NEC Dodoma, JK akana kumtuma Nape kumwita Lowassa gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC Dodoma, JK akana kumtuma Nape kumwita Lowassa gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Nov 25, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sikuamini macha yangu, nikasoma magazeti mpaka matatu ili nijiaminishe, sasa nimeamini kuwa JK ni msanii wa kutupwa.
  Baada ya Lowasa kujitetea kuhusu Richmond na kufanikiwa kumhusisha JK na Richmond, pia alimtuhumu Nape kwa kumchafua yeye ( Lowasa) bila ushahidi, alifuatia waziri mkuu mstaafu Sumaye ambaye pamoja na maelezo mengine ya kumtetea Lowasa alihoji, tuwafanyeje Nape na Chiligati ikiwa kamati ya maadili itamsafisha Lowasa? aliuliza Sumaye.

  Hii ni kutokana na kwamba hawa akina Nape wameshazunguka nchi nzima kumchafua Lowasa kama bw Lowasa alivyotuambia. Kitu ambacho sikutegemea,

  JK alikadakia kauli ya Sumaye na kusema, watachukuliwa hatua za kinidhamu.
  Sakata hili ni baada ya NEC kukubaliana na pendekezo la CC ya NEC lilisomwa na Pius Msekwa la kuomba suala kujivua gamba lirudishwe ktk kamati ya maadili, hoja ambayo ilipita.

  My take,
  Mbele ya macho yangu, ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka 2011, JK akiwa mgeni Rasmi ktk tamasha Nyimbo za Injili alituambia, Nape anayoyazungumza kuhusu gamba siyo maneno yake mwenyewe bali ya ccm - ndiyo kazi tuliyomtuma.
  Jana alisema kama ikidhihirika ktk kamati ya maadili kuwa Nape alimtuhumu Lowasa Bila kufuata utaratibu wa chama basi atachukuliwa hatua za kinidhamu.

  Ikumbukwe kwamba;

  Hoja mojawapo ya Lowasa na Sumaye ni kwamba, kwa nini suala la Lowasa halikupelekwa ktk kamati ya maadili kama ilivyotaratibu za Chama na badala yake Nape akalikimbiza ktk vyombo vya habari?

  Pili, Ikimbukwe kuwa ktk maelezo ya Lowasa alisema, Mkiti unakumbuka ukiwa nje ya nchi, nilikupigia kukushauri kuwa tuvunje mkataba wa Richmond, wewe ukasema ngoja tusikie ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ambao ndo waliosababisha mkataba usivunjwe?

  Tatu, mkiti unafahamu kuwa hakuna jambo nililofanya ambalo sijakushirikisha, kila kitu unajua.
  Nne, Lowasa akiwa ameshika hansard ya Bunge aliuliza ripoti ya Richmond haijasema nimehusika, ilisema ninapaswa kuwajibishwa kutokana na makosa ya watendaji walioko chini yangu.

  My take 2

  Nini hatma ya Nape Ndani ya CCM?
  Je, tukisema kuwa ccm imefika mwisho huu utakuwa ni ushabiki wa kisiasa?
  Je, Lowasa kufanikiwa kumhusisha JK na Richmond moja kwa moja, JK atapata wapi ujasiri wa kuendeleza zoezi la kuwavua wengine gamba au kupambana na ufisadi.

  Je, kama zoezi la uvuaji wa gamba likihitimishwa kwa staili hii, nini kitawafanya watz wasiichague Chadema 2015?
  je, hoja ya Chadema ya Ufisadi ambayo waliiparamia sasa si itawabakiza magamba kweli.


   
 2. r

  rwazi JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunamshukuru Mungu kwa kutomficha mnafiki.Watanzania tuendelee kusali hakuna mnafiki hata mmoja atakaye bakia kwenye hii serikali bila kujulikana.Leo tunaona gambakuu ni kikwete, aliwahi kusema kuwa hajui Richmond ni nani sasa kaumbuka.

  Chadema songa mbele maana jamaa wkitikiswa wanatikisika mpaka watawaambia watanzania madudu yote wanayoyafanya
   
 3. Mutwale

  Mutwale Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naaaaaapppeee kwisha habari yake! Maskini hawezi kushindana na tajiri bwana! El alianza siasa kabla ya nape kuzaliwa, el amefanya siasa na baba yake nape mzee mosses mnauye!

  Hii ndiyo ccm na huyu ndo jk hajui wala hakumbuki alilo lisema jana! Kama rais is not consistent how is possible serikali iwe consistent?

  Sasa ni wakati wa wapinzani kujiimarisha ili kukabiliana na el katika kinyanganyiro cha urais! Kazi kweli kweli! Kumbe jk alimkataza el asivunje mkataba wa richmond? Je ni kweli jk alikuwa anamfahamu mwenye richmond?

  Tunahitaji rais imara sasa..............
   
 4. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  CCM na JK wake wote ni kaole na ukizingatia kuwa Bagamoyo ndio inakotoka kaole na JK ndio kwao ndipo utakapojua fika kuwa gamba siku 90 wote huu ulikuwa ukaole mtupu solution CCM needs a replacement from CDM and no question about it u can't foul tanzanians that way everybody knew that GAMBA na kukiokoa CCM kwenye mauchafu iliyonayo huu ndio wakati wa kujisafisha.

