NEC inataka vyama vipeleke wataalam wa IT kujiridhisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC inataka vyama vipeleke wataalam wa IT kujiridhisha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Speaker, Oct 15, 2010.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  "TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IMEVITAKA VYAMA VYA SIASA KUTOA WATAALAM WAO WA WA KOMPYUTA KUJIRIDHISHA NA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUJUMLISHA MATOKEO"

  Nimeziona tetesi hizo facebook,kama ni kweli jamani humu JF kuna wataalam kubao okoeni jahazi kusiwe na lawama baadae
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kama nec ina nia kweli ya kuweka mambo kuwa wazi wajibu kwanza madai ya chadema kupitia kwa profesa baregu alipohoji idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura kuwa milioni 19.6
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika facebook? Kwa nini wasiwe wawazi kutangaza hilo -- kwenye mkutano na waandishi wa habari??
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Taarifa toka facebook itakuwaje credible?
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Facebook?

  BTW: Wataalamu wa IT wanaweza kuridhika na mfumo wa Kompyuta (practically this is simple). Je ni wataalamu gani watakahakiki idadi ya wapiga kura?
   
 6. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kama kweli wana nia ya dhati, waanze kushirikisha wataalamu hao wa vyama kwenye kuhakiki daftari la wapiga kura, idadi ya vituo vya kupigia kura, mfumo wa uhesabuji vituoni, Utangazaji wa matokeo vituoni, upelekaji wa matokeo NEC na ujumlishaji wake.
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli,Basi jambo hili ni jema!na linaweza kupunguza msuguano!
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  NEC:VYAMA VYA SIASA LETENI WATAALAM WENU WA TEKNOLOJIA YA KOMPYUTA WAJIRIDHISHE NA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUJUMLISHA MATOKEO


  Na Joseph Ishengoma

  Wa Tume ya taifa ya uchaguzi

  Oktoba 31,2001, Watanzania

  *wenye sifa za kupiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

  * watakao waongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

  Siku hiyo ni siku maalum na yapekee ambayo Mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18, nakujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na mwenye shahada ya kupiga kura atatumia haki yake Kikatiba kuwachagua viongozi atakaoshirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

  Kura anayotarajia kupiga Mtanzania mwenye sifa zilizotaja hapo juu, ndiyo nguvu pekee aliyonayo mwananchi ya kuamua hatma ya Taifa lake kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. Mtanzania mwenye sifa, aliyetumia muda wake kujiandikisha katika Daftari le Kudumu la Mpiga Kura na anayependa maendeleo ya nchi yake,hana budi kushiriki katika tukio hili muhimu.

  Jumla ya wapiga kura 20,136,588 ambapo wapiga kura 19,728,919 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 407,669 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wanatarajia kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Uchaguzi ni tukio muhimu sana katika jamii yoyote ile inayozingatia utawala bora. Uchaguzi utakaofanyika oktoba 31,2001, unatarajia kuhitimisha kipindi cha kampeini kilichoanza tangu tarehe 20 Agosti,2010.

  Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ilikutana na Viongozi wa Vyama Vya Siasa Jijini Dar Es Salaam na kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu. Pia katika mkutano huo Tume ilitaka kupata maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Vyama hivyo yenye lengo la kuboresha uchaguzu huo ili uwe huru na wa haki na kukidhi matarajio ya Watanzania.

  Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume yataifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji mstaafu Lewis makame aliwaambia viongozi hao kuwa sambamba na kunadi sera za vyama vyao, viongozi hao wanawajibika kwa wananchi wote wanaojitokeza kuhudhuria mikutano ya kampeini za uchaguzi katika k uhakikisha kunakuwepo na amani na utulivu wakati wote kama inavyoelekezwa katika maadili waliyotia saini.

  “Tume inaamini kwamba vyama vitaendelea kuheshimi na kufuata maadili hayo ili kipindi kilichobaki, kila chama kipate fursa nzuri ya kunadi sera zake katika mazingira ya utulivu na amani,” alisema.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, hali hiyo itasaidia kuwavuta wananchi wengi kuhudhuria mikutano ya vyama bila kuogopa na kusikiliza kwa makini sera za vyama husika.

