NEC: Chama cha Siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe! Tume haiko kushawishi chama kushiriki

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,012
2,000
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amesema chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe kwa kuwa haiko kumshawishi mtu au chama kushiriki.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 12,2017 jijini Dar es Salaam, Kailima amesema chama kushiriki uchaguzi ni jambo la hiari na NEC ipo kwa ajili ya kuweka na kutengeza mazingira yatakayofanya vyama vya siasa kushiriki uchaguzi.

Kailima katika taarifa iliyotolewa na NEC amesema iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi, kitakachoshiriki hata kama ni kimoja mgombea wake atapita bila kupingwa.

“Ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” amesema alipozungumza na waandishi wa habari waliotaka ufafanuzi wa NEC kuhusu tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.


Rejea hapa matamko hayo ya UKAWA juu ya kujitoa kwenye Uchaguzi; UKAWA na CHAUMMA wasema hawatashiriki uchaguzi mdogo ujao hadi kasoro zilizojitokeza uchaguzi uliopita zitatuliwe


Kailima ameviasa vyama vya siasa vinavyotishia kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na kata sita Januari 13,2018 kufuata mifumo ya kisheria ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi.

Juzi Mbowe alitishia kuwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) havitashiriki uchaguzi iwapo changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 Novemba 26,2017 hazitafanyiwa kazi na NEC.

Akizungumzia hoja hiyo, Kailima amesema katika orodha ya vyama vilivyopo NEC, Ukawa si moja ya vyama vya siasa.

“Niwasihi vyama vya siasa watumie mifumo iliyopo ya kawaida ya kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili; kujaza fomu namba 14 kabla ya kura kuanza kupigwa; fomu 16 wakati kura zinapigwa; na kuwasilisha malalamiko mahakamani baada ya kura kuhesabiwa,” amesema Kailima.

Amesema hiyo ndiyo mifumo iliyowekwa kisheria katika kushughulikia changamoto za uchaguzi zinapojitokeza na kuhoji wanayotaka wao ni ipi.

“Kama kuna mgombea hakuridhika mahakama zipo aende maana wamepewa siku 30 za kufungua kesi,” amesema.

Amesema NEC haiwezi kuahirisha uchaguzi kwa kuwa sheria inatamka kuwa uchaguzi unaweza kuahirishwa iwapo tu kuna mgombea amefariki; kutokuwepo mgombea; zikitokea ghasia na fujo au wagombea wakifungana kwa kura.

“Je kuna mgombea amefariki? Haya mambo yote manne hayajatokea, sasa tutaahirishaje uchaguzi?” amehoji Kailima.

Kuhusu jimbo la Longido ambalo Mbowe alidai shauri la uchaguzi bado liko mahakamani na wameiandikia NEC kuhusu suala hilo na barua kutojibiwa, Kailima amesema madai hayo si ya kweli kwa kuwa barua zote walizoandikiwa wamezijibu.

Amesema jimbo hilo liko wazi kwa kuwa Mahakama ndiyo imeiandikia NEC kuitaarifu kumalizika kwa kesi iliyokuwepo mahakamani.

Kailima amesema NEC itasimamisha uchaguzi wa jimbo hilo iwapo tu Mahakama itawaeleza wasimamishe mchakato huo.

“Nimesikitishwa na kauli kwamba eti wametuandikia barua sisi Tume ya kusimamisha uchaguzi wa Longido eti hatujawajibu. Tulipata barua kutoka kwa ole Nangole (Onesmo) tukamjibu, tukapata barua kwa wakili wa Ole Nangole nikamjibu; tukapata barua kutoka kwa katibu wa Chadema tukamjibu na nikaongea naye kwenye simu, sasa leo wanaposema hatujawajibu kwa kweli kauli hiyo imenisikitisha,” amesema.

CHANZO: Mwananchi
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,371
2,000
Kwani hao ukawa walipokuwa wanashiriki walipoka haki ya vyama vingine kupata kura mpaka useme leo ni fursa kwao?
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,298
2,000
Ameambiwa arekebishe kasoro ili hivyo vyama vishiriki. Sijamsikia akizungumza kurekebisha hizo kasoro. Hata mpirani unachezaje na yimu iliyokuja na refa wao, sheria zao,mpira wao, uwanja wao halafu utegemee ushindi?

DED ndio returning officer wa uchaguzi. Leo anaonekana katika mkutano wa CCM sasa unategemea atatangaza matokeo ya aina gani?
 

Elevat Kapela

JF-Expert Member
Dec 9, 2017
526
1,000
Ni bora kususia kuliko kuendelea kuwatia watu ukilema. Yawezekana mleta mada hukuwa field wakati uchaguzi huu unafanyika. Tuliokuwa field tumeona mengi ambayo hata nikiyaandika hapa kesho nitaitwa mchochezi. Kwa kifupi tumepigwa mbele ya vyombo vya usalama. Tumevurugiwa uchaguzi kabisa. Pia tunatumia gharama kwenye chaguzi Siku ya mwisho anatangazwa aliyeshindwa kuwa mshindi. Tuliokuwa kwenye maeneo ya uchaguzi tumeelewa maazimio ya kamati kuu ambao hamkuwa sight hamuwezi kuelewa. Sasa rafiki zangu tuliokuwa nao field wanauguza vidogo na cha kusikitisha kabisa kuna mwanachama wenzangu alikatwa pango na uvccm na cha ajabu yeye yuko ndani na aliyemkata panga yuko nje anapeta.
wewe kalime nyanya usijifanye sehemu ya viongozi wa kisiasa wakati kapuku.
 

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,310
2,000
...Sijamsikia akizungumza kurwkebisha hizo kasoro. Hata mpirani unachezaje na yimu iliyokuja na refa wao, sheria zao,mpira wao, uwanja wao halafu utegemee ushindi?

DED ndio returning officer wa uchaguzi. Leo anaonekana katika mkutano wa CCM sasa unayegemea atatangaza matokeo ya aina gani?
Na wewe hebu rekebisha kwanza hizo kasoro za kiuandishi hapo.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,326
2,000
Sababu walizotoa Chadema kugomea Uchaguzi zitaendelea kuwepo mpaka 2020, na tunategemea hazitofanyiwa Marekebisho yoyote hivyo hatutegemi Kama watagombea!


Serikal yetu ingeiga tangazo la Serikal ya Venezuela Jana ilitangaza ukisusia Uchaguzi maana yake umehalalisha Chama hicho kutoshiriki Tena Uchaguzi wowote wa baadae!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom