Elections 2010 NEC toeni majina ya wapigakura tuyaone kwenye mtandao

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,516
1,865
Wakati zimebaki takribani siku 26 hivi, NEC itoe majina ya watu wanao tarajia kupiga kura ili kila mtu siku ya kupiga kura ajipange kwenye eneo sahihi ili kuokoa kupoteza muda.

Hakuna haja ya kubandika majina badala yake yawekwe kwenye mtandao kila mtu ajione atakuwa kituo gani na eneo gani. Mfano, Kinondoni - manyanya C, au Mwenge stendi, G.

Wadau mnasemaj kupunguza usumbufu wakati wa zoezi la kura?
 
Asante kwa post yako nzuri na imekuja wakati muafaka. NEC hawawezi kutoa majina katika mtandao kwa sababu daftari liko hovyo kabisa, nyie mtaona siku ya kupiga kura!

Watabanika majina kwenye vituo vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi, ni siku chache mno mtu kufanya chochote iwapo jina lake litakuwa halipo -- kama vile tu ilivyokuwa mwaka 2005. Mwaka ule walibandika majina hayo lakini bila ya utaratibu unaoeleweka wa kupetition. Katika jimbo la Temeke majina 100,000 hayakuonekana siku ya kupiga kura.

Inanikumbusha mwaka 1995 uchaguzi mkoa wa Dsm ulivyvovurugwa na NEC na walipotangaza kurudiwa hawakuweka utartibui mzuri na matangazo kwa kujiandikisha upya kwa wale waliokuwa wamezirarua kadi zao kwa hasira.
 
Excellent idea. NEC ina majina yote kwenye kompyuta na ni kiasi tu cha kuyaweka kwenye website yao kama hawaogopi kuwa uchakachuaji wao utabainika. Tatizo la wapiga kura kukosa majina yao katika maeneo waliojiandikisha ni kubwa na ni makusudi kwani mchezo wa kuwapa "mabakia ya wajumbe wa CCM wa nyumba kumi" kazi ya kuorodhesha shahada za wapiga kura wa CCM kwenye maeneo yao ina malengo ya kuiwezesha Tume ya Uchaguzi kuhamisha sehemu kubwa ya majina ya wapiga kura WASIO wa CCM kutoka maeneo waliojiandikisha na kuyapeleka maeneo mengine ili kuwapa usumbufu hadi wasindwe kupiga kura.

Pili kwa kuweka mambo yote waziwazi - majina ya wapiga kura yakiorodheshwa na vituo vyao vya kupigia kura - kutaondoa pia dukuduku kuwa kuna wapiga kura hewa na vituo vya kupigia kura hewa yote hayo kwa lengo la kuchakachua matokeo halisi ya kura. Kama hoja hii si kweli basi NEC iweke daftari la wapiga kura na vituo vyao vya kupigia kura kwenye mtandao kuanzia sasa hivi na libaki daima kwenye mtandao.
 
Back
Top Bottom