Nec Resolution Dodoma...

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
854
127
Wananchi wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu nini kitaamuliwa huko kwenye kikao cha NEC.......Sasa nawaleteeni kwa mtizamo wangu nini haswa kilipangwa huko.....

(a)Mkapa asafishwe


``Nataka serikali itupe maelezo jinsi anavyoandikwa Rais mstaafu Mkapa huku ikiwa imekaa kimya,`` alisema Bw. Mzindakaya.

Alisema anasikitishwa na hali hiyo kwa kuwa Bw. Mkapa alifanya mambo mazuri mno wakati wa uongozi wake.

``Amelijengea taifa hili heshima kubwa? Juzi juzi tu nilikutana na wazungu wakanihoji, eti kwa nini Mkapa anasakamwa na vyombo vya habari.

Wakasema hata tuseme vipi ni bure kwani wao wataendelea kumheshimu kwa kuwa wanaufahamu mchango wake kwa Tanzania,`` alisema Bw. Mzindakaya.

Bw. Mzindakaya alisema pia anawashangaa baadhi ya Wabunge kumsema vibaya Rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu huku wakisahau kwamba, ukumbi wanaoutumia sasa, ulijengwa na yeye (Mkapa).

``Jumba hili (la Bunge), limejengwa na yeye? Kwa nini tunalitumia tena kumtukana?`` Alihoji....Source IPP MEDIA

(b)Msafisheni Lowassa na Karamagi

Karamagi amshangaa Mwakyembe

Na Mwandishi Wetu

"Dokta amesikika akisema Kamati Teule ilificha baadhi ya mambo...nani alimpa mamlaka ya kuficha ukweli, wakati Kamati ile ilikuwa ya Bunge na si ya mtu binafsi?," alihoji Bw. Karamagi ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya ripoti ya Kamati hiyo.

Alisema anashangaa kusikia hayo, wakati Kamati ile iliundwa kuichunguza Serikali na badala yake Dkt. Mwakyembe anasema kuna mambo yalifichwa kwa ajili ya kulinda heshima ya Serikali.

Bw. Karamagi alisema tangu mwanzo waliotuhumiwa walisema Kamati hiyo haikutoa ukweli wote kama alivyokiri na kuthibitisha Dkt. Mwakyembe juzi.

"Hivyo mambo haya ni dhahiri yamejikita katika masuala ya kisiasa zaidi ya ilichotumwa kutafuta ukweli wa mambo ... inashangaza pia kuwa tunavyojua kwa kawaida kamati inapopewa kazi ya uchunguzi, huwa si ya kudumu na ikishawasilisha ripoti nayo huvunjika.

"Jana (juzi) tulisikia kuwa kuna vielelezo vya ziada na hivyo Bunge litengue kanuni, mjadala urudi upya, je Kamati hiyo bado ipo? Kama haipo vielelezo anavyo nani, wanavyo au wamempa mtu awatunzie?," alihoji Bw. Karamagi.

Alitaka pia kujua kama wabunge ambao ndio walioidhinisha kuteuliwa kwa kamati hiyo waliambiwa mapema kuwa kuna vielelezo na walipaswa kujua, kwa sababu Kamati hiyo ni mali ya Bunge na si ya mtu au watu.

Alisema hiyo ni changamoto kwa Bunge ambalo sasa litatakiwa kuthibitisha kama Kamati hiyo bado ipo na kama inaweza kutengua kanuni zake na litachukua hatua gani dhidi ya kufichwa kwa vielelezo zaidi ambavyo vinatakiwa kutolewa baada ya kanuni kubatilishwa.

Aliliomba Bunge, kwamba ili suala la Richmond lisichukuliwe kisiasa kama njia ya kukomoana, kupakana matope kwa nia ya kuangushana; ili kuondoa utata iundwe tume huru ambayo haina masuala ya siasa, haishindanii vyeo, wala kuangushana na kumalizana.

"Ninaomba iundwe tume huru ambayo itagundua ukweli uliopo na vilivyojificha na vilivyoongezwa vijulikane na tume hiyo inapaswa kuundwa na majaji," alisema Bw. Karamagi.

Naye kama alivyoapa Dkt. Mwakyembe juzi, alisema kama Tume hiyo ya majaji itabaini kuwa yeye Waziri aliyejiuzulu alishirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutositisha mkataba wa Richmond, basi atakuwa tayari kuachia nyadhifa zake zote.

"Na kama itathibitika kwamba ametuhumiwa kimakosa, basi aliyemtuhumu naye ajiuzulu nyadhifa zake zote," alisema Waziri huyo wa zamani na kuongeza kuwa kauli ya Dkt. Mwakyembe ina maswali mengi zaidi ya majibu. –Source Majira

(c)Zimisha EPA na RICMONDULI na kwa kiburi

Kuhusiana na kampuni ya MEREMETA, ambayo inahusisha pia kampuni ya Tangold, Waziri Mkuu alisema suala hilo linahusisha ulinzi na usalama na kwamba si jambo la uraiani, hivyo hawezi kulizungumzia.

"Siwezi kulizungumzia, mkiona mnisulubishe kwa hilo sawa," alisema Waziri Mkuu, ambaye katika majibu yake alionekana kujiamini, huku akizungumza kwa lugha ya upole na yenye kueleweka.

Bado tumangojea Madini,Kiwira...nk... yote yanayokuja majibu yatakuwa mafupi na yaliyojaa kiburi......waswahili walishamaliza maneno, walisema MBUZI WA MASIKINI HAZAI PACHA.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom