NEC: Idadi ya Wapiga Kura bara ni 22,751,292 na Zanzibar ni 503,193

Namshukuru Mungu ckuwahi mpgia kura huyu jamaa na chama chake hata cku moja kwa sababu hawa ni janga la taifa yy na chama chake.Wanafikir na kutuona km watz ni watumwa kwao vle
 
Inabidi ukawa wawabane hawa watu vizuri. Lakini mnyika machale yalishamcheza. Hapa ni kwamba kwenye kituo lawasa inaweza kuwa kura 190 magufuli 170 then mchakato unafanywa wa kumuongezea magufuli 90 then anakua na 260. Bao la mkono linapigwa kiulaini. Na uchaguzi wa bongo ni simple majority tu hata akipata asilimia 50.1 ameshinda. CCM wanafanya wizi wa huu uchaguzi. Tena mchana kweupe na sisi tunashuuhudia.
 
Katika magazeti ya leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amenukuliwa akisema kuwa:
1. jumla ya vituo vya kupigia kura ni 64,736
2. Kila kituo kitakuwa na wapigakura 450.
3. jumla ya wapiga kura waliothibitishwa ni 23,254,485 (22,751,292 (Bara), 503,193 (Zanzibar)

Ukokotoaji:
1. jumla ya wapiga kura (23,254,485) ugawe kwa idadi ya wapiga kura kila kituo (450) = 51,677
Hii ina maana kwamba, vituo vilivyohitajika kupigia kura ni 51,677 tu na sio 64,736. hii ina maana kuna nyongeza ya vituo 13,059. HIVI NI VITUO 'HEWA'? vya nini na kwa faida ya nani?

2. Ikiwa kila kituo ni watu 450 na vituo hewa ni 13,059, hii ina maana kuwa jumla ya wapiga kura katika 'hewa' (Maruhani) ni 450x13,059 = 5,876,555. Maruhani karibu milioni 6 watapiga kura! wanatoka wapi? nani atawaleta? kwa faida ya nai? je tume inawahitaji hawa?

3. Kwa idadi ya vituo 64,736 na wapiga kura 23,254,485, maana yake ni kuwa kila kituo kinapaswa kuwa na watu 360 tu, na sio 450 kama tume inavyotueleza.(chukua idadi ya wapiga kura ugawe kwa idadi ya vituo vya kupigia kura vya NEC - 450). hII INA MAANA KUWA kwa kila kituo kutakuwa na nyongeza ya watu (Maruhani) 90 (450-360). tunajiuliza, hawa wameongezwa kwa faida ya nani?

4. Ikiwa idadi ya vituo ni 64,736 na kila kituo wapiga kura 450, hii ni sawa sawa na idadi ya wapiga kura 29,131,200 (64,736x450). maana yake ni kuwa wapiga kura waliozidi (kutoka 23,254,485) ni 5,876,715.

NB: Tume itoe maelezo ya kina na watuambie wametumia 'calculation' za mtaala wa hesabu wa nchi gani ambao ni tofauti kabisa na huu wa kwetu?
 
Naomba niseme jambo hapo kwa jins ambavyo mkurugenz NEC alvyosema idadi ya watu walioandikshwa kwenye ktuo kimoja ndio watakao gawanywa kwenye vtuo vdogo vdpgo vya kupgia kura vyenye watu 450 na watakaobaki watatengenezewa ktuo kngne.

Lets say kituo kikubwa kiliandksha watu 1700 hvi kwa hesabu za watu 450 hapa utapata vtuo vdogo vya kupgia kura kutoka kwenye hcho ktuo cha kuandksha wapga kura 3 ambavyo idadi yake ni watu 1350 na watu 350 wataanzsha ktuo kngne!!!

Hesabu ya aina hii itafanyka kwenye kla ktuo kikubwa klchoandksha wapga kura kwahyo kwa maono yangu kla ktuo kikubwa ndcho ktachozalsha hivi vtuo vya zaida kwahyo hapa si kuangalia idadi ya wapga kura wote ila ni kuangalia kla ktuo kmeandsha watu wangap na mgawanyo wake uko vp!!!
 
Naona cha msingi Ukawa waanze kuhakiki vituo viko sehemu gani, wasiwasi wangu mwingine ni upande wa zanzibar! Kule nafikiri kuna vituo vitakuwa na watu mia
 
Idadi ya Wagombea wa Ubunge
Jumla Wagombea 1,218 wa nafasi ya Ubunge waliteuliwa, Kati ya hao Wanaume ni 985 na wanawake ni 233.

Idadi ya Wagombea wa Udiwani
Jumla ya Wagombea 10,879 waliteuliwa kuwania nafasi za
Udiwani kati ya hao wanaume 10,191 na wanawake 679.

Jumla ya Majimbo 264 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kata 3,957 za Tanzania Bara zitashiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Jumla ya Wagombea 8 wa nafasi ya Kiti cha Rais waliteuliwa kuwa Wagombea kati ya hao mwanamke ni 1 na wanaume 7.

