangalia jumla ya kura zilizopigwa na matokeo yake basi wanaweza kuchukulia Adv'ge ya kuvunja uchaguzi
Mbwewe zote zile ooh matokeo ya uraisi ndani ya siku moja, mara ooh! ITC iatatumika vilivyo kuhakikisha speedy reporting zimeishia wapi???????? Yaani kumbe ni uchuro tu!
Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini na Nkenge.
Pia uchaguzi wa madiwani katika kata takribani 20 hautafanyika kutokana na kupungua kwa vifaa
Jana usiku NEC wametangaza kuahirisha uchaguzi katika majimbo matatu na kata nyingi tu mpaka tarehe nyingine itakayopangwa na kutangazwa hapo baadaye.
Sababu ya kuahirisha ni ukosefu wa vifaa.
My take:
Kwa nini NEC hawajifunzi kutoka NECTA kusambaza vifaa?
CCM wana hila wanataka kuarishwa ili wajizatiti kwa kuhonga
Mh, mnaweza kusikia UCHAGUZI UMEAHIRISHWA NCHI NZIMA!
Miafrika in action. Na bado
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.
Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-
1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)
2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:-
Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.
(Rajabu R. Kiravu)
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Naomba Watu wa sheria wafafanue hili, kama Uchaguzi katika majimbo hayo hayatafanyia je Matokeo ya Urais yatasubiri mpaka na Ndugu zetu wengine wapige Kura?
Ufafanuzi Tafadhali
Wewe vipi? Kura zilizoahirishwa ni kura wabunge au/na madiwani... sasa kura za Rais zinaathirika je?
Ufafanuzi: Uchaguzi wa Rais Unaendelea kama kawaida.
Na majimbo haya ya uchaguzi; Uchaguzi wao utarudiwa.