NEC: Hatujapata taarifa za Kafumu kuvuliwa ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC: Hatujapata taarifa za Kafumu kuvuliwa ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 30, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema bado haijapata taarifa rasmi za hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora iliyomng'oa ubunge wa Igunga, Dk Dallaly Peter Kafumu.
  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Julius Mallaba alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii.

  "Hatuwezi kutangaza kuwa jimbo la Igunga liko wazi hadi hapo tutakapopata nakala ya hukumu hiyo, tumezisikia habari za kutenguliwa ubunge wa mbunge huyo kupitia vyombo vya habari," alisema Mallaba.

  Alisema tume inaweza kulitangaza jimbo hilo kuwa wazi baada ya kuipata hukumu hiyo.
  Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Igunga, kimesema kimeanza kuipitia kwa umakini hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora ili kubaini upungufu uliopo.

  Chama hicho ambacho Dk Kafumu alikuwa ni mbunge wake, kimesema kikibainisha upungufu uliomo kwenye hukumu hiyo, kitakata rufaa.

  Katibu wa CCM wa Wilaya ya Igunga, Mary Maziku alisema wanawatumia wanasheria wao kuipitia hukumu hiyo.
  "Tuna uhakika kwamba tutakata rufaa hivi karibuni baada ya wanasheria wetu kumaliza kuipitia hukumu hii kwa sababu tunataka kuwa na uhakika na uamuzi tutakaouchukua," alisema Maziku aliyekuwa akizungumza kwa njia ya simu.
  Maziku alisema, "tukimaliza kuipitia hukumu hii na siku ya kukata rufaa tutawajulisha lakini haitachukua muda mrefu kuanzia sasa."

  Kauli hiyo imekuja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye kutangaza uamuzi wa chama hicho kukata rufaa kwa sababu ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali.

  Nape alisema chama kimeitafakari hukumu ya kesi hiyo na kujiridhisha kuchukua uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi hiyo.

  Hata hivyo jana, Nape alipoulizwa kuhusu maendeleo ya kusudio la kukata rufaa alisema, "bado nawasiliana na wanasheria wa chama, kwa sasa sina taarifa za kukueleza."
  Hivi karibuni Jaji Shangali alitoa hukumu iliyotengua ushindi wa Dk Kafumu baada ya kuridhishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.

  Dk Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba mwaka jana baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inamaana NEC hawasikilizi redio wala kusoma magazeti?
  Anyway watapata tuu taarifa rasmi.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ysaani nchi hii imeoza sana. Sasa hawana taarifa maana yake nini?
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Makosa yoote yaliyomtoa kafumu yalifanywa na chama na siyo kafumu. Ngoja wamkatie rufaa, inaonekana jamaa anapelekwa kama roboti hata hajielewi.
   
 5. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kwa mwenendo huu hakuna haja ya kuwa doctor (Hivi ni 'Ph. D holder au ni Doctor wa namna gani!)
   
 6. L

  LIBRARY JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  PhD!!!!!!!!:nerd:
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa mbona hawaeleki, wanasema hawajaridhika na uamuzi watakata rufaa, huku wanadai wanasubiri wanasheria wao, which is which?
   
 8. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wastage of time
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania tuna tatizo kubwa sana la watu/taasisi kukaa na kusubiri kila kitu kiletwe kwenye sahani. Tumeona polisi inavyotaka 'muathirika' awe ndio mpelelezi badala ya wao kufanya kazi hiyo, sasa NEC nayo inasubiri iletewe kila kitu. Kama hao wakubwa wamesikia taarifa inayohusu ofisi yao kwenye vyombo vya habari, wameshindwa kitu gani kuwasiliana (kwa barua) na ofisi husika ili wapate barua 'maalum?
   
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Watakata rufaa lakinu yawezekana kwamba wanataka tuu kupunguza facts zilizowadondosha lakini hawawezi kushinda hata chembe
   
 11. i

  iseesa JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usiwatukane Mkuu. Kiutaratibu ni lazima wataarifiwe rasmi na siyo kusikiliza redio na kusoma magazeti.
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimeongeza wasiwasi wangu wa kutoiamini TUME ya UCHAGUZI (NEC) kama ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Nashangaa wanavyosema hawana taarifa za mahakama juu ya utenguzi wa ushindi wa Dr. Kafumu wakati washatkiwa wengine katika kesi ile walikuwa ni Mwanasheria mkuu wa Serikali na msaidizi wa uchaguzi huo (Protace Magavane). Ninamashaka kunakitu kinatengenezwa nyuma ya pazia ili kuleta mizengwe katika hukumu hii.
   
 13. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,243
  Likes Received: 2,925
  Trophy Points: 280
  NEC haraka ya nn
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huwa mnakurupuka bila kusoma? hiki nini?, nimekitoa hapo post #, ngoja nikukuzie labda una matatizo ya kuona:

  "Hatuwezi kutangaza kuwa jimbo la Igunga liko wazi hadi hapo tutakapopata nakala ya hukumu hiyo, tumezisikia habari za kutenguliwa ubunge wa mbunge huyo kupitia vyombo vya habari," alisema Mallaba.
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nape alipokuwa analiongelea kwa nia ya kukata rufaa alishapewa nakala ya kushindwa sio?
  Hatuwezi kuuheshimu utaratibu unaopingana na comon sense.

  Barua rasmi, matokeo rasmi, kauli rasmi huku muda unasonga!
  Iko siku mtashtukia tumefoleni tunataka kuingia bungeni kushiriki maamuzi ya jimbo letu bungeni. Manake hii sheria kipofu haiwezi kuona athari za kutokuwakilishwa bungeni. Sheria inaonekana kuogopa mtu na kupuuza watu.
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  hatuwezi kuvumilia kutokuwakilishwa na muwakilishi halali,

  na bado wanaendelea kuonyesha wanavyotudharau! Kimsingi hawataki, na sheria kukaa kimya, tuwe na mwakilishi wetu.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  wameiomba nakala hiyo kama utaratibu wa mahakama unavyoelekeza?
  Ameonyesha nakala ya barua ya kuomba nakala ya hukumu!
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanini wao waiombe? kwa kusikia magazetini? funguka kidogo!
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli "justice delayed is justice denied" hoja yangu inazidi kuwa kweli,

  "tactic delay"
  hakimu/jaji anaposoma hukumu, hiyo hukumu inamlenga mtuhumiwa, na habari hiyo humuhusu yeyote atakayehusika.
   
 20. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Hivi katika hili ni nani anayeiomba nakala ya hukumu? Chukulia ccm hawana mpango wa kukata rufaa, so hawana kazi na hiyo nakala ya hukumu hivyo wasiiombe Mahakama. Na Chadema ambao ni interested part ktk kesi wao wakaiomba na kupewa, then wakaiwasilisha kwenye Tume ya Uchaguzi. Je, Tume itaipokea na kuifanyia kazi nakala ya hukumu kutoka mikononi mwa Chadema? Kama sivyo, then wao Tume wataletewa na nani hiyo hukumu bila kuiomba? Tujadili kisomi zaidi.
   
Loading...