NEC: Hatujapata taarifa za Kafumu kuvuliwa ubunge

hatuna uongozi thabiti ndio tatizo kila anaeongoza ni maneno kuliko vitendo haijulikani nani anatakiwa afanye nini ..
kila mtu anasubiri aletewe mezani au akurupushwe ndio afanye wananchi wasipo goma busi tena
 
Sasa wamejuaje kuwa hukumu ina mapungufu ilhsli hawajaipitia bado? mwongo utamjua tuu
 
Kafumu hataki siasa,hataki kukata rufaa na hataki tena ubunge wao wanataka kumlazimisha kukata rufaa ili iweje? tusubiri tuone maana katika kesi hii anayetakiwa kukata rufaa ni kafumu wasije wakafoji hata saini yake ili mradi tu ionekane amekata rufaa.
 
Tanzania tuna tatizo kubwa sana la watu/taasisi kukaa na kusubiri kila kitu kiletwe kwenye sahani. Tumeona polisi inavyotaka 'muathirika' awe ndio mpelelezi badala ya wao kufanya kazi hiyo, sasa NEC nayo inasubiri iletewe kila kitu. Kama hao wakubwa wamesikia taarifa inayohusu ofisi yao kwenye vyombo vya habari, wameshindwa kitu gani kuwasiliana (kwa barua) na ofisi husika ili wapate barua 'maalum?

Well said. Nimebaki najiuliza, hivi watumishi wa nchi hii wakoje? Wao huwa hawafuatilii bali wanasubiri kuletewa?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Watakata rufaa lakinu yawezekana kwamba wanataka tuu kupunguza facts zilizowadondosha lakini hawawezi kushinda hata chembe

Si wanafanya kuwaiga CDM pasipo kutumia akili na kuangalia mwenendo wa mambo
 
Kwa mwenye kumbukumbu kuhusu ile kesi ya Arusha iliyong'oa Lema madarakani ilichukua muda gani kwa NEC kutangaza jimbo liko wazi na walingoja jalada la hukumu kama sasa ama wana lao jambo kwa hao waajiri wao?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom