Mada inahusika.
Tukiwa katikati ya mchakato wa kuelekea uchaguzi Mkuu, Tanzania iko katika mstari mwembamba sana wa kutunza historia yake ya utulivu, amani na umoja kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Baada ya uchaguzi wa 2015, yaliyotokea hapo katikati hadi 2020 kwa upande wa umoja wetu, ustawi wa kisiasa , demokrasia na haki basi ukilanganisha na miaka ya nyuma tulitetereka sana.
Watawala hawawezi kukwepa lawama za kushambuliwa watu, kupotezwa watu na wasiojulikana, kumimnywa uhuru wa habari na kujieleza na kumimnywa haki hasa kwa upinzani. Zile chaguzi za marudio na za Mitaa haziwezi kusahaulika kwenye historia.
Pengine ni majaaliwa tu, lakini kutegemea amani katika mazingira yale ilikuwa ni " ku-risk" Tanzania na watanzania na kama kuna somo la kujifunza basi watawala na vyombo vyetu vya Dola ilibidi wajifunze na waseme basi imetosha.
Tumeona na huu mchakato wa kupata wagombea ulivyokwenda na hadi sasa kuna wabunge na Madiwani wa CCM eti wamepita bila kupingwa laKINI BILA KIFICHO WALIPATIKANA KWA HILA . UMINYAJI HAKI NA UONEVU ULIOKUBUHU.
NEC haikwepi lawama hadi sasa, Propaganda huwa hazidumu NA SIO "GUARANTEE" kusaidia Tanzania kuwa na AMANI YA KUDUMU KILA SIKU.
NEC imecheza mdundo wa CCM na watawala kwa kukubali kuhenyeshwa wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi kuingia katika mtego. Likiharibika basi NEC hawawezi kukwepa lawama.
MAMBO MAWILI YA KUZINGATIWA KWA SASA
Tanzania inaninginia baina ya muda wa RUFAA ZA MAPINGAMIZI YA OVYO na baina ya UPIGAJI KURA NA KUTENDA HAKI HAPO TARAHE 28 Oktoba, 2020.
Huo ndio muda ambao Busara za NEC na ueledi utaivusha Tanzania yetu.
Tunajuwa namna NEC inavyopata masindikizo ya kutokubali hoja za rufaa huko, tunajuwa namna wanavyopata "pressure" ya wadau wa demokrasia na tunajuwa namna wanavyokosa msimamo wa pamoja kutokana na kuchanganywa taaluma za sheria na wanasiasa huko NEC wenyewe.
NEC haipaswi "ku-risk" amani ya Tanzania kwa kutaka kuwafurahisha watawala waovu wasioitakia mema Tanzania kwa kisingizio cha Madaraka yao.
Mtihani wa kwanza kwa sasa ni RUFAA ZA MAPINGAMIZI baada ya NEC kukubali kucheza mdundo wa CCM
Mtihani wa Pili ni haki na Uchaguzi siku ya tarehe 28 Oktoba ikiwa NEC itafanikiwa kuruka kiunzi cha kwanza cha rufaa kama nilivyoeleza
NEC inapaswa kujuwa ukubwa wa dhamana waliyopewa kwamba inavuka mipaka ya Tanzania yetu. Dunia inawatazama kwa karibu na kila tukio na hatua zinarikodiwa vyema.
Mazoea ya NEC kuwadekeza CCM hasa hii miaka mitano 2015 - 2020 ya CCM kufanya watakavyo kwa kuwatumia wakurugenzi makada na watiifu kwa CCM haiwezi ikawa kinga kwao. Mwenyekiti na Mkurungenzi wake Mkuu watabeba lawama zote.
USHAURI KWA NEC
Simamieni HAKI na SHERIA bila upendeleo na msiwe sehemu ya hila dhidi ya wengine.
Kwa mifano yenu ya kuwaenguwa UPINZANI tu kote BARA NA ZANZIBAR tayari mmeshafanya KOSA la awali na endelevu ambalo kujisafisha kwenu kutakuwa kugumu na kuanzia hapo mna wakati mgumu kujisafisha hilo eleweni.
NEC mnao muda wa kurekebisha mkitaka, hizo pressure za CCM zisiwatishe kumbukeni maisha baada ya uchaguzi.
Kumbukeni "timing" ya wapinzani si ya kubahatisha waliwasoma wakawaelewa watawala , NEC, vyombo vya haki, vyombo vya Dola na taasisi za kidini zinazotumika na KWA KWELI WALIWAELEWA VILIVYO. Mstirajie WAPINZANI watapotenza hii fursa nakuambieni.
MWISHO
Tunachukuwa hii fursa kutimiza wajibu wetu kama raia wa nchi hii kuwaomba NEC kusimamia haki na usawa walau kwa hii fursa ndogo ya kuitunza amani ya Tanzania iliyobaki.
Yaliyofanyika ndani ya miaka hii mitano hayapaswi kujirejea kwenye uchaguzi huu ambao ndio fursa ya mwisho kwa wapinzani, wanamageuzi , wapenda haki na wanademokrasia kote ZANZIBAR na BARA na dalili zote zinaonesha hatari iliyoko mbele.
Shime NEC tendeni haki na msimamie haki kwa dhati.
Kishada.