NEC: Kama CHADEMA hawakumuandikia Spika barua hakukuwa na tatizo

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,663
Wakuu nipo naangalia taarifa ya habari hapa Azam UTV, mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Emanuel Kavishe anasema kuwa ishu ya mbunge wa Ndanda, CHADEMA walikosea steps.

Anasema walipomfukuza Cecil Mwambe walipaswa kumuandikia barua hapo hapo Spika wa bunge ili yeye awataarifu wao lakini pia akaonya kuwa kama mbunge anafukuzwa ubunge ikiwa imebakia mwaka ambapo muda wa uchaguzi mdogo kwa mujibu wa sheria inategemea busara za Spika.

"Ukimfukuza mbunge wakati unajua kuwa muda wa uchaguzi mdogo umeisha inamaana wananchi watakaa bila mwakilishi na hivyo unawanyima haki ya wawakilishi hivyo ingetegemea busara za Spika"

Bwana Kavishe pia amezungumzia kuanza kwa kuhakiki kwa daftari la wapiga kura.

My take: Naona ishu ya Mwambe, CHADEMA wameshapigwa knockout.

USSR
 
Mwambe hakufukuzwa mbona, alitamka kuwa ajiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama ikiwemo ubunge na kujiunga na CCM na kupokelewa na CCM, Ni Kama akina Waitara, Mollel, n.k walivyofanya, kwani Hawa Chadema iliandika barua kwa Nec au kwa Spika?

Utashangaa Mahakama Kuu nayo ikatoa uamuzi Kama huu. Hii nchi kila taasisi ya Serikali ipo corrupted, kuanzia Executive na branches zake, Bunge, Mahakama.

Kwa hapa tunahitaji mapinduzi na sio uchaguzi kubadili huu upumbavu na kuweka taasisi imara.
 
Ndio chadema walipaswa kuandika barua kwa spika
Hivi Mwambe alifukuzwa au aliachia ngazi mwenyewe? Hiyo sheria anayo iongelea huyo Kavishe iko kifungu gani?
Hivi siku hizi jambo lililoko mahakamani hujadiliwa mubashara? CCM mko vizuri
 
Mpumbavu akiamua kuhalalisha kinyesi kuwa keki anaweza kukuambia ulijuaje ni kinyesi nawe hujapeleka kwa mkemia?
Nchi hii watu wajinga wamepewa madaraka na kwa ujinga wao wanataka kuamini wengine wote ni wajinga ili kumfurahisha mteuzi.
Kama tafsiri ya mahakama zetu nayo itakuwa hivyo basi tuhesabu kuwa TUMEKWISHA KAMA TAIFA
 
Hivi Mwambe alifukuzwa au aliachia ngazi mwenyewe??
Hiyo sheria anayo iongelea huyo Kavishe iko kifungu gani?
Hivi siku hizi jambo lililoko mahakamani hujadiliwa mubashara??
Ccm mko vizuri
Usiangalie sheria moja tu, angalia pia sheria ya usalama kazini. Serikali inafanya kazi kwa uthibitisho wa mawasiliano rasmi ya barua ama ya muajiriwa au muajiri. Hapa wote wawili hakuna aliyempa taarifa spika ( The Boss) Mbaya zaidi hata msajili wa vyama hajaandikiwa ili kutaarifu spika atangaze jimbo li wazi.
 
Usalama kazini sheria ya (OSHA ) na uchaguzi wapi na wapi?
Usiangalie sheria moja tu, angalia pia sheria ya usalama kazini. Serikali inafanya kazi kwa uthibitisho wa mawasiliano rasmi ya barua ama ya muajiriwa au muajiri. Hapa wote wawili hakuna aliyempa taarifa spika ( The Boss) Mbaya zaidi hata msajili wa vyama hajaandikiwa ili kutaarifu spika atangaze jimbo li wazi.
 
Wakuu nipo naangalia taharifa ya habari hapa Azam UTV, mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Emanuel Kavishe anasema kuwa ishu ya mbunge wa Ndanda Chadema walikosea steps.

Anasema walipo mfukuza Cecil Mwambe walipaswa kumuandikia barua hapohapo spika wa bunge ili yeye awataarifu wao lakini pia akaonya kuwa kama mbunge anafukuzwa ubunge ikiwa imebakia mwaka ambapo muda wa uchaguzi mdogo kwa mujibu wa sharia inategemea busara za spika.

"Ukimfukuza mbunge wakati unajua kuwa muda wa uchaguzi mdogo umeisha inamaana wananchi watakaa bila mwakilishi na hivyo unawanyima haki ya wawakilishi hivyo ingetegemea busara za spika"

Bwana kaviche pia amezungumzia kuanza kwa kuhakiki kwa daftari la wapiga kura.

My take: Naona ishu ya Mwambe Chadema wameshapigwa knockout.

USSR
Kwani Cecil Mwambe alifukuzwa?
 
Back
Top Bottom