NEC kushurutisha wapiga kura kurudi majumbani badala ya kusubiri matokeo vituoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC kushurutisha wapiga kura kurudi majumbani badala ya kusubiri matokeo vituoni!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Yaelekea CCM na NEC wamegundua mbinu mpya za medani za kuchakachua kura kiulaini kwani NEC wataiagiza polisi kufukuza watu watakaokuwa wanataka kubaki vituoni ili kulinda kura kwa madai ya kuwa hiyo siyo kazi yao.

  NEC yadai kubaki vituoni kunaweza kusababisha fujo lakini hawana tatizo na mashushu kuwepo vituoni. Hii ni changamoto mpya kwani Kenya mbona wapiga kura hubaki vituoni ili kutenda haki?

  NEC ina maelezo gani juu ya watumishi wa Idara ya usalama wa taifa ambao sasa hivi wanatawanya kona za Nchi ili kuchakachua kura zetu aisee.

  Hapa nina wasiwasi ya kuwa tone la damu laweza kudondoka.

  Chadema yapaswa kuwasiliana na NEC haraka iwezekanavyo ili kuweka utaratibu wa uwazi wa wapiga kura kushuhudia uhesabuji wa hata kwa kuwa nje ya kituo chao cha kupiga kura ili kumulika mashushu wabebao mikoba myeusi iliyorundikana mapesa.

  Bila ya kufanikisha hilo basi CCM atatumaliza kabisa.

  Kama mbinu hizi Chadema hazitazitafutia muarobaini mapema basi kilio na kusaga meno cha wasubiri
   
 2. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwani si kuna kua na mawakala wa kila chama katika kila kituo!!?
  Mnaanza kutafuta sababu ya kulalamika sasa!
  Kituoni ubaki kufanya nini? ebo!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Uchaguzi huru na haki ni kwa mpiga kura kuruhusiwa kukaa mita 100 toka eneo la kitu cha kupigia haya yanayosemwa ni kinyume.Natamani NEC watamke mapema ili sauti zetu zisikike hadi kwa hao wanatupatia ufadhiri wa fedha za uchaguzi japo siwapendi pia
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapiga kura watalazimika kubaki vituoni kwa sababu ya hila zilizozoeleka za CCM za kuchezea kura zetu. Hakuna mpiga kura (asiye mwana CCM) mwenye imani na chama hiki cha majambazi. NEC lazima waonywe mapema wasije wakasababisha matatizo kama ya Kenya.
   
 5. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pumbafu!!!! unakwenda nyumbani kufanya nini haki yako iko sehemu ya kupigia kura
  subiri kura zisichakachuliwe ebo!
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huyu mwenzetu anataka kulinda kura zake, ni kama vile hawaamini MAWAKALA wa chama chake, sasa kama ni kulinda kura ndani ya mita 100 huwezi kuiona hata ballot box utalinda nini!
  anachoongelea hapa anataka kulinda kura zake, hivyo basi,,,hizo mita 100 sidhani kama ataridhika..
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sio kweli uchaguzi huru na haki ni kuwa na tume ya uchaguzi iliyo huru kabisa. Hii tume sio huru, Makame anatakiwa kustaafu, Kiravu anatakiwa kustaafu wanafanya nini mpaka saa hizi wamesahau nini????? Kama wenzao wamestaafu na hawa wanafanya kazi on borrowed time kitu gani kitawazuia hawa wakuu wa tume kumpendelea bosi wao aliyewapa extension ya mikataba yao?????

  Suala la mita 100 umelitoa wapi wewe???? Hebu tuambie
   
 8. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  kaka umenivunja mbavu he he he
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Ulinzi wa kura unahitaji wapiga kura wawepo hata mita 100 ili kuwamulika mashushu ambao watataka kuingia ndani ya chumba cha kuhesabia kura ili kuwarubuni mawakala. Kisheria ya uchaguzi mashushu hawapaswi kuruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura na wapigakura ndiyo wakuhakikisha hilo. Hali hii ni mbaya sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  Kenya wapigakura huruhusiwa kuwa nje ya vituo ili kuhakikisha watu wasiohusika na chaguzi hawaingii ndani ya chumba bila ya hilo tumekwishaaaaaaaaaaaaaaa
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  watu wa vyama vyote waliopiga wakibakia kwenye vituo, sasa hamuoni hapo huweza kukatokea uvunjifu wa amani?

  hili nalo linahitaji elimu ya chuo kikuu kuligundua?

  nyny kila lifanywalo na serikali na vyombo vyake basi mpinge tu


  nani kakwambieni maana ya upinzani kupinga lifanywalo na serikali?

