NEC ilipanga kuboresha daftari la wapiga kura Arumeru, serikali ilikataa kutoa fedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC ilipanga kuboresha daftari la wapiga kura Arumeru, serikali ilikataa kutoa fedha

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Zak Malang, Apr 2, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza nakiri kuwa habari hizi ni tetesi, na ndiyo maana nimezainisha vilivyo. Ni habari nizopata kutoka kwa mtu ninayefahamiana naye katika Tume ya Uchaguzi (NEC) katika ngazi za juu. Hivyo unaweza kuchukuwa kwamba source ya hii ni mimi, ingawa sijazithibitisha, lakini wana-JF wenye jamaa, maswahiba nk katika NEC wanaweza kufuatilia hili ili kupata ukweli wake:

  Bada ya jimbo la Arumeru kutangazwa kuwa wazi, NEC chini ya uongozi mpya wa Jaji mstaafu Damian Lubuva aliamua kuboresha daftari la kupiga kura katika jimbo hilo, na pia katika maeneo mengine, yaani kata ambazo pia zilitangazwa kuwa wazi.

  NEC iliona kwamba tangu mara ya mwisho daftari lilipoboreshwa takriban miaka mitatu iliyopita, kuna maelfu ya watu hasa vijana waliotimiza miaka 18 hawamo katika daftari, na watu wengine wengi waliokufa, waliohama nk ambao bado wamo.

  NEC ilifanya tathmini na kuona kwamba ingeweza kufanya zoezi hilo katika majimbo husika kwa muda wa mwezi mmoja, na hivyo chaguzi husika zisogezwe mbele kwa mwezi mmoja kutoa nafasi ya kuboresha daftari. Hivyo NEC ikapeleka maombi hayo serikalini na kuomba fungu Sh 1.2 bilioni.

  Serikali ikakataa kutoa fungu kwa maelezo kwamba hakuna fedha na hivyo kuiambia NEC katika chaguzi hizo itumie takwimu za daftari za miaka 3 iliyopita.

  Ikawa hakuna namna tena. Mtoa habari wangu pia alinieleza kuwa Lubuva alipanga kulizungumzia hili katika mkutano wake na waandishi wa habari wiki kadha zilizopita, lakini baadaye aliamua vinginevyo. Huenda serikali ilimwelekeza asilizungumzie.

  My take: Huenda serikali ilikuwa na valid reason ya ukosefu wa fedha, lakini p[ia iliogopa kwamba iwapo daftari lingeboreshwa, hasa huko Arumeru, basi vijana wengi wangejiandikisha kupiga kura, vijana ambao inasadikiwa wengi nwao ni wa Chadema.   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kama kweli lengo lao ilikuwa ni kupunguza kura za vijana baada ya kuona wana kiu ya mabadiliko, watakuwa wanajidanganya tu. Kwani kutakuwa hakuna jinsi tena ya kuwazuia vijana kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 ambao ndiyo utakuwa wa kuizika ccm.
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nadhani walikuwa wanataka kufanya jambo zuri sana
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Daftari lililoboreshwa ndio suluhu!
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania nayo imekuwa na gharama za ajabu! Tsh 1.2 billion kuboresha daftari la kura kwenye maeneo machache hivyo? Kuna nini kikubwa kinachofanyika hadi watake 1.2 billion?
   
 6. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizi ni Chai tu.... Hakuna jipya mnataka kujitoa.... NEC ni nani na Serikali ni nani? Mbona mnatuzingua? Isue hapa ni serika na mafisadi na NEC lao moja tu...

  Huu ni wizi mtupu... Mrekebishe daftari muache hata wakipiga kura watu 2 tunawapiga bao tu.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa CDM wameshinda Arumeru bila kuboreshwa daftari, basi CCM lazima wajisikie wako mavini. Ina maana wazee sasa nao pia wanaikubali CDM kwa kasi ya ajabu. Watafute mikakati mingine kuliko hii ya kunyima watu haki zao za msingi za kupiga kura.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  chadema inabidi ipeleke mswaada bungeni maalum wa sheria utakayoitaka tume ya uchaguzi kumuandikisha mtanzania yeyote ambaye amefikisha umri wa 18 au zaidi pindi anapokuwa na sifa za kuwa mpiga kura. haiwezekani watu wasubiri kwa miaka 5 ili wapewe nafasi ya kujiandikisha tena kwani huo ni ugandamizaji wa demokrasia wa kutupwa. kwahiyo cdm hii ni nafasi yenu muhimu na hata kama mswaada huo ukikwama lakini mtakuwa mmeshapeleka ujumbe mkubwa across the country kwa vijana wote kwamba adui yao ni nani anayewauzia haki yao ya kupiga kura?
   
Loading...