Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,273
Kuna habari ifuatayo iliyojiri hivi mapema kuhusiana na mfumo wa siasa yetu nchini, tafadhali soma hapa chini:
Wapinzani watinga kortini
2007-10-05 17:38:14
Na Sharon Sauwa, Mahakama Kuu
Hatimaye ushirika wa Vyama vya Upinzani nchini leo umetinga rasmi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuishitaki Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ujumbe wa kwanza unaowakilisha vyama hivyo, ulitinga kwenye Mahakama Kuu leo asubuhi majira ya saa 10:30 ukiwa na wajumbe wawili kutoka vyama vya CUF na Chadema.
Wajumbe hao ni Bw. Wilfred Lwakatare (CUF) na Singo Benson ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Organization wa chama cha Chadema.
Wakiongea na gazeti hili nje ya Mahakama Kuu, wawakilishi hao wamesema wenzao kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi na TLP wangeungana nao muda si mrefu.
Wamesema katika kesi hiyo watawakilishwa na wakili maarufu, waliyemtaja kwa jina la Mpare Mpoki.
Katika malalamiko yao, wanataka mahakama itangaze kusitisha uchaguzi mdogo wa madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Hatua yao hiyo wanasema inafuatia NEC kusisitiza kuendelea na uchaguzi huo kwa maelezo kuwa wanafuata taratibu na sheria zilizopangwa.
Uchaguzi huo mdogo unaofanyika katika kata 16 za mikoa kumi ya Tanzania Bara, lengo lake ni kujaza nafasi za madiwani waliofariki dunia, kuachishwa udiwani, kujiengua uanachama wa chama walichogombea au kuhama chama.
Pia wanataka mahakama iilazimishe Tume kuhakikisha inawaandikisha raia waliofikisha umri wa miaka 18 katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Waliomo kwenye daftari hilo ni wale walioandikishwa mwaka 2004, na hivyo, wapinzani wanadai kuwa katika kipindi cha miaka mitatu kuna Watanzania wengi wamefikisha umri huo na hivyo kufanya uchaguzi bila kuwaandikisha ni kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao.
Hali kadhalika, wapinzani katika madai yao wanataka yafanyike marekebisho ya Daftari la Kudumu katika kata zitakazohusika na uchaguzi huo ili kuwapa shahada za kupigia kura wale wote waliozipoteza pamoja na utaratibu wa kuondoa majina ya watu waliokufa au kupoteza sifa za kupiga kura.
Hata hivyo Tume imeshasema kwamba Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya mwaka 1979, kifungu cha 13 (1) hutoa siku 90 kufanywa kwa uchaguzi tangu nafasi kuachwa wazi, hivyo kusitisha uchaguzi mdogo ni kuvunja Sheria.
SOURCE: Alasiri
SteveD.