Uchaguzi 2020 NEC: Hatutaruhusu mtu kukaa mita 100 kusubiri matokeo ya uchaguzi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kukaa mita 100, kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Badala yake NEC imeelekeza kuwa kila mpiga kura anayekwenda kupiga kura kituoni, baada ya kukamilisha shughuli hiyo arudi nyumbani.

Hayo yalielezwa na Ofisa elimu kitengo cha mpigakura, Nuru Liwa, katika mkutano wa kuijengea uwezo Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC).

Liwa alisema ni kosa la jinai kukiuka utaratibu uliowekwa na NEC siku ya kupiga kura na kabla ya kupiga kura na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakao kiuka sheria

Mpigakura unatakiwa kufika kituoni katika muda uliotapangwa na NEC na muda wa kupiga kura ukiiisha hakuna mtu mwingine atakayeruhusiwa kupiga kura, lakini ikitokea muda umeisha na wapiga kura wapo katika mstari, askari wa kituo husika atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho hadi wale waliokuwa katika mstari wamalizike kupiga kura,” alisema Liwa.

Mbali na kutoruhusu mtu yoyote kukaa mita 100 kutoka katika kituo husika, pia NEC imetahadharisha watu kutokuchana orodha ya wapiga kura pamoja na mabango yanayoelezea elimu kwa mpiga kura yaliyopo katika vituo vya kupigia kura.

“Kuchana mabango yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura ni kosa, hivyo wananchi wajiepushe na jambo hilo, na wananchi wanatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa katika siku ya kupiga kura ili kuepuka kuvunja sheria,” alisema Liwa.

Suala hilo liliibua mvutano katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, hadi likafikishwa kortini ambapo Mahakama Kuu iliamuru kuwa si ruhusu watu kukaaa mita 100 kutoka kituo cha kupigia kura.
Awali, Mwenyekiti wa Klabu ya DCPC, Irene Mark aliwataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuhabarisha jamii badala kupotosha umma.

“Nawaomba wanahabari wenzangu, tutumie kalamu zetu vizuri kwa ajili ya kuelimisha umma, si katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, bali wakati wote kwa sababu waandishi ndio masikio ya jamii,” alisema Mark.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Kitengo cha usimamizi na utekelezaji wa Sheria na masharti ya leseni, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA), Dk Philip Filikunjombe amewataka waandishi wa kuisoma vizuri sheria ya maudhui ya vyombo vya habari ili waweze kuelimisha jamii wakati wa uchaguzi.

Alisema kama mwanahabari ataielewe vizuri sheria hiyo, itamsaidia katika utendaji kazi wake.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo la watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii, Dk Filikunjombe alisema, wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kuruhusu kupiga au kupigwa picha zenye utata na wapenzi wao ambao kuzituma mitandaoni.

Alisema TCRA, imekuwa ikipokea kesi nyingi za namna hiyo, nyingi zinawahusu wanawake kudhalilishwa mitandaoni kwa sababu wao ni wachangiaji wakubwa wa masuala binafsi mtandaoni.
 
Wana uwezo gani wa kutuzuia?

Wana nini wao Kama Nani? Tena hatukai mita mia tunakaa nje ya kituo mpaka kieleweke.

Yaani tukiamka tarehe 28 asubuhi haturudi ndani mpaka Lissu atangazwe.

Sheria inasema watu wanaweza kukaa mita mia halafu wenyewe wanaleta bla bla.

Wajaribu kuzuia nguvu ya umma mwaka huu waone Kama wataweza mwaka huu hatuna mchezo kabisa na uchaguzi.
 
Wana uwezo gani wa kutuzuia?

Wana nini wao Kama Nani ? Tena hatukai mita mia tunakaa nje ya kituo mpaka kieleweke.

Yaani tukiamka tarehe 28 asubuhi haturudi ndani mpaka Lissu atangazwe ..

Sheria inasema watu wanaweza kukaa mita mia halafu wenyewe wanaleta bla bla..

Wajaribu kuzuia nguvu ya umma mwaka huu waone Kama wataweza mwaka huu hatuna mchezo kabisa na uchaguzi..
Lazima kura zilindwe
 
Ni kwanini wana wasiwasi kama haki itatendeka!
Wanajua kuwa hawana mpango wa kutenda haki
JamiiForums2000245234.jpg
 
Back
Top Bottom