  Look at it now eti walipeleka suala hili CC for what? Kweli late Nyerere alikufa na chama chake siyo Kigunge, malecela, na wakongwe wa chama ambao wana sauti ya kusema sasa imetosha nobody can do that this is very bad and sad to the who have vested their trust to this party, CCM.
   
 5. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Contradiction nyingine, JK alisema hajui Richmond, sasa mbona jana hajamwambia Lowasa kuwa yeye hajui Richmond? Mbona hakukana? Je, Dr Slaa alikuwa sahihi kwamba Richmond ni ya JK.
  Je, kama Rais ni mwongo, ataongozaje nchi?
   
 6. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe gamba kuu ni kikwete, ha ha ha hah hah, kweli mungu mkubwa.

  My take;
  Nape ataificha wapi sura yake?
   
 7. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Na kama ccm wanakitaka chama bac wamsimike EL kama mgombea wake kwani wananchi hamtaki only a fraction of who haves and majority who do not are not favorite to EL but to CDM.
   
 8. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi na bwana mkubwa hatukukutana barabarani, taratibu ukweli utajulikana tu.
   
 9. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mh Rais,

  Pamoja na kuwa umekuwa ni mtu wa safari za nje lkn naamini kuna kipindi unakuwa angalau kwenye ardhi ya Tz, ingawa inawezekana muda mwingi unatumia kusafiri nje ya nchi.

  Tukirejea kwenye kikao cha NEC tuliona angalau hoja za msingi za MH. Lowassa, si kweli kuwa aliyokuwa anafanya Nape na Chiligati dhidi ya Lowassa hujui, tena kuna baraka za mkono wako. Haiwezeakni watu hawa uwliowatuma kufanya kazi uwakane eti kuwa hukuwatuma, tabia ya kutojiamimni na kufanya mambo kwa kujifcha ficha ndo iliyozaa seriakli legelege, si kweli kuwa watu wawili ndani ya CCM ndo wachafu ungekuwa na busara hata wewe ulipaswa kuvuliwa gamba.

  Nakubaliana na Lowassa kuwa hakuna alilokuwa anafanya kama waziri mkuu ambalo hujui ni jambo la ajabu na fedheha kuwa mara kadhaa rais anatamka hadharani haijui Richmond/dowans, ni bora kunyamaza kuzungumza kuliko kutoa kauli zisicho na maana kabisa kwa watz.

  Tabia ya kufanya kazi kwa tetesi za mitaani hazitaifikisha serikali hii dhaifu kokote.

  Nawasilisha
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JK ni bingwa wa "divide and rule".NAPE ajitafakari,aachie ngazi.
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Aweda kwani ulikwa hujui kwamba damu ya wana wa Tarime , Geita na kokote waliko wachimba madini zimwi behind ni JK ? Ruswa na uroho wa kutafuta madaraka JK alianza zamani sana sana leo unashangaa richmond? Je IPTL ?

  JK is never clean na CCM wanajua na watanzania walishindwa kujimbua na kumtumainia. JK akiwa waziri wa nje alikuwa anapida deals kwemye Limosine toka London hadi London Gatwick na wahindi kisha weka sahihi. Ndiyo maana Karamagi alikuwa anatembea na mihuri si yeye wa kwanza kufanya hayo .
   
 12. j

  jigoku JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Unafiki ni sehemu ya utaratibu wa kawaida sana wa CCM.kwa hiyo msishangae
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  NINGECHANGIA ILA SIYAPENDI MAGAMBA KWA WIZI WAO! wacha yafe tuu!
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  kwamba kumbe alishauriwa mkataba wa richmond uvunjwe wakati hakuna madhara, sasa umevunjwa unaligharimu taifa billions!! kwamba hajui dowans lakini alishaulizwa kuvunjwa kwa mkataba na kampuni iliyoozaa dowans!! sitaki kuamini tunaye rais muongo!!!
   
 15. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ****** fani yake ngoma na kujaza dunia, haya mengine mnamsingizia tu
   
 16. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  ROBOT features
   
 17. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Taratibu kila kitu kitakuwa hadharani. Ikumbukwe kuwa , JK akitoka madarakani mengi zaidi yatajulikana.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Je mpaka hapo wa-tz mtaendelea kumwita EL fisadi? Jk ndio------
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kweli kama aibu leo Kikwete kaumbuka kiutu uzima,
  ..alisema maneno ya Nape ni ya chama leo anajidai hajui
  ..alisema haitambui Richmond na mmiliki wake leo ambaye hawakukutana barabarani kamwambia yeye anajua kila kitu
  ya jana ni 10% tu nasikia kuna mengi pamoja na rais wetu kutishia kujiunga na upinzani asingepitishwa kugombea urais duh my president.

  Aibu aibu kwa rais wangu.
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Jk uwezo wake ni mdogo sana, japo watu wanadai ana CV ndefu lakini hawataki kusema kafanya nini kila alipopitia. Inakuwaje alipata ushauri wa Makatibu wakuu na asiwajue Richmond??
   
Loading...