Uchaguzi 2020 NEC: Hatutaruhusu mtu kukaa mita 100 kusubiri matokeo ya uchaguzi

Ni Mjinga pekee anayeamini kwamba maaskari wapo na Ccm, labda Mabeyo,Sirro, yule mkuu wa Magereza, kale kamama ka uhamiaji, na yule wa zimamoto
 
Kipanya ( 386 X 640 ).jpg
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kukaa mita 100, kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Badala yake NEC imeelekeza kuwa kila mpiga kura anayekwenda kupiga kura kituoni, baada ya kukamilisha shughuli hiyo arudi nyumbani.

Hayo yalielezwa na Ofisa elimu kitengo cha mpigakura, Nuru Liwa, katika mkutano wa kuijengea uwezo Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC).

Liwa alisema ni kosa la jinai kukiuka utaratibu uliowekwa na NEC siku ya kupiga kura na kabla ya kupiga kura na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakao kiuka sheria

Mpigakura unatakiwa kufika kituoni katika muda uliotapangwa na NEC na muda wa kupiga kura ukiiisha hakuna mtu mwingine atakayeruhusiwa kupiga kura, lakini ikitokea muda umeisha na wapiga kura wapo katika mstari, askari wa kituo husika atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho hadi wale waliokuwa katika mstari wamalizike kupiga kura,” alisema Liwa.

Mbali na kutoruhusu mtu yoyote kukaa mita 100 kutoka katika kituo husika, pia NEC imetahadharisha watu kutokuchana orodha ya wapiga kura pamoja na mabango yanayoelezea elimu kwa mpiga kura yaliyopo katika vituo vya kupigia kura.

“Kuchana mabango yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura ni kosa, hivyo wananchi wajiepushe na jambo hilo, na wananchi wanatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa katika siku ya kupiga kura ili kuepuka kuvunja sheria,” alisema Liwa.

Suala hilo liliibua mvutano katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, hadi likafikishwa kortini ambapo Mahakama Kuu iliamuru kuwa si ruhusu watu kukaaa mita 100 kutoka kituo cha kupigia kura.
Awali, Mwenyekiti wa Klabu ya DCPC, Irene Mark aliwataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuhabarisha jamii badala kupotosha umma.

“Nawaomba wanahabari wenzangu, tutumie kalamu zetu vizuri kwa ajili ya kuelimisha umma, si katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, bali wakati wote kwa sababu waandishi ndio masikio ya jamii,” alisema Mark.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Kitengo cha usimamizi na utekelezaji wa Sheria na masharti ya leseni, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA), Dk Philip Filikunjombe amewataka waandishi wa kuisoma vizuri sheria ya maudhui ya vyombo vya habari ili waweze kuelimisha jamii wakati wa uchaguzi.

Alisema kama mwanahabari ataielewe vizuri sheria hiyo, itamsaidia katika utendaji kazi wake.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo la watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii, Dk Filikunjombe alisema, wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kuruhusu kupiga au kupigwa picha zenye utata na wapenzi wao ambao kuzituma mitandaoni.

Alisema TCRA, imekuwa ikipokea kesi nyingi za namna hiyo, nyingi zinawahusu wanawake kudhalilishwa mitandaoni kwa sababu wao ni wachangiaji wakubwa wa masuala binafsi mtandaoni.

SHERIA inaruhusu kukaa mita Mia mbili (200) siyo kwenda NYUMBANI.
 
Wana uwezo gani wa kutuzuia?

Wana nini wao Kama Nani ? Tena hatukai mita mia tunakaa nje ya kituo mpaka kieleweke.

Yaani tukiamka tarehe 28 asubuhi haturudi ndani mpaka Lissu atangazwe ..

Sheria inasema watu wanaweza kukaa mita mia halafu wenyewe wanaleta bla bla..

Wajaribu kuzuia nguvu ya umma mwaka huu waone Kama wataweza mwaka huu hatuna mchezo kabisa na uchaguzi..
Thubutu kutia mguu ndani ya mita 200 uone moto
 
Wametunga sheria ya kuwalinda ili wanapokwiba kura,ambapo ni kosa la jinai wasibughudhiwe na watu??
 
SHERIA inaruhusu kukaa mita Mia mbili (200) siyo kwenda NYUMBANI.

Mahakama kuu ya Tanzania yamaliza mzozo wa mita 200​

23 Oktoba, 2015
Mahakama kuu ya Tanzania iliamua kutoruhusu mikusanyiko ya watu umbali wa mita 200.

Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Dar Es Salaam, Alhamis iliamua kutoruhusu mikutano wala mikusanyiko yeyote ya watu umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika hukumu ya shauri la kikatiba lililofunguliwa na mwanasheria mmoja hivi karibuni.

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa shauku na watanzania ilifuatia shauri hilo la kikatiba lililofunguliwa na mgombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, alipoiomba mahakama kutoa tafsiri ya kifungu cha sheria namba 104 kifungu kidogo cha 1,sura ya 343, akiomba mahakama iangalie maana ya kifungu hicho cha watu kuweza kukaa mita 200 kutoka umbali wa kituo cha kupiga kura.

Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji watatu lililokuwa linaongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo, jaji Lugano Mwamdambo , alisema mahakama hiyo katika tafsiri yake, ilisema, sheria iko wazi na bayana na kwamba inakataza mikutano, bila kujali umbali na kwamba tafsiri ya sheria namba 72 inaeleza watu gani wanapaswa kuwepo sehemu ya kuhesabia kura na kwamba ambaye hakutajwa hatakiwi kuwepo eneo hilo.

Akisisitiza tafsiri hiyo, kiongozi wa jopo la majaji hao,Jaji Sakieti Kihiyo, alisema,sheria inakataza pia mikusanyiko, uwepo wa nembo, bendera ama alama yoyote ya chama umbali wowote katika siku hiyo ya uchaguzi.
 
Wana uwezo gani wa kutuzuia?

Wana nini wao Kama Nani ? Tena hatukai mita mia tunakaa nje ya kituo mpaka kieleweke.

Yaani tukiamka tarehe 28 asubuhi haturudi ndani mpaka Lissu atangazwe ..

Sheria inasema watu wanaweza kukaa mita mia halafu wenyewe wanaleta bla bla..

Wajaribu kuzuia nguvu ya umma mwaka huu waone Kama wataweza mwaka huu hatuna mchezo kabisa na uchaguzi..
Sema sikai na sio hatukai, kwa anaeelewa utaratibu wa uchaguzi lazima ataondoka, nyie ndio watu ambao mnasubiria kipigo eee...sasa jaribu uonee.

Kura yangu kwa Magufuli
 
Thubutu kutia mguu ndani ya mita 200 uone moto
Wacha wajiingize kwenye moto hukumu ya hiyo kesi ilishaamriwa na Mahakama kuu 2015 hukumu hii hapa

Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa jana na jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza shauri hilo, likiongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo, akisaidiana na Aloyisius Mujulizi na Lugano Mwandambo, ilikataa ombi hilo la mtoa maombi. Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya jopo hilo, Jaji Mwandambo alisema mdai amefanikiwa katika maombi yake kwa kiwango cha kupata tafsiri sahihi tu ya kifungu hicho, kama alivyoomba.
“Kwa upande wa pili, hakufanikiwa katika ombi lake la pili la dai la kukiukwa kwa haki yake ya kusimama au kuwapo umbali wa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura,” alisema Jaji Mwandambo katika uamuzi huo.
Kuhusu tafsiri kama mdai alivyoomba, Mahakama ilisema kifungu hicho kinapiga marufuku mambo yote yaliyoainishwa. “Hatuna shaka kwamba Kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi (Sura ya 343 kilichorejewa mwaka 2002) ni cha kuweka marufuku kwa mtu yeyote kufanya mambo yaliyoainishwa katika maeneo mahsusi na kwa wakati maalumu.”
Akisoma tafsiri ya kifungu hicho, Jaji Mwandambo alisema: “Ni marufuku kwa mtu yeyote kuitisha au kufanya mkutano wa aina yoyote siku ya uchaguzi; mahsusi kwa kufanyika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi au katika eneo la jimbo la uchaguzi kunakofanyika uchaguzi wa mbunge:
“Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvaa au kuonyesha kadi, picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea fulani katika uchaguzi, ama ndani ya jengo ambamo zoezi la kupiga kura linafanyika au kuendelea: “Ni marufuku kwa mtu yeyote kuonyesha au kuvaa kadi au picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea fulani katika uchaguzi, popote pale ndani ya wigo wa mita 200 kutoka kituo ambako zoezi la uchaguzi linafanyika au ambako zoezi la kuhesabu kura linafanyika.”
Jaji Mwandambo alisema kifungu hicho pia kinafanya kuwa kosa la jinai kwa yeyote yule atakayefanya hayo yote yaliyopigwa marufuku.
Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 104 (2) cha Sheria ya Uchaguzi, mtu anayefanya mambo hayo yaliyopigwa marufuku anaweza kushtakiwa mahakamani na kwa kosa hilo. Alisisitiza kuwa hicho ni kifungu jinai na kinatakiwa kutafsiriwa moja kwa moja pasipo kuingiza maana ambayo haikukusudiwa na Bunge.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Akson alitoa wito kwa wananchi kufuata uamuzi huo akisema Mahakama ndicho chombo chenye mamlaka ya kutoa tafsiri ya kisheria.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Mimi Francis John Njewike mpiga kura kituo cha TIA uhasibu karibu na kambi ya twalipo nitalinda kura yangu pamoja na baadhi ya wanajeshi wa hapo kambini, kwani hakuna mwanajeshi hapo kambini anaipenda Ccm tena,nimedokezwa watanisapoti.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kukaa mita 100, kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Badala yake NEC imeelekeza kuwa kila mpiga kura anayekwenda kupiga kura kituoni, baada ya kukamilisha shughuli hiyo arudi nyumbani.

Hayo yalielezwa na Ofisa elimu kitengo cha mpigakura, Nuru Liwa, katika mkutano wa kuijengea uwezo Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC).

Liwa alisema ni kosa la jinai kukiuka utaratibu uliowekwa na NEC siku ya kupiga kura na kabla ya kupiga kura na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakao kiuka sheria

Mpigakura unatakiwa kufika kituoni katika muda uliotapangwa na NEC na muda wa kupiga kura ukiiisha hakuna mtu mwingine atakayeruhusiwa kupiga kura, lakini ikitokea muda umeisha na wapiga kura wapo katika mstari, askari wa kituo husika atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho hadi wale waliokuwa katika mstari wamalizike kupiga kura,” alisema Liwa.

Mbali na kutoruhusu mtu yoyote kukaa mita 100 kutoka katika kituo husika, pia NEC imetahadharisha watu kutokuchana orodha ya wapiga kura pamoja na mabango yanayoelezea elimu kwa mpiga kura yaliyopo katika vituo vya kupigia kura.

“Kuchana mabango yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura ni kosa, hivyo wananchi wajiepushe na jambo hilo, na wananchi wanatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa katika siku ya kupiga kura ili kuepuka kuvunja sheria,” alisema Liwa.

Suala hilo liliibua mvutano katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, hadi likafikishwa kortini ambapo Mahakama Kuu iliamuru kuwa si ruhusu watu kukaaa mita 100 kutoka kituo cha kupigia kura.
Awali, Mwenyekiti wa Klabu ya DCPC, Irene Mark aliwataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuhabarisha jamii badala kupotosha umma.

“Nawaomba wanahabari wenzangu, tutumie kalamu zetu vizuri kwa ajili ya kuelimisha umma, si katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, bali wakati wote kwa sababu waandishi ndio masikio ya jamii,” alisema Mark.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Kitengo cha usimamizi na utekelezaji wa Sheria na masharti ya leseni, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA), Dk Philip Filikunjombe amewataka waandishi wa kuisoma vizuri sheria ya maudhui ya vyombo vya habari ili waweze kuelimisha jamii wakati wa uchaguzi.

Alisema kama mwanahabari ataielewe vizuri sheria hiyo, itamsaidia katika utendaji kazi wake.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo la watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii, Dk Filikunjombe alisema, wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kuruhusu kupiga au kupigwa picha zenye utata na wapenzi wao ambao kuzituma mitandaoni.

Alisema TCRA, imekuwa ikipokea kesi nyingi za namna hiyo, nyingi zinawahusu wanawake kudhalilishwa mitandaoni kwa sababu wao ni wachangiaji wakubwa wa masuala binafsi mtandaoni.
Sheria za uchaguzi zinasema kaa mita 100 ,sisi tutakaa kulinda kura zetu.
 
Wana uwezo gani wa kutuzuia?

Wana nini wao Kama Nani ? Tena hatukai mita mia tunakaa nje ya kituo mpaka kieleweke.

Yaani tukiamka tarehe 28 asubuhi haturudi ndani mpaka Lissu atangazwe ..

Sheria inasema watu wanaweza kukaa mita mia halafu wenyewe wanaleta bla bla..

Wajaribu kuzuia nguvu ya umma mwaka huu waone Kama wataweza mwaka huu hatuna mchezo kabisa na uchaguzi..
Kwenye Mitandao mnaweza sana!! Nje na Mitandao ni hoho tupu
 
Sheria za uchaguzi zinasema kaa mita 100 ,sisi tutakaa kulinda kura zetu.
Nikishamaliza kupiga Kura yangu basi tena, kama hazitatosha Kwa niliyemchagua, shauri yake!

Siwezi kuacha usingizi wangu Kwa ajiri yake, siwezi kujitaabisha tena Kwa lolote Kwa ajiri yake!

Akiona ameibiwa, mahakama IPO, aende huko

Ya nini kujipa tabu nyingine baada ya kupiga Kura?

Huo nimsimamo wangu Paul Sylvester

Eti nikaandamane! Kwangu huo ni upumbavu na ujinga na pia ni kuonesha uzembe wa kazi,

Tunawawakilishi kibao bungeni wa vyama mbalimbali, Kwa nini wasipiganie tume huru humo bungeni?

Kwa nini wasitupiganie kutuletea katiba humo bungeni?

Wakome kutujua baada ya kupiga kura
 
Back
Top Bottom