Uchaguzi 2020 NEC itupe ufafanuzi wa kisheria juu ya masuala haya yafuatayo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Ukisoma sheria za uchaguzi mkuu ya mwaka 2015 na mabadiliko yake yote na sheria ya matumizi kwenye uchaguzi kuna mambo yafuatayo:

1. NEC imepewa mamlaka ya kisheria kutangaza Tarehe ya Uchaguzi lakini Sheria haikuipa NEC mamlaka ya kutangaza tarehe rasmi ya kuanza kampeni! Je, mamlaka ya kutangaza tarehe rasmi ya wanasiasa kuanza kampeni NEC imeyatoa wapi?

2. Pili Sheria inataka NEC itoe kwenye Gazzette majina ya wateuliwa kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi miezi isiyopungua miwili na isiyozidi mitatu baada ya kuwa nominated, Kwa nini NEC mpaka hivi sasa haijatimiza sharti hili, maana imebaki miezi miwili tufanye uchaguzi lakini NEC mpaka sasa hivi haijapitisha majina ya wagombea wa uraisi au ubunge!

3. Sheria waziwazi imempa msajili wa vyama vya siasa uwezo wa kumuwekea pingamizi mgombea yeyote huko NEC kutokana na kuvunja sheria ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi na makosa mengine ya uchaguzi,Je ni mtu gani tena mwingine tena kwa mujibu wa sheria za uchaguzi tulizo nazo anaweza kumuwekea pingamizi mgombea na kwa vifungu vipi?

Naambatanisha hapa sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 na sheria ya makosa ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi.
 

Attachments

  • 1506507832-The National Election Act (CAP 343) Revised 2015) (1).pdf
    5.3 MB · Views: 15
  • 1598123216-Sheria ya Gharama za Uchaguzi Rev 2015.pdf
    8.1 MB · Views: 10
Dunia inashangaza utashangaa mpaka umauti Madogo wakulungu watume nyuti Hatukurupuki kunyesha tunanyesha baba Hatiuchuruzuki tumechill tuko full hatufurukuti.
 
Unaiuliza NEC hii iliyokua inasubiri rais apumzike kidogo halafu amalize mchakato ya kuchuja watu ndani ya chama chake halafu akishamaliza ndiyo NEC na yenyewe ianze michakato yake?
 
Ukweli ni kwamba hatuna Tume ya Uchaguzi, tunayo tume ya Mwenyekiti wa CCM inayoongozwa na kauli ya Rais ambaye habanwi na Katiba wala sheria, kauli yake ndiyo sheria kuu.
 
Back
Top Bottom