Uchaguzi 2020 NEC: Matokeo ya Urais yataanza kupokelewa kuanzia usiku wa leo kutoka kwenye Majimbo

Uchaguzi huu CCM inashinda kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera amesema kuanzia leo usiku Jumatano Oktoba 28, 2020 tume hiyo itaanza kupokea matokeo ya kura za urais kutoka kwenye majimbo.

Dk Mahera ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu maandalizi ya kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais shughuli inayofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

“Tutaanza kupokea matokeo kuanzia leo na kuendelea kwa hiyo kesho tutakuwa tuko serious kupokea matokeo kutoka maeneo mbalimbali na kuyatangaza ila matokeo ya udiwani yatatangazwa kwenye kata.”

“Matokeo ya Ubunge yatakuwa yanapokelewa na kutangazwa kwenye jimbo halafu wanatutumia sisi hapa(JNICC) tunayajumlisha na kuyatangaza tena kwamba jimbo fulani tayari matokeo yake yameshatangazwa kwa nafasi ya rais,” amesema Mahera.

Dk Mahera amesema tayari ameshajiridhisha na maandalizi yote kufanikisha tukio hilo baada ya kufanya ukaguzi wa vifaa na kumbi zitakazotumika JNICC.
Hakuna tatizo wakianza kutupa yao waliyopiga kisha tujumuishe na yajayo.
 
CCM ni magwiji wa siasa za TANZANIA na AFRICA kwa ujumla na experience huwa haidanganyi.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hatoboi sababu ya kura yako moja? Umeweka kijiko cha chumvi ziwani na huyo unayemsema atashinda kwa zaidi ya 85%
Ila hongera kwa kutimiza wajibu wako
😂🤣😂🤣😂😂😂🤣😂😂😂😂😂😂🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣
 
Hatoboi sababu ya kura yako moja? Umeweka kijiko cha chumvi ziwani na huyo unayemsema atashinda kwa zaidi ya 85%
Ila hongera kwa kutimiza wajibu wako
😂🤣😂🤣😂😂😂🤣😂😂😂😂😂😂🤣😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣
 
Leo kwa tarehe ya wenzetu (tarehe 12 kwa kalenda ya kiislam) ni siku ya kuzaliwa mtume na kesho ni siku ya Maulidi.

Kesho mheshimiwa Majaliwa Kassim amekaribishwa chakula cha mchana pale ukumbi wa Karimjee.

Pia atapata fursa ya kuzungumza machache kutunuku siku hiyo muhimu kwa taifa letu.

Inshaalah!
 
💥🙏
 
Back
Top Bottom