NEC lazima mjue Wasabato wana haki ya kupiga na kupigiwa kura

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Katika nchi inayozingatia haki za raia wake, Mamlaka na taasisi mbalimbali huzingatia haki za raia wake bila kujali kama ni wengi ama ni wachache katika kufikia maamuzi mbalimbali,na ndio maana katika nchi nyingi duniani chaguzi hufanyika katikati ya wiki ili uchaguzi usiingiliane na siku tatu kuu za kuabudu yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Hivi wakati Tume ya uchaguzi taifa inapanga tarehe ya uchaguzi katika majimbo matatu ya Longido, Singida kaskazini na haikujua kuwa siku waliyopanga ilikuwa ni Jumamosi (sabato)?

Je kwa kitendo hicho NEC hawakujua Kuwa kinawanyima haki yao ya msingi waumini wote wa kanisa la waadventista Wasabato kupiga kura?

Kwa mujibu wa imani ya kanisa la Wasabato siku ya Jumamosi ni siku maalum kwa kuabudu tu na si vinginevyo.

Naamini pia idadi ndogo ya wapiga kura imechangiwa pia na kitendo hicho ingawa hakitajwi.

Kwa nini NEC imeamua kuhamisha siku bila kwanza kuelimisha umma?
Tafadhali sana naomba NEC iheshimu haki za raia hata kama ni wachache.

NEC Wajifunze kutokana na hili lisije likajirudia ni aibu kwa serikali,

iCHURCH Magazine

WASABATO WAISHINDA SERIKALI MAHAKAMANI.

Monday, 15 January 2018

Kanisa la Waadventista Wasabato leo limeishinda serikali katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwalimu Ezekiah Oluoch dhidi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Mazingira na Muunguno, January Makamba pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika shauri hilo Mwalimu Ezekiah alikuwa akipinga muongozo wa Waziri huyo unaotaka kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku maalumu ya kufanya usafi kitaifa. Mwalimu huyo alidai kwamba agizo hilo la serikali linaingilia haki na uhuru wa kuabudu kwa Wakristo wa madhehebu ya Waadventista Wasabato, ambao kwa imani yao siku ya jumamosi hawatakiwi kufanya kazi.

Mwalimu Oluoch aliiomba mahakama, pamoja na mambo mengine, itamke kwamba agizo hilo la kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi linaingia uhuru wa kuabudu kwa waadventista wasabato.

Kwa sababu shauri hilo lilikuwa ni la kikatiba lilisikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika masijala kuu ya mahakama hiyo (Main Registry) kwa mujibu wa sheria.

Mahakama Kuu imempa ushindi mleta maombi (mwalimu Ezekiah Oluoch) kwa kutamka kwamba agizo hilo la wizara limeingilia uhuru wa kuabudu wa mleta maombi pamoja washiriki wenzake wa imani hiyo.

Mahakama pia imeeleza kwamba agizo la wanachi kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho ya mwezi, halitatumika kwa mleta maombi pamoja na wenzake wa imani hiyo kwa kuwa kumlazimisha kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wake wa kuabudu kama unavyolindwa na katiba. Kwa maana hiyo kuanzia leo waumini wa madhehebu ya waadventista wasabato hawatashiriki kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi kama inavyotakiwa.
 
Katika nchi inayozingatia haki za raia wake, Mamlaka na taasisi mbalimbali huzingatia haki za raia wake bila kujali kama ni wengi ama ni wachache katika kufikia maamuzi mbalimbali,na ndio maana katika nchi nyingi duniani chaguzi hufanyika katikati ya wiki ili uchaguzi usiingiliane na siku tatu kuu za kuabudu yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Hivi wakati Tume ya uchaguzi taifa inapanga tarehe ya uchaguzi katika majimbo matatu ya Longido, Singida kaskazini na haikujua kuwa siku waliyopanga ilikuwa ni Jumamosi (sabato)?
Je kwa kitendo hicho NEC hawakujua Kuwa kinawanyima haki yao ya msingi waumini wote wa kanisa la waadventista Wasabato kupiga kura?
Kwa mujibu wa imani ya kanisa la Wasabato siku ya Jumamosi ni siku maalum kwa kuabudu tu na si vinginevyo.
Naamini pia idadi ndogo ya wapiga kura imechangiwa pia na kitendo hicho ingawa hakitajwi.
Kwa nini NEC imeamua kuhamisha siku bila kwanza kuelimisha umma?
Tafadhali sana naomba NEC iheshimu haki za raia hata kama ni wachache.
Mbona chaguzi nyingi huwa zinafanyika jumapili lakini sijawahi kusikia wakatoliki wakilalamika, nyie wasabato mna yenu sio bure
 