  kuna mawakala wa vyama, observer wa nje na wandani na wengineo kama kuna dhuluma si itasemwa au wote hamuwaamini?

  ati Kenya huu upumbavu kufananisha hali za Tanzania na Kenya,


  nani kakwa
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,201
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  siku hiyo sitoki kituo cha kupigia kura

  wanataka kuiba sio!!!!
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  omba chama kikuweke uwe wakala wake utakuwa ktk hali ya usalama

  la unataka kuijaribu serikali kuwa kwenye kikao kwa kupinga agizo halali uone vp serikali inafanya
   
 13. N

  Njaare JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naomba mtaalamu wa sheria ya uchaguzi atujuze juu ya hili. Kama sheria inasema kuwa ukipiga kura urudi nyumbani basi itakuwa iliwekwa maalumu ili kuruhusu wizi wa kura. Kama haimzuii mtu kubaki eneo la kituo basi namba wanasheria au wanaojua mtujulishe ili tubaki vituoni.

  Pamoja na kuwa na mawakala, lakini mawakala wengine wanakuwa ni mapandikizi au wazembe. Kwa mfano mwaka 2005, kuna wakala mmoja wa chama kimoja cha upinzani alionekana anatumwa chips na wakala wa chama kingine. Kama wapigakura watakuwepo eneo la kituo wakala kama huyu hata kama ni pandikizi hatathubutu kutoka au kufanya uzembe.

  Shime wapiga kura. Tulinde kura zetu. Kushinda njaa siku moja na kuja kushiba miaka mitano inayofuata si vibaya. Kuipa CCM kuongoza nchi kwa uvivu na woga wa kulinda kura zetu ni kuchagua miaka mitano ya ufisadi, mfumuko wa bei, dharau (ulinichagua kwa kiherehere chako), nk
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  This is the last bullet to win elections CCM has, get people out of groups so that it will be east to lock them in their houses for two to three days once things go worse.

  Watu wanapokuwa vituoni ni hatari kwa CCM na wanausalama kwani mob psychology hutawala. Kama kweli CCM na NEC wanathibitishia watanzania na dunia kuwa uchaguzi huu utakuwa huru na haki basi hawana la kuogopa kutokana na wananchi kukaa mita chache toka kituoni baada ya kupiga kura. Mbona watu maelfu kwa maelfu watimu shabiki huingia mpirani at the end referee anapopuliza kipenga cha mwisho kunakuwa hakuna fujo kwani shabiki wa timu iliyofungwa wanakuwa wameshuhudia haki ikitendeka uwanja wakati wa mchezo wote na pindi referee akienda kinyume uwanja unawaka moto.

  CCM na NEC wasiwe na woga wanachotakiwa kufanya kwa NEC kama referee ni kuchezesha fair game na CCM kama timu icheze bila kuwa na mentality ya referee yupo upande wao. Hili likifanyika uchaguzi utaisha salama, Dr Slaa atatangazwa mshindi kwa amani na utulivu, wabunge wa upinzani watakuwa about 50% na maisha yatakuwa bora kwa wote wana CCM na watanzania wote.

  Ila kama wanataka ushindi wa mezani kwa kuingiza timu uwanjani, watarajie kuwa opponent team itaingia kucheza na ina mashabiki wake ambao watataka kuona referee amecheza fair na matokeo ya uwanjani yawe ndiyo ya mwisho. Kama wanataka ushindi wa mezani wafute mchezo (Kuwe hakuna uchaguzi).
   
 15. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaitwa uchakajuaji huru! Yaani kura yako haina impact...mimi tukutane mkesha wa 31October!
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  kwani hujui kuwa ccm, kazi yenu ni kuhonga mawakala, na kubadili kura zilizopigwa na kuweka zingine ili kujipatia ushindi.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  yaani hapo ndio penye wizi wa kura wenyewe. Bila ya wananchi kuwa jirani kulinda kura zao hamna kitu
  .
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mada zingine hazina kichwa wala miguu! Wapi imeandikwa ukipiga kura ubaki kituoni? Nini kazi ya mawakala wa vyama ? Wacheni uchuro wenu! Na mwingine amedesa uandikishaji wa daftari la kudumu kule Pemba, ambapo waliokuwa wakiandikishwa walitakiwa kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha kujiandikisha!

  Na bado hata mkikesha vituoni siku tano kabla ya siku ya kupiga kura, CCM itaibuka na ushindi tu!
   
 19. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi ukae na helmet ama tayarisha maji ya moto yaliyochemshwa na chumvi kukanda maamuvi ya virungu utakavyokula. Siku hiyo mke/mume wako ndiyo atakuwa daktari wako na nesi wako. :becky: :becky: :becky:
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hapana ni mita 200
   
Loading...