NEC lihurumieni taifa hili tusijenge historia mbaya

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
NEC hihirumieni taifa hili lisijenge historia mbaya.

Ninasema hili nikiwa namaanisha kwamba mazingira tuliyonayo NEC kama chombo huru kisichoegemea popote kwa mujibu wa sheria ikifikia mahali kikajisahau kikaingizwa mkenge na CCM kwakuwa tu Chama hiki kina serikali inayo Dola na kitawalinda kitawadanganya.

CCM ni chama tu kikishindwa kitaondoka na NEC watabakia kuendelea na majukumu yake. Hawa wanasiasa wasiwadanganye kwa tamaa zao mkaliingiza taifa matatizoni. Hawa wanasiasa wanapita kesho hawapo NEC simameni katika haki, mnaweza kukibeba Chama tawala na kisibebeke mwisho wa siku Zigo litaangukia kwengu.

Nimekuwa nikiliza kauli za baadhi ya viongozi wa CCM wakijiapiza kwamba iwe isiwe lazima washinde kwa hali yeyote ile. Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Wilaya moja mkoani Singida anayewatishia Wagombea kuwa wapende wasipende wapinzani hata wakishinda hawatatangazwa na haya huwa anayesema hadharani kabisa, anajiapiza kanisa kwa kusema lasivyo hao wapinzani wataokotwa mahospitalini.

Najiuliza kama kweli wapinzani watashinda na wao wakasema lazima watangazwe hali itakuwaje?

Inaeleweka kabisa kuwa CCM wanawategemea kwa kiasi kikubwa wasimamizi wa uchaguzi ambao nao wanahisiwa kuwa nao ni makada. Kama kweli hawa wasimamizi nao watafanya hivyo basi NEC mjiandae kubeba lawama hizi. Mtakua wa kwanza kulijengea taifa letu historia mbaya.
 
Back
Top Bottom