Elections 2010 NEC: Gazeti latumika kupandikiza uchochezi...................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM lina habari kuu leo isemayo.....NEC: Gazeti latumika kupandikiza uchochezi...................

Habari hii imekuja baada ya gazeti moja linalosadikiwa kuwa ni Tanzania Daima kuandika habari isemayo.............Usalama wa Taifa: Dr. Slaa alishinda uchaguzi kwa 64%.............

Tatizo kwa NEC ni kuwa wapigakura wengi hawana imani nayo na wanaamini ni matunda ya mfumo wa chama kimoja cha siasa ambapo Raisi wa Nchi huteua watendaji na viongozi wake kwa uficho na bila ya kuvishirikisha vyombo vingine vya umma kama kuzitangaza nafasi hizo, kufanya mahojiano ya kuwasaili waoombaji na wateule kuthibitishwa na Bunge..................

Vile vile ushiriki wa Idara ya Usalama wa taifa katika kufuatilia matokeo ya kura nao unatilia mashaka kuwa malengo yao huwa nini kwa sababu hizo siyo moja ya majukumu yao kuingilia NEC katika kusimamia chaguzi zetu.........................

Haya yote huenda ndiyo yanasababisha hisia za kuwa chaguzi zetu siyo huru na wala siyo za haki........................
 
NEC wasisingizie gazeti, ni serikali yao na wao wenyewe kuonyesha waziwazi kuwa walikipendelea chama tawala kwenye uchaguzi uliopita. Kibaya zaidi ni kushirikisha vyombo vya Dola katika kutekeleza azma ya CMM ya ushindi ni lazima. Hiki ndicho walichokipanda hivyo wasiogope kivuli chao wenyewe, walikubali kutenda kinyume na maadili hawana budi kukubali matokeo yake.
 
O Campo Njoo Bongo. hata km hatukupigana lkn waliochakachua KURa wapelekwe the HAGUE. km kuna gazeti SILIPENDI ni UHURU
 
Mkuu ukinitajia NEC nasikia kich..f.ch..f, yaaaaan nina hasira nao balaaaaa
 
Kwa hiyo NEC wanahitaji nini? Uchochezi uko wapi? wao kama wanadhani ni uchochezi waruhusu mahakama iingilie kati kuchunguza nyaraka zinazohusika ili ionekane ukweli uko wapi! Propaganda hazitawasaidia.
Tanzania Daima wameripoti kitu ambacho wameletewa na source of information. Kama ni za uongo Wao NEC wazikatae au wawaite watoa habari kwa sababu wametajwa katika gazeti na kuwauliza ukweli wa habari walizozitoa. Wasitake kuwafunga watu midomo kwa kisingizio cha uchochezi.
NEC jitokezeni kujitetea kama habari hizi ni za kweli. Msilete propaganda ati.
 
Gazeti leneyewe ni Uhuru, mzao wa mti wa Uchakachuaji. waende kuzimu na NEC yao.
 
NEC WAJIUZULU WEZI WAKUBWA WAMESHIRIKI MAPINDUZI YA KIJESHI YA CHAGUO LA UMMA. SASA KAMA NI UONGO SI WAENDE MAHAKAMANI? WASITUMIE MABAVU NA UDIKITETA. KAMA O CAMPO -ICC WALIVYOSEMA KWA KENYA KWAMBA SUSPECT SIYO TU WALIFANYA CRIME LAKINI PIA WALIKIUKA HAKI ZA BINADAMU. SASA NADHANI MAKAME NA WENZAKE AKIWEMO SHIMBO WALIKIUKA HAKI ZA BINADAMU SIYO CRIME TUU, NI HEKIMA TUU ZA SLAA(PhD) NA CHADEMA ZIMEEPUSHA KUMWAGA DAMU ILA HAKUNA TOFAUTI NA KENYA. MAKAME ATOKE NA ASHITAKIWE ICC
 
Hiyo habari ya tanzania Daima ya Usalama wa Taifa: Dr. Slaa alishinda uchaguzi kwa 64% imewachoma sana walishitaki kwa uchochezi na hapo ndipo tutafaidi watanzania.....
 
kama kuna magazeti yanayochochea chuki hapa nchini, hilo gazeti la chama tawala linaongoza kwani linatoa habari za kuegemea upande mmoja apparently likionekana kuwa liko juu ya sheria kwani hakuna anayeweza kulikemea.
 
Haya bwana NEC,hongereni kwa kuwa na uwezo wa kushika vichwa vya waTZ wajinga na kuwatumia kuiharibu nchi yao wenyewe,lakini kumbukeni,mwisho wa haya yote hautakuwa mzuri sana na mtjutia kwa mnayoyafanya sasa.Kwako mTZ,usikubali kutumika,ushtukiapo kutumika kwako,jinasue na usonge mbele kizalendo kama mtu mpagani aliyeokoka................!!!!!:embarrassed:
 
Jk asijidanganye kuwa wa tz waliumbwa tofauti na wakenya, wanyarwanda, wasudan na wengineo. Binadamu ana mwisho wa kuonewa na ni jukumu la wenye madaraka kusoma hilo ili kuepusha balaa. Nina uhakika siku itafika na sisi tutapunguzana population kama wakenya. Mungu saidia kutu zilizoshika kwenye ubongo wa watawala wajitambue na wachukue hatua zinazofaa. Riz-1 si unamwona Kenyata? mshauri dingi asome alama za nyakati
 
Hivi wadau bado mnasomaga gazeti la UHURU????????????????????????????????????????? Yaani mimi nikiliona hata kichwa cha habari sisomi..........Maana linakifu kama si kuchefua.....Nikilikuta limejichanganya kwenye magazeti au documents zangu..mara moja nalichoma moto
 
O Campo Njoo Bongo. hata km hatukupigana lkn waliochakachua KURa wapelekwe the HAGUE. km kuna gazeti SILIPENDI ni UHURU

Mkuu naona una hasira sana!!Ipo siku Ocampo atatua Bongo kama tusipobadlisha katiba yetu!!!
 
Nec wanajua walichokifanya, maana wafadhili walijitoa mapemaa kwa sababu nec haipo huru,je pesa za kujiendesha wanazitoa wapi?
 
Cham cha MAPINDUZI maana ya hilo neno MAPINDUZI ni nini?
Utawala wa kidemokrasia uliompa ridhaa Dr Slaa kuiongoza nchi UMEPINDULIWA na chama cha MAPINDUZI kupiti general Shimbo na nec.
Vipi jamani bado tu jumuiya za kimataifa zitaendelea kuitambua serikali ya MAPINDUZI ya kijeshi?
Tunaomba Tanzania turejeshewe utawala wa kiraia haraka iwezekanavyo!
.
 
Kwanza angalau NEC wameamka usingizini kwa ndoto zile zile kwamba watanzania nao bado wamlala. Lakini cha msingi NEC watuambie nini kilitokea na ukweli ni upi hata baada ya Dr. Slaa ushahidi wa uchakachuaji kwenye baadhi ya vituo na wao kukiri (Vituo 15).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom