Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,496
- 9,278
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuna majimbo manne ambayo uchaguzi wa madiwani haujafanyika.
Majimbo matatu Wagombea wamefariki na jimbo moja la Kibosho Kati karatasi za kura zimekosewa hivyo tume itapanga tarehe husika ya uchaguzi.
Akizungumzia hali ya uchaguzi mapema jioni hii, Jaji Kaijage amesema tume hiyo haijapokea taarifa za uwepo wa kura feki katika majimbo ya Kawe, Pangani na Kigoma.
Amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika muda huu mchache uliobaki.
Aidha, aliwataka wapiga kura kufanikisha upigaji kura wa amani na kuwataka wananchi ambao hawakujitokeza kupiga kufanya hivyo zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya zoezi la kupiga kura kumalizika.