Jumla ya Vyama vya siasa tisa (9) tu ndivyo vimewasilisha fomu na majina ya wagombea wa Viti Maalum mpaka ilipofika siku ya mwisho, yaani tarehe 25 Septemba, 2015. Vyama hivyo ni CCM, CUF, UPDP, UMD, TLP, DP, NLD na ACT-Wazalendo. Vyama vingine mpaka sasa havijawasilisha orodha kama Sheria inavyosema.

Jumla ya taarifa za wananchi 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja hadi mara nane kwa mtu mmoja.

Jumla ya taarifa 3,870 wamebainika kuwa waliandikishwa wakiwa sio raia wa Tanzania na hivyo, vitambulisho vyao vimerejeshwa na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya Daftari la Kudumu.

Hivyo, jumla ya taarifa za Wapiga kura 1,031,769 zimefutwa kutokana na sababu tajwa hapo juu.

Kwa maana hiyo, idadi halisi ya Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga la Kura ni 22,751,292 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 503,193 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

Idadi ya Vituo vya Kupigia Kura
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 65,105, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 525 na Zanzibar ni Vituo 1,580. Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500.

Asante kwa taarifa nzuri. Wanaotengeneza idadi yao wanalao jambo. Wasilaum mtu wao ndiyo chanzo cha maneno yasiyo na msingi wowote.
 
Inabidi ukawa wawabane hawa watu vizuri. Lakini mnyika machale yalishamcheza. Hapa ni kwamba kwenye kituo lawasa inaweza kuwa kura 190 magufuli 170 then mchakato unafanywa wa kumuongezea magufuli 90 then anakua na 260. Bao la mkono linapigwa kiulaini. Na uchaguzi wa bongo ni simple majority tu hata akipata asilimia 50.1 ameshinda. CCM wanafanya wizi wa huu uchaguzi. Tena mchana kweupe na sisi tunashuuhudia.

Usitumie title ya Dr. kama reasoning yako ndogo hivyo.
 
UKAWA hebu jifunzeni kusoma na kuelewa. Mnaboa sana na vihoja vyenu vya uchochezi na kulaumu kila kitu.

Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500.

Ni kipi msichoelewa hapo?

Labda niwasaidie.

1. Kila mwanaume wa Kiislam ana uwezo wa kuoa wake wanne. Je ina maanisha wanaume wote wa Kiislam wana wake wanne? (La hasha, wengi wana mke mmoja)

2. UDOM kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 50,000. Je ina maanisha kuna wanafunzi 50,000 UDOM? (La hasha, hawafiki hata 20,000)
 
Ukiangalia kwa umakini utagundua idadi ya wapiga kura aliyoitoa kikwete ina onyesha uhusiano mkubwa na idadi ya vituo vya wapiga kura vilivyotangazwa. vituo elfu 65 vilivyotangazwa ni sawa na wapiga kura milioni 29 kwa kila kifuo kubeba watu 450 kwa makadirio ya juu.

Data za lubuva zinazua utata mkubwa kwa wapiga kura kwani hazionyeshi uhusiano wowote na vituo vya kupigia kura vilivyo tangazwa. idadi ya vituo vya kupigia kura imepaa mno hivyo kikwete data zake ndio zipo sahihi kwani hata ukitoa wale wapiga milioni moja walio tolewa bado data hizo zinashadidia uhalisia.

Lubuva kwa nini udanganye umma wa watanzania
 
Tumia akili angalau hata kidogo! Lubuva ni mwenyekiti wa tume,ndie msemaji wa tume. Kikwete hawezi kuwa msemaji wa tume. Takwimu za Lubuva ndio rasimi.
 
Basi tunaziamini data za Kikwete mwenyekiti wa tume ya uchaguzi :sad::sad::sad:
 
Mleta Mada,Kikwete hao watu aliowatangaza alikuwa anawasajili yeye binafsi na kina Ridhiwani,Ali,Miraji,Mwanaasha,Khalfani na nduguze pale Msoga?!! Then Lubuva wa nini?!
 
Hivi unafikiri watu ni kama mahindi? Kila kituo unaambiwa si zaidi (NOT MORE THAN) 450. Hivyo authority ya kutoa idadi ya waliojiandikisha ni LUBUVA. Na watakaopiga kura lazima wawe pungufu ya Data za Lubuva
 
Ukiangalia kwa umakini utagundua idadi ya wapiga kura aliyoitoa kikwete ina onyesha uhusiano mkubwa na idadi ya vituo vya wapiga kura vilivyotangazwa. vituo elfu 65 vilivyotangazwa ni sawa na wapiga kura milioni 29 kwa kila kifuo kubeba watu 450 kwa makadirio ya juu.

Data za lubuva zinazua utata mkubwa kwa wapiga kura kwani hazionyeshi uhusiano wowote na vituo vya kupigia kura vilivyo tangazwa. idadi ya vituo vya kupigia kura imepaa mno .


Mleta mada ni hivi, kwa mujibu wa goli la mkono Kikwete yuko sahihi, lakini kwa jinsi tume ilivyobanwa hapo ilipo inashindwa kujua ichukue idadi ipi, hiyo halali ya tume au hiyo ya mwenyekiti wa ccm ya goli la mkono.
 
Back
Top Bottom