NEC Itoe Mwongozo Kwa Wale Majina yao Hayajaonekana Katka Vituo Vyao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC Itoe Mwongozo Kwa Wale Majina yao Hayajaonekana Katka Vituo Vyao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Oct 26, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wana Jamvi

  Zimebaki siku chache watanzania wenye Umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kulijongelea Sanduku la Kupiga kura ili Wafanye Maamuzi yatakaamua Hatma ya Maisha yao kwa kipindi kingine cha miaka 5 yaani kutoka 2010 mpaka 2015.

  Siku zinapokaribia joto la Uchaguzi linapanda si tu kwa Wagombea wa nafasi mbali mbali bali hata kwa Wapiga kura ambao wengi mwaka huu wameonesha hamasa kubwa sana ya Kushiriki huu uchaguzi

  Wiki kama moja iliyopita Tume ya Uchaguzi iliwataka Wananchi wote wakahakikishe majina yao katika vituo walivyojiandiskisaha kupigia Kura.

  Tayari kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wananchi kwamba hawajaona majina yao katika vituo walivyojiandikisha kupiga kura na hisia zimeanza kutawala na kulihisisha tukio hili na Kitendo kilichokuwa kikifanywa na Chama kimojawapo cha kuorodhesha namba za Shahada za kupigia kura


  Sipendi kuchukua nafasi hii kumtafuta Mchawi, bali ningependa Kiravu, Makame na NEC kwa Ujumla watoe Muongozo ya nini kinapaswa kufanywa pale mtu anapokwenda kwenye kituo na kukuta Jina lake halipo kwenye Orodha iliyochapishwa

  NEC Isipofanya hivyo itatufanya hata sisi wengine Kuamini kwamba NEC walipelekewa majina (nazungumzia yale yaliyokuwa yanaorodheshwa na Chama fulani) ili wayaondoe katika Orodha na kuwanyima wale waliodhaniwa ni Wapinzani wa Serikali Fursa ya Kupiga Kura

  Naomba NEC wafanye yafuatayo

  1: Kiravu na makame tunaomba mtueleze sisi ambao majina yetu hayachapishwa katika vituo tulipojiandikisha kupiga kura nini Tufanyeje

  2: NEC ituambie ni kwa nini mtu amebadilisha kituo cha kupiga Kura lakini jina lake halikufutwa katika kituo cha mwanzo? Na huyu mtu ana kadi mbili kwa maana alipofanya marekebisho hamkuichukua ile ya kwanza na hamkumfuta katika kituo chake cha mwanzo, Je hili limefanywa Makusudi ili mtu huyu akipiga Kura Asubuhi TEMEKE aweze kuwahi kwenda kupiga kura kwenye kituo chake cha zamani cha Ubungo?


  Asanteni sana
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Niliyoyazungumza naona sasa ndio yanatokea, Naomba NEC itoe tamko ili watu waliojiandikisha lakini majina yao hayapo waweze kupiga kura
   
 3. p

  petermakatu Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 18
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 5
  Kwa wale ambao majina yao hayapo kwenye orodha iliyobandikwa nje ya kituo na nakala iliyoko mikononi mwa DIRECTION CLERK aliyepo nje, wasihofu kwani kuna orodha iko ndani yenye majina na picha ambayo ndiko uhakiki wa majina na picha unakofanyikia. Waombe majina yao yaangaliwe huko. Orodha hii inayo majina yote. Baadhi yetu wameitumia na wasimamizi wasaidizi wamewasaidia kuangalia na kuwaruhusu kupiga kura.
   
Loading...