NEC: Tutamtangaza mshindi halali Igunga

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemtaka Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Protas Magayane, kuhakikisha anatangaza matokeo halisi ya uchaguzi huo bila kuingiliwa, kushurutishwa wala kutishwa na chama cha siasa, taasisi au mtu yeyote mwenye mamlaka ya juu serikalini ili kuepusha machafuko.

Mwenyekiti wa muda wa NEC, Profesa Amon Chaligha, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba wangependa kuona hali ya amani inaendelea kuwepo jimboni humo hata baada ya uchaguzi na namna pekee ya kuidumisha ni kutangaza matokeo sahihi na ya kweli.

My take: Wanaposema watamtangaza mshindi halali kwani siku zingine huwa wanafanyaje.
 
inamaanisha igunga kila aliykuwa anashinda alikuwa anashinda kimagumashi lakini safari hii wanataka mshindi awe ameshinda kihalali.na huu ni mwanzo mzuri kuelekea 2015.somo alilotoa mwana mama wa zambia naona limeanza kueleweka.mia
 
Kamba ya utawala wa CCM kukatikia Igunga endapo mtu yeyote, chombo chochote kitachezea kura halali za Wa-Tanzania zitachezewa kama hapo mwaka jana. Machalii hili halina ubishi.
 
inamaanisha igunga kila aliykuwa anashinda alikuwa anashinda kimagumashi lakini safari hii wanataka mshindi awe ameshinda kihalali.na huu ni mwanzo mzuri kuelekea 2015.somo alilotoa mwana mama wa zambia naona limeanza kueleweka.mia
Mara zote wanaingiliwa katika maamuzi ila safari hii hawataingiliwa, tunashukuru sana NEC kwa kutoa siri tumewasamehe lakini hatutawasahau.
 
mmmh sijaelewa kidogo labda kwasababu sijaenda lunch; subiri nikirudi ntauliza swali moja tu kwamba, mshindi halali yukoje na ambaye siye halali yukoje? je hao waliowahi kutangazwa walikua katika category gani kati ya hizo? na Je, kuna nini hadi watangaze hivyo? kuna nguvu gani iliyowasukuma kusema hivyo? ina maana kuna walioko madarakani ambao sio "halali"? Kaaaazi kweli kweli.............
 
safi sana wameona cha moto na moto wameuona unakuja mbele yao magamba wanalo wamezoea kuiba na saizi wanaona akuna ujanja hata kidogo
 
Kwa maana hiyo mara zote walikuwa wanatuibia tu!?,kweli hii ni Tz zaidi ya uijuavyo.
 
Danganya toto tu hio, wanataka watu-fool, hamna lolote hapo,si utaona?
 
inamaanisha igunga kila aliykuwa anashinda alikuwa anashinda kimagumashi lakini safari hii wanataka mshindi awe ameshinda kihalali.na huu ni mwanzo mzuri kuelekea 2015.somo alilotoa mwana mama wa zambia naona limeanza kueleweka.mia
Sometimes mkwara nao huwa unasaidia hebu sikiliza huu........

Last edited by a moderator:
Hapo wenye akili zetu tumekunyaka Mkuu kwamba miaka yote mnatangazaga matokeo kutokana na shinikizo kutoka serikalini. Lakini tunajua kwamba si mapenzi yako kutamka ulichotamka bali mmeshapata fundisho kwamba CDM hatutakubali kuchakachuliwa na hilo umeliona na advertise ya kwanza uliishuhudia kwa Mkuu wa Wilaya mliyemtuma kupima upepo mkapata jibu kwamba mwaka huu Watanzania hawataendekeza tena ujinga ujinga wa nec na Serikali. Na kama unataka kuona itakuwaje, jaribuni kuiba this time.
 
Mara zote wanaingiliwa katika maamuzi ila safari hii hawataingiliwa, tunashukuru sana NEC kwa kutoa siri tumewasamehe lakini hatutawasahau.
Kwa CCM hizo ni ndoto, hata lile lizee lililostaafu lilisema hivyo hivyo wakati wa uchaguzi wa Octoba 2010, lakini kilichokuja kutokea nadhani jibu unalo, bila aibu walichakachua hadi kura za RAISI Dr. Slaa. Rushwa waliopokea iliwafanya wawetayari hata kama watanzania wangechinjana kama KUKU wao kwao ilikuwa ni sawa tu. Limebaki jinga moja hapo kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi sijui litastaafu lini. Pumbafu kabisa. Pinda ndiye amepangwa kuwa kinara wa uchakachuaji wa kura huko Igunga. Ila iko siku kitaeleweka tu.
 
Wanafikiri sisi ni MAZUZU siyo??? Kizuri alichokifanya ni kutowekea siri wazi ila behind the cine bado wanapanga namna ya kuwaliza wana Igunga!!
 
Igunga hakuna mshindi halali bali mwenye nguvu ndiye ataibuka mshindi. NEC msitudanganye.
 
Hakika huyo prof ambaye anakaimu chairperson wa Nec anajharibia kupata permanent deal. Kwa tamko lake lenye uadilifu litamgharimu.yaan ameivua nguo serikali ya wahuni Ccm..
 
Mara zote wanaingiliwa katika maamuzi ila safari hii hawataingiliwa, tunashukuru sana NEC kwa kutoa siri tumewasamehe lakini hatutawasahau.
Hili nalo linatia mashaka lakini hii inatokana na baadhi ya vyama kulalamikia tume hii juu ya utendaji wake kazi kuwa ni kibabaishaji na umekuwa ukiingiliwa na wanasiasa hususani chama tawala. Yetu macho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom