Vyama vyote vya Siasa vinapata fedha ktk Serikalini ili kujiendesha, hivyo kwa kuwa tunavilipa pia vina jukumu la kushiriki chaguzi zote zilizoko kisheria, hivyo kwa maoni yangu Chama ambacho kinasusia Uchaguzi kilazimishwe kurudisha fedha zetu za ruzuku, hata sehemu tu ya fedha zetu irudi hazina, ...
Wengine wanasusia kwa sababu ile pesa ya ruzuku inanyakuliwa kama mwewe anavyonyanyua kifaranga na haikai hata wiki moja. Kwanza kumlipa mwenyekiti pesa aliyokikopesha chama kwenye uchaguzi mkuu. Pili kumlipa mjumbe wa kamati kuu milioni kama mia mbili kwa kukiongezea chama idadi ya wabunge na hivyo kuongeza ruzuku. Hapo bado mishahara, pango, umeme nk. Kutabaki pesa ya uchaguzi mdogo hapi?