NEC inabidi ifunguliwe mashtaka kwa ahadi za uongo. -Mawakili wa upinzani kazi kwenu


Mwiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
7,614
Likes
230
Points
160
Mwiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
7,614 230 160
Nchi ya Brazil walifanya uchaguzi siku ya Jumapili kama Tanzania. Idadi ya watu (population) huko Brazil ni kiasi cha 190 milioni na eneo la nchi yao ni kilometa za mraba 8,514,877 (square kilometres).Matokeo a uchaguzi wao yalitangazwa Jumapili jioni mara tu baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika.

Cha kushangaza ni kuwa mpaka dakika hii NEC hawajamaliza kujumlisha idadi za kura. Tuliambiwa kuwa kura zingehesabiwa katika vituo. Huo, kama si uzembe uliokubuhu, basi ni uzezeta uliopindukia mipaka. Ni aibu kuwa na tume yenye kiwango cha utekelezaji wa aina hiyo. Ni hasara na mzigo mkubwa wa walipa kodi ambao wengi wao ni wanyonge wa Mungu.

Nasubiri kwa hamu siku ambayo tume hii itapelekwa mahala inapostahiki kuwepo.
 

Forum statistics

Threads 1,251,868
Members 481,917
Posts 29,788,291