  Hata hivyo Jaji Makame alitumia fursa hiyo kuwasii viongozi wa vyamavya siasa kuhakikisha wanawadhibiti washabiki na wafuasi wao ili wasifanye fujo katika mikutano ya kampeini. Taadhari hiyo inatokana na taarifa kuwa kuna baadhi ya wafuasi wa vyama, wamekuwa chanzo cha fujo na vitendo vya uvunjifu wa amani.

  Alisema, “Viongozi wote wa vyama vya siasa watumie muda uliobaki kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu na kujiandaa kwa ajili ya siku ya kupiga kura.”

  Akiwasilisha mada ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Katibu wa Tume Bwana Rajabu Kiravu, alieleza hatua mbalimbali za maandalizi zilizokwisha fanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hatua hizo ni pamoja na shughuli za kuandaa na kusafirisha vifaa, uchapishaji wa karatasi za kura uliofanywa na Kampuni ya Kalamazoo Secure Solutions ya Uingereza na maandalizi ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  Mengine ni uteuzi wa wagombea, kampeini za uchaguzi, ushirikishwaji wa wadau wa uchaguzi, maandalizi ya siku ya kupiga kura, watendaji wa vituo vya kupiga kura, ulinzi wa vituo vya kupiga kura, mawakala wa upigaji kura, mabadiliko ya muundo wa karatasi za kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo pamoja na mchango wa washiriki wa maendeleo na asasi zisizo za kiserikali.

  Pia Bwana Kiravu alitumia fursa hiyo kujibu hoja mbalimbali zilizoulizwa na viongozi hao wa vyama vya siasa ikiwemo ile ya mkakati wa kutumia teknolojia ya kompyuta kuiba kura.

  Alisema mfumo (system) utakaotumika kupokea matokeo ya awali kutoka majimboni unaojulikana kwa kitaalam kama

  Result Management System (RMS) umebuniwa na wataalam wa Tume na ndio wanaouratibu. Kwa mujibu wa Bwana Kiravu, lengo la kuwa na mfumo huo ni kuharakisha zoezi la kujumlisha matokeo kutoka maeneo mbalimbali ilii wananchi wapate matokeo haraka, sio kuhujumu matokeo.

  “Kama vyama vina mashaka na mfumo huu, basi vilete wataalam wake wa kompyuta wakae na wataalam wa Tume na kujiridhisha jinsi unavyofanya kazi ili wasiwe na mashaka nao, “ alisema. Alifafanua kuwa katika dunia ya leo inayoongozwa na teknolojia, Tanzania haiwezi kuepuka matumizi ya teknolojia, ila kinachotakiwa ni vyama vyenyewe kujipanga na kuiarifu tume lini watakuja kujiridhisha na mfumo hu.

  Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu utendaji kazi wa mfumo huo, Mkuu wa Idara ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dr. Sisti Cariah alisema, “Tume itatoa kompyuta mbili kwa kila Halmashauri zitakazotumika kujumlisha na kuleta matokeo makao makuu ya Tume. Kompyuta hizo zitakuwa na namba maalum, hivyo haitakuwa raisi kompyuta nyingine tofauti na hizo kutuma matokeo ya uchaguzi makao makuu ya tume ya Uchaguzi.”

  Aidha kila wilaya itateua na kutuma wataalam wawili wa kompyuta makao makuu ya tume Dar Es Salaam kuhudhuria mafunzo ya kutumia mfumo huo wa kupokea matokeo.

  Pamoja na kutumia mfumo huo, vyamavyote vya siasa vitapewa nakala ya matokeo katika vituo. “Hivyo vyama navyo vinaweza kujumlisha na kupata matokeo sahihi” alisema.

  Kuhusu wanavyuo kuruhusiwa kupiga kura, Bwana Kiravu alisema kuwa “Tume haina data base ya wanavyuo, ina data base ya wapiga kura. Daftari la Wapiga Kura halikuboreshwa wakati mmoja. Kuna mambo ambayo huwezi kuyafanya kiujumla na sasa hivi hatuwezi kulifumua kufanya mabadiliko yoyote vinginevyo uchaguzi hautafanyika. Tukubali kuwa watakaoshindwa kupiga kura sio wanavyuo peke yao.”

  Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa muundo wa karatasi za kura umebadilika.

  Alisema kuwa muundo wa sasa, Mpiga kura baada ya kumaliza taratibu zote za kujitamblisha na kukabidhiwa karatasi za Kura, atatakiwa kuweka alama ya Vema inayoashiria amemchagua nani kwenye chumba kilicho wazi, kulia kwa picha ya Mgombea.

  “Hata akiweka alama hiyo katika picha, kura hiyo itatambuliwa kwasababu ameonyesha dhamira yake,” alisema.

  MWISHO.
   
 9. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwani liko wapi tatizo la wapiga kura kuandikishwa milioni 19,728,919?????
   
 10. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Matatizo: Wote tunajua komputa hufanya inachoagizwa kufanya tena kwa ufanisi zaidi. Tatizo ni:
  1. TUME SIO HURU - haina watendaji wake Wilayani
  2. Sio siri watendaji wa tume ni makada wa CCM
  3. CCM imeshaonyesha kutoheshimu TUME kwa kuwahamisha watendaji (DED) wakati wa zoezi hili na TUME haikuweza kufanya lolote ilhali wanajua kuwa zoezi litaathiriwa
  4. CCM imeshawatisha watendaji hao kuwa watafutwa kazi kama CCM itashindwa majimboni mwao.

  Suluhisho:
  Watafutwe wasimamizi wa uchaguzi wasiotegemea CCM kwa maisha yao. Hata kama watatoka mwezini.

  Mazingira haya ndiyo yatasababisha matokeo yawe na utata na NI LAZIMA hayataaminika. NEC haitaweza kuwahakikishia waTZ kuwa CCM itakuwa imeshinda kwa halali hata kama itakuwa ndi hivyo. Hekima ilitakiwa iwepo miaka minne iliyopita kuibadilisha hii tume na utendaji wake. CCM wakakataa wakijua hakutakuwa na upinzani mkumbwa wa kuwasumbua.

  Kujitokeza kwa Dr Slaa kumebadilisha picha nzima. Walio wengi wataibiwa kura zao na utegemee vurugu. Kwa kujihami, wameanza kutishia watu kwa kauli za jeshi. Shimbo hawezi kutoa kauli aliyoitoa kama hakutumwa na JK. PIa JK hajatamka kuwa hata yeye akishindwa atakubali! ATATUMIA NGUVU KUBAKI IKULU kwa kuwa ana uhakika kura zitakazompa sio zilizopigwa na wa TZ bali zitakazoandikwa kwenye karatasi ya matokeo.

  Naomba Mungu apishilizie mbali lakini hii kwangu ni ishara mbaya ki usalama.
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwanin mpaka sasa hawajabandika majina??NEC hii ndo hujuma wanayotaka kufanya??
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Watahakiki yes. lakini kwa namna hao wataalam wa nec walivyoiandaa walah tutaona maajabu siku ya ukokotoaji matokeo.

  NEC haijawa huru, je inadhani tunaamini kwamba hata hizo ajira zao za ndani zipo huru kiasi cha kutoa na kusimamia haki?
   
 13. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa nini waweke kwenye Facebook, magazeti ya taifa.....oh sorry I meant magazeti ya SISIEMU yako wapi kuweka hiyo taarifa, sijui ombi!!
   
 14. b

  bojuka Senior Member

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutoka kusini mwa tanzania kuna taarif kuwa j4 wataalam wa IT wanakwenda kufundishwa namna ya kuchakachua matokeo JIJINI DAR. Wanajf wenye utaalam wa kujua wizi huo watuelimishe kuokoa taifa letu.
   
 15. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kamuulizen kabourou enzi zile alipokuwa KIgoma Chadema alikuwa anashindaje? na kwa nini matokeo yalikuwa hayabadilishwi?
   
Loading...