Katika nchi inayozingatia haki za raia wake, Mamlaka na taasisi mbalimbali huzingatia haki za raia wake bila kujali kama ni wengi ama ni wachache katika kufikia maamuzi mbalimbali,na ndio maana katika nchi nyingi duniani chaguzi hufanyika katikati ya wiki ili uchaguzi usiingiliane na siku tatu kuu za kuabudu yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Hivi wakati Tume ya uchaguzi taifa inapanga tarehe ya uchaguzi katika majimbo matatu ya Longido, Singida kaskazini na haikujua kuwa siku waliyopanga ilikuwa ni Jumamosi (sabato)?
Je kwa kitendo hicho NEC hawakujua Kuwa kinawanyima haki yao ya msingi waumini wote wa kanisa la waadventista Wasabato kupiga kura?
Kwa mujibu wa imani ya kanisa la Wasabato siku ya Jumamosi ni siku maalum kwa kuabudu tu na si vinginevyo.
Naamini pia idadi ndogo ya wapiga kura imechangiwa pia na kitendo hicho ingawa hakitajwi.
Kwa nini NEC imeamua kuhamisha siku bila kwanza kuelimisha umma?
Tafadhali sana naomba NEC iheshimu haki za raia hata kama ni wachache.
KWANI TZ . KUNA UCHAGUZI TENA ZAIDI YA KUZUGA NA KUPOTEZA MUDA NA RASILIMALI TU ILA MSHINDI NI LAZIMA ATOKEE CCM HAINA HAJA ENDELEENI NA MFUMO MLIYOUAMUA NA MISITUPOTEZEE MUDA HADI MTAKAPO JIREKEBISHA KUPATIKANA KWA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA VINGENEVYO NO NO.
 
Katika nchi inayozingatia haki za raia wake, Mamlaka na taasisi mbalimbali huzingatia haki za raia wake bila kujali kama ni wengi ama ni wachache katika kufikia maamuzi mbalimbali,na ndio maana katika nchi nyingi duniani chaguzi hufanyika katikati ya wiki ili uchaguzi usiingiliane na siku tatu kuu za kuabudu yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Hivi wakati Tume ya uchaguzi taifa inapanga tarehe ya uchaguzi katika majimbo matatu ya Longido, Singida kaskazini na haikujua kuwa siku waliyopanga ilikuwa ni Jumamosi (sabato)?

Je kwa kitendo hicho NEC hawakujua Kuwa kinawanyima haki yao ya msingi waumini wote wa kanisa la waadventista Wasabato kupiga kura?

Kwa mujibu wa imani ya kanisa la Wasabato siku ya Jumamosi ni siku maalum kwa kuabudu tu na si vinginevyo.

Naamini pia idadi ndogo ya wapiga kura imechangiwa pia na kitendo hicho ingawa hakitajwi.

Kwa nini NEC imeamua kuhamisha siku bila kwanza kuelimisha umma?
Tafadhali sana naomba NEC iheshimu haki za raia hata kama ni wachache.
Unapiga kura siku nzima?
 
Mkuu ukiendekeza udini kwenye siku hufiki mbali jumapili ni siku ya wakristo jumamosi wasabato ijumaa waislamu Alhamisi ni siku ya wakorino,jumatano dini ya ngemela wanayosali ,jumanne ni siku.ya wadini ya Sloamu,Jumatatu siku ya wa sokh .kila kundi likipiga yowe hakuna siku itakuwa bure na hatuji piga kura milele
 
Back
Top